SAMATA: TUNGEKUWA MAKINI TUNGESHINDA KWA IDADI KUBWA YA MAGOLI


Mbwana Samata
Baada ya kufanikiwa kuifungia Stars goli moja kwenye ushindi wa goli 2-0 ilioupata Stars ikiwa nyumbani dhidi ya Malawi, Mazembe Mbwana ambaye ni nyota wa Tanzani anaecheza TP Mazembe amesema, kama wachezaji wa Stars wangekuwa makini basi wangeweza kufunga magoli mengi zaidi kwenye mchezo huo.
Samata amesema ilikuwa ni rahisi kupata magoli mengi hasa kipindi cha kwanza lakini Malawi walirudi tofauti kipindi cha pili. Samata ameongeza kuwa, Stars inaweza kufuzu kwa hatua inayofuata kwasababu anaamini walimu wameona makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa Jumatano na watafanya marekebisho kabla ya mechi ya marudiano siku ya Jumapili itakayochezwa nchini Malawi.
“Kama tungekuwa makini, tungeweza kushinda kwa idadi kubwa ya magoli lakini sijui tulikuwa na uoga wa kudhani mechi inaweza kuwa ngumu zaidi ya ilivyokuwa. Kipindi cha pili jamaa wakaja wamebadilika kwasababu walikuwa wanaona kwamba matokeo yanaweza kuwa mabaya zaidi kwao”, amesema Samata ambaye alifunga goli la kwanza wakati Stars ikiibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Malawi.
“Ilikuwa rahisi kupata magoli mengi kipindi cha kwanza, lakini tushukuru kwa ushindi huu tulioupata kwasababu hii ni game huwezi jua, tuache tu ushindi ubakie hivyo”.

“Nadhani hata kwa goli hizi mbili nadhani wanashukuru wanadhani wanawea wakabadili matokeo wakiwa kwao. Lakini sisi tunaweza ku-qualify, nafikiri walimu wameona wapi tunatakiwa kurebisha na kupata matokeo mazuri Jumapili tukiwa Malawi”.

Comments

Popular posts from this blog