HII STORI YA MAISHA YA MWIGIZAJI MASANJA INAWEZA KUKUTOA MACHOZI
Masanja Mkandamizaji si jina geni masikioni mwa watu wengi kutokana na uwezo wake wa kuwavunja mbavu watazamaji pale anapoonekana katika runinga na Kundi la Original Comedy.
Licha ya kufika hapo alipo sasa, anakiri wazi kuwa amepitia katika maisha magumu hususani wakati alipoamua kuanza maisha binafsi ya kujitegemea baada ya kutoka nyumbani kwa dada yake alipokuwa akiishi.
Anasema kabla ya kuondoka kwa dada yake alimuomba amtafutie chumba ili ajitegemea na kuanza maisha binafsi kama kijana . Nilimwambia dada anitafutie chumba na alifanya hivyo ingawa alikuwa anahofia kama nitaweza ,basi nikapata 'geto' langu maeneo ya Tabata Aroma na nilitakiwa kulipa kodi ya TSh. 5,000 kwa mwezi, anasema Masanja. Anakiri wazi kuwa changamoto katika maisha ndizo zilizochangia kumfikisha mahali alipo sasa kwani licha ya kuwa katika hali ngumu
Hakukata tamaa bali alizidi kujituma kwa nguvu zake zote. Anasema kuna wakati ilikuwa vigumu kuipata hata hiyo hela ya kodi kwahiyo ilikuwa inamlazimu kurudi kwa dada yake kwa muda unapofikia wakati kulipa kodi. Yaani hiyo TSh. 5,000 kuipata ilikuwa shughuli maana ilikuwa ikifika karibu na mwisho wa mwezi narudi kwa dada kuzuga kidogo ili mama mwenye nyumba ajue nimesafiri,anasema. Anasema alianza kwa kulala chini mpaka siku alipofanikiwa kupata fedha kidogo iliyomuwezesha kununua godoro la sufi jambo ambalo anajivunia nalo kwani aliweza kununua kwa jasho lake.
Anaongeza kuwa kamwe hawezi kumsahau marehemu Steven Kanumba pamoja na mtu mwingine aliyemtaja aitwaye Mtitu kutokana na mchango wao uliosaidizi kumfikisha hapo alipo sasa.
“Namshukuru sana marehemu Kanumba alikuwa anakuja kunichukua kule Tabata tunaenda kupiga 'inshu' ambazo zilikuwa zikiniingizia pesa kidogo iliyoniwezesha kuishi hata hivyo maisha yalikuwa magumu. Wakati naanza maisha sikuwahi kutoa hela hata ya kununua chipsi kavu lakini siku moja nilifanya kazi na Mtitu ambayo alinilipa laki moja sikuamini macho yangu, kwa mara ya kwanza kununua chipsi kuku kwani nilikuwa nikitamani mlo huo nililazimika kusaidia kumenya viazi kwa washikaji” alieleza Masanja.
Sambamba na uchekeshaji Masanja pia amejiingiza katika shughuli za kumtukuza Mungu baaada ya kuokoa na sasa anafanya vizuri pia katika uimbaji wa nyimbo za injili na kesho Jumapili atazindua albamu yake ya pili ya muziki wa Injili inayoitwa Hakuna jipya chini ya jua.
-via bongo movies
Comments
Post a Comment