Posts

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA NYUMBA ZA MAKAZI ZA NHC MINDU UPANGA DAR ES SALAAM

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe uzinduzi wa jengo la nyumba za makazi za NHC Mindu, Upanga Jijini Dar es Salaam Oktoba 7, 2015 zilizojengwa na NHC na kuuzwa kwa wamiliki . Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Zakhia Meghji na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi . Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la ufunguzi la jengo la nyumba za makazi za NHC Mindu, Upanga Dar es Salaam zilizojengwa na NHC na kuuzwa kwa wamiliki. Wanaoshuhudia nia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Zakhia Meghji  Jengo la nyumba za makazi za NHC Mindu, Upanga Dar es Salaam zilizojengwa na NHC na kuuzwa kwa wamiliki linavyoonekana. Baad

KINANA APIGA KAMPENI YA NGUVU VISIWA NANSIO UKEREWE

Image
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye eneo la mkutano wa kumnadi mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye visiwa vya Nansio Ukerewe.  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nansio kwenye mkutano wa kumnadi mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye visiwavya Nansio Ukerewe. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nansio waliojitokeza kwa wingi kwenye eneo la mkutano wa kumnadi mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli,Ukerewe.

SAMATA: TUNGEKUWA MAKINI TUNGESHINDA KWA IDADI KUBWA YA MAGOLI

Image
Mbwana Samata Baada ya kufanikiwa kuifungia Stars goli moja kwenye ushindi wa goli 2-0 ilioupata Stars ikiwa nyumbani dhidi ya Malawi, Mazembe Mbwana ambaye ni nyota wa Tanzani anaecheza TP Mazembe amesema, kama wachezaji wa Stars wangekuwa makini basi wangeweza kufunga magoli mengi zaidi kwenye mchezo huo. Samata amesema ilikuwa ni rahisi kupata magoli mengi hasa kipindi cha kwanza lakini Malawi walirudi tofauti kipindi cha pili. Samata ameongeza kuwa, Stars inaweza kufuzu kwa hatua inayofuata kwasababu anaamini walimu wameona makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa Jumatano na watafanya marekebisho kabla ya mechi ya marudiano siku ya Jumapili itakayochezwa nchini Malawi. “Kama tungekuwa makini, tungeweza kushinda kwa idadi kubwa ya magoli lakini sijui tulikuwa na uoga wa kudhani mechi inaweza kuwa ngumu zaidi ya ilivyokuwa. Kipindi cha pili jamaa wakaja wamebadilika kwasababu walikuwa wanaona kwamba matokeo yanaweza kuwa mabaya zaidi kwao”, amesema Samata