UKAWA WAPATA PIGO MKOANI IRINGA.....WAPOKELEWA KWA MABANGO YA KUWAPINGA, MKUTANO WAGUBIKWA NA VURUGU KUBWA
UMOJA
wa Katiba ya Wananchi ( UKAWA ) umepokelwa kwa mabango
yanayowapinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa yaliyokuwa
yamebebwa na vijana.... Mabango
hayo yalikuwa yanasomeka kuwa, "Tuna mashaka na ndoa ya UKAWA
watauza nchi", huku yakisisitiza umuhimu wa vijana wa Wilaya ya
Mufindi kutaka Serikali mbili.....
Pia mabango hayo yalikuwa yanawataka wajumbe wa UKAWA warudishe posho kwanza bungeni mjini Dodoma....
Katika
mkutano wao uliofanyika juzi mjini Mafinga Viwanja vya mashujaa,
mkutano huo uliendeshwa na mwenyekiti wa chama cha Wananchi (
CUF ) ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA.....
Wengine
waliohutubia ni pamoja na mwakilishi wa chama cha
NNCR-Mageuzi,Danda Juju na kiongozi wa taasisi ya kiislam ya
Shura ya Imamu,Rajabu Katimba.
Baadhi
ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na vijana hao wilayani Mufindi
yalikuwa na ujumbe uliosomeka: "Vijana Mafinga tuna mashaka na
ndoa ya UKAWA,watauza nchi" na bango la waendesha bodaboda
lilisomeka: "Rudisheni posho kwanza mjengoni Dodoma"
Mengine
na ujumbe wake kwenye mabano ni lililowatambulisha
wafanyabiashara wa sokoni lililosomeka, "Mafinga Sokoni,Serikali
tatu siyo suluhisho la matatizo ya wananchi", na la wapiga debe
mafinga stendi lilisomeka, "Karume Oyee, Nyerere Oyee, Muungano
Saafi!".
Bango
la waliojitambulisha kuwa ni machinga lilisomeka,"Tunataka
Serikali inayojali wajasiriamali, siyo kujali matumbo yao"...Na
lile la wakulima lilisomeka, "Kilimo Kwanza, Utaifa kwanza".
Wakati
mabango hayo yakizungushwa katika mkutano huo muda ambao Profesa
Lipumba alikuwa akihutubia, usikivu ulipotea kwa takribani
dakika 15 hadi 20 baada ya sehemu ya kundi la vijana
lililokuwa likimsikiliza kuelekea upande walikokuwa vijana wenye
mabango hayo....
Polisi
waliokuwepo walilazimika kuingilia kati kadhia hiyo na mzozo
huo baina yao na vijana waliokuwa na mabango ulisikika....
Mmoja
wa polisi aliyekuwa akiwatuliza vjana hao alisema,"Jamani huu
ni mkutano halali wa kisiasa, acheni wenzenu wafanye mkutano
wao, yatoeni mabango yenu"
Mmoja
wa vijana aliyekuwa amebeba bango mojawapo jina halikupatikana
mara moja alisikika akisema, "UKAWA siyo chama cha siasa, wao
wanamtazamo wao na sisi tuna mtazamo wetu, kwa hiyo siyo jambo
la ajabu wakajua kwamba Mafinga wengi hatuwaungi mkono na siyo
dhambi kuonyesha hisia zetu katika mkutano wao"
Akielezea
vurugu hizo, profesa Lipumba alisema zinafanywa na vijana
waliotumwa na CCM kwa sababu ya msimamo wao wa kutaka serikali
mbili, tuhuma zilizokanushwa na katibu wa CCM wilaya ya
Mufindi,Miraji Mtaturu aliyehojiwa baada ya mkutano huo...
"Siamini
kama mkutano huu ungekuwa unahutubiwa na mwenyekiti wa CCM wa
taifa Jakaya Kikwete wangekuja na mabango yao na kufanya
vurugu hizi," alisema Lipumba na sauti toka kwa baadhi ya
vijana hao zikasikika zikisema, "Kama angekuja na msimamo wa
serikali tatu ni lazima angekutana na mabango haya, sisi
tunataka serikali mbili"
Hata
baada ya vurugu hizo kutulia na Profesa Lipumba kuruhusu
maswali baada ya kufafanua sababu mbalimbali zilizowafanya
wasusie bunge la katiba na kuanzisha UKAWA, mkutano huo ulitaka
kuvurugika tena....
Swali
liliotaka kuuvuruga mkutano huo lilitoka kwa kijana
aliyejitambulisha kwa jina la Rahid Rashid ambaye alitaka kujua
kwa nini CCM hawapo katika umoja huo.
Pamoja
na vijana wengine kupiga kelele wakiashiria kuwa hilo siyo
swali,Profesa Lipumba alijibu na kusema hilo ni swali zuri.
Alisema
milango ya UKAWA ipo wazi kwa mtu yeyote ndani na nje ya
bunge la katiba wakiwemo wabunge na viongozi wa CCM
"Tutafurahi
kuwapata wana CCM,tunawakaribisha UKAWA ili kwa pamoja
tushirikiane kupata katiba inayotokana na wananchi,"alisema
Mwingine
aliyeuliza swali alikuwa Winfrida Ngoti aliyesema harakati za
kudai serikali tatu hazitakuwa na maana yoyote kama matatizo
ya wananchi hayatashughulikiwa.
"Watanzania
wana matatizo lukuki,vituo vya huduma za afya havina
wataalamu,dada,wakulima hawapati pembejeo kwa wakati na bei zake
ni kubwa, wafanyabiashara wadogo wanabanwa na kukamuliwa kodi,
walimu haapati mishahara kwa wakati, askari wana mishahara midogo
," alifafanua
Katika majibu yake, profesa Lipumba alisema hayo yote yatafanyiwa kazi kukiwa na katiba bora itakayosisitiza uwajibikaji na uadilifu
Comments
Post a Comment