MASIKINI ADAM KUAMBIANA, ALIJUA KIFO CHAKE AKAJIANDAA LAKINI ALICHELEWA! KILICHOMUUA KIKO HAPA, KUAGWA KESHO LEADERS NA KUZIKWA KINONDONI

KWELI kifo hakina huruma! Msemo huu umetimia juzi kufuatia kifo cha ghafla cha mwigizaji na mwongozaji wa filamu za Kibongo, Adam Philip Kuambiana (38) kilichotokea akiwa njiani kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.Kuambiana aliugua ghafla kwenye kambi ya kurekodi filamu na wasanii wenzake iliyopo katika Nyumba ya Kulala Wageni ya Silvarado iliyopo Sinza ya Kwaremmy, Dar.Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ alisema muda mchache kabla ya kufikwa na mauti,  Kuambiana alimlalamikia maumivu ya tumbo ambapo Ijumaa iliyopita alisema hali yake si nzuri kwani alikuwa akiendesha damu tupu.




Q-Chillah alisema:
 Jana (Ijumaa) jioni Kuambiana na wasanii wenzake walikuwa baa wakinywa pombe hadi usiku mnene lakini bado aliendelea kulalamikia maumivu ya tumbo.

Wenzake walimuuliza ni kwa nini alikuwa akiendelea kunywa pombe kama anaumwa? Akawaambia wamuache!
Baada ya kumaliza kunywa kila mmoja alikwenda kulala chumbani kwake huku tukiahidiana kwamba itakapofika saa 3:00 asubuhi tuwe tayari kwa ajili ya kwenda ‘location’.
Lakini ulipofika muda huo sisi tukiwa tayari kwa safari tulikwenda kugonga mlango wa chumba chake bila mafanikio.
Cha kushangaza, alisikika sauti yake kwa mbali. Kwa bahati nzuri mlango ulikuwa wazi, mmoja akaingia ndani na kumkuta ameanguka chooni na hajiwezi. Neno lake la mwisho alisema kwamba anajisikia kuishiwa nguvu na anaharisha damu.
Kutokana na hali yake hiyo mbaya tulimbeba na kumlaza kitandani kisha tukatafuta gari na kumkimbiza Hospitali ya Mama Ngoma ambapo daktari alisema kwamba alishafariki dunia muda mrefu.
Kwa mujibu wa watu wa karibu, Kuambiana kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo (ulcers). Lakini pia inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na kisukari (diabetes).
Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (aliomba jina kuhifadhiwa)alisema:
 Kwa kawaida, mtu kuharisha damu kwa sababu ya vidonda vya tumbo inawezekana kabisa, hiyo kitaalam inaitwa heamatemesis. Inatokana na perforation ya tumbo yaani kidonda kuwa kikubwa.
 Kwa mtumiaji wa pombe ni kipindi anatakiwa kusimama au kuacha moja kwa moja. Kama hatajali afya yake anaweza kufa ghafla kwani uwezekano wa utumbo kukatika ghafla ni mkubwa.
Q-Chilla ambaye ni miongoni wa wasanii wanaocheza filamu hiyo, aliendelea kusema kuwa siku chache kabla ya kifo, Kuambiana alimwambia filamu yake hiyo inayoitwa Jojo ndiyo ya mwisho, hatajishughulisha tena na sanaa na alikuwa na mpango wa kwenda China kupumzika kwa muda mrefu.
 Nimeumia sana kwani hii filamu ndiyo ilikuwa apate fedha nyingi sana kwa sababu ni ya kwake mwenyewe na ni kali mno, amecheza vizuri akinishirikisha mimi.

Lakini ndiyo hivyo tena imeishia katikati, sijui ni nani atakayeiendeleza maana mwenyewe katuachia majonzi yasiyoelezeka
 alisema Q-Chillah.
Habari zaidi zinasema kwamba, Kuambiana ameaga dunia hata arobaini ya mdogo wake wa damu, Patrick  haijafika. Patrick alifariki dunia mwezi mmoja uliopita.
Baada ya taarifa kuenea, wasanii mbalimbali wa filamu walikusanyika katika Hospitali ya Mama Ngoma ambapo Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ walivunja rekodi ya kulia kufuatia kifo hicho.
Wadau na mashabiki wa filamu waliokuwa eneo hilo walisikika wakisema kwamba wasanii wengi hawana tabia za kucheki afya zao, jambo ambalo linawagharimu kiasi cha kupoteza maisha.
Wengine walisikika wakisema kwamba watu wanaoanguka chooni mara nyingi huwa hawaponi, wakipona huwa wanapooza miili.
Unajua watu wengi wanakosea, pale mtu anapodondoka chooni wanamkimbiza hospitali badala ya kumtibu kienyeji, mtu akianguka  chooni tu anatakiwa kupewa ndizi mbivu lakini akipelekwa hospitali lazima afe
walisikika watu.
Marehemu Kuambiana alizaliwa mwaka 1976, Ifunda mkoani Iringa. Kabila ni Mmakua wa mkoani Mtwara

Comments

Popular posts from this blog