DONGOBESH FC YAICHAPA STAND FC YA HAYDOM GOLI 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KURUGENZI CUP 2018
Mchezaji wa timu ya Dongobesh FC Antipas Vicent akiwa amebebwa juu juu na mchezaji mwenzake mara baada ya kumalizika kwa mchezo katika yake na timu ya Stand FC ya Mjini Haydom ambapo mchezaji huyo ndiye aliyeifungia timu yake goli 1-0 na timu ya Dongobeshi kufanikiwa kuingia nusu fainali katika michuano ya Kurugenzi Cup 2018 linaloandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom.ikidhaminiwa na Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha Iringa, na benki za NMB na CRDB. Wachezaji wa timu ya Dongobash FC wakisikiliza maelezo ya Mmoja wa Waratibu wa michuano hiyo Bw. Phars Nyanda wakati akiwapa utaratibu mara baada ya mchezo huo kumalizika. Benchi la Ufundi la Timu ya Dongobesh FC likinyanyuka juu na kushangilia mara baada ya kuifunga timu ya Stand FC ya mjini Haydom katika mchezo uliofanyika leo jioni kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom. Golikipa wa timu ya Stand...