Posts

Breaking News: Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini Ajiuzulu

Image
HATIMAYE Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ametangaza kujiuzulu urais wa nchi hiyo usiku huu ikiwa ni siku chache baada ya chama chake cha ANC kuanzisha vuguvugu la kumng’oa madarakani. Akitangaza uamuzi huo, Zuma amesema asingependa damu imwagike na chama(ANC) kimeguke kwa sababu yake. ANC kikiongozwa na Cyril Ramaphosa, siku chache zilizopit kilituma ujumbe maalum kumtaka rais huyo kuachia madaraka, kutokana na harakati nyingi za kumtaka afanye hivyo tangu mwaka jana. Jacob Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ambapo Bunge la nchi hiyo kujaribu kupiga kura za maoni ili kumuondoa lakini ilishindikana, ndipo chama kikafanya mkutano na kuchukua uamuzi huo mgumu wa kumtaka afanye hivyo, la sivyo kitamtoa kwa nguvu. Zuma amefuata nyayo alizopita rafiki yake mkubwa Robert Mugabe ambaye alikuwa Rais wa Zimbabwe, aliyetakiwa kufanya hivyo mwishoni mwa mwaka 2017 na jeshi la nchi hiyo, la sivyo lingetumia nguvu kumng’oa, na hatimaye kuac

Zari Atangaza Rasmi Kuachana na Diamond

Image
IKIWA ni siku ya wapendanao,  leo Februari 14, 2018, Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari the Boss Lady ametangaza kuvunja rasmi mahusiano yake ya kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Kupitia ukurasa wake wa Instagaram, Zari amefunguka kuwa kilichompelekea kufanya hivyo ni kutokana na Diamond kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao huku akibainisha kuwa kuachana katika mahusiano ya kimapenzi hakutaathiri uhusiano wao kama wazazi. Diamond ambaye alianza mahusiano na Zari takribani miaka mitano iliyopita baada ya kuachana na staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu, amezaa na Zari watoto wawili ambao ni Tiffah na Nilan huku pia akitajwa kuchepuka jambo ambalo limepelekea akazaa mtoto mwingine na mwanamitindo Hamissa Mobeto. Mbali na Mobeto, Diamond amekuwa akihusishwa kurudiana na Wema ambapo hivi karibuni walionekana kugandana kwenye hafla ya kutambulishwa kwa msanii Mbosso kwenye lebo ya WCB Wasafi.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 15.02.2018

Image
                                     

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image
             

Fangasi Sehemu za Siri za Mwanaume

Image
Watu wengi wanaamini kuwashwa sehemu za siri kunasababishwa na fangasi tu, ndiyo maana nimepata maswali ya wasomaji juu ya matibabu na jinsi ya kujikinga na fangasi kwa kuwa wanaamini muwasho unaowasumbua kwa muda mrefu ni matokeo ya maambukizi ya fangasi. Watu wanapaswa kufahamu kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani ndani ya mwili wako pengine isiwe ni fangasi na ikawa ni mzio (allergy) tu. Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe kitu hicho kikiondolewa. Kuondolewa kwa kitu hicho kunatia ndani matibabu sahihi na kuendelea na njia bora za kujikinga kutopata maambukizi tena. Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi. Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari. Kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu kunaweza sababisha ugonjwa kusambaa mwilini na kuongeza hatari ya kifo. Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri za Mwanaume? Kuwashwa uume au sehemu zingine za s

Katibu wa Bunge Azungumzia Afya ya Spika Job Ndugai

Image
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema hali ya afya ya Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyepo nchini India inaendelea vizuri. Kagaigai amesema leo Februari 14,2018 kuwa Spika Ndugai yupo India kwa ajili ya kuangalia afya yake (check-up) na anatarajiwa kurejea nchini wakati wowote. Katibu huyo wa Bunge amesema, “Tulikwisha kusema kwamba Spika yuko India kwa ajili ya ‘check-up’ na hali yake inaendelea vizuri.” Alipoulizwa kuwa Spika atakuwa ughaibuni hadi lini, Kagaigai amesema: “Hilo ni kati ya daktari wake na yeye lakini ninachoweza kusema wakati wowote anaweza kurudi nchini.”

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO IKULU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu mara baada ya kufanya nae mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu mara baada ya kufanya nae mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni mtoto wa Profesa Mahalu ambaye ni Mwanasheria wa Kijitegemea Jaja Costa Mahalu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mtoto wa Profesa Mahalu ambaye ni Mwanasheria wa Kijitegemea Jaja Costa Mahalu mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Mama Diamond Ajitoa Kwa Zari, Mobeto

Image
DAR ES SALAAM: Mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim (pichani) amejitoa kwenye gogoro linaloendelea kati ya ‘wakweze’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na Hamisa Mobeto. Kabla ya kauli ya mama Diamond juu ya warembo hao mapema wiki hii, wikiendi iliyopita kuliibuka ubuyu kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram kuwa, ugomvi kati ya Zari na Mobeto ulikuwa umeibuka upya baada ya kupoa kwa siku kadhaa. Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko ulibaini kwamba, ugomvi baina ya wawili hao ulirejea upya baada ya Mobeto kukutana na Diamond kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii na kukubaliana juu ya malezi ya mtoto wao, Abdulatif Nasibu ‘Prince Dully’. Ilisemekana kwamba, kuna maneno aliyoweka Zari kwenye Mtandao wa Snapchat yakiashiria kutokuwepo kwa maelewano kati yake na Diamond kufuatia tukio hilo lililoonekana kumweka jamaa huyo karibu na Mobeto. Kama hiyo haitoshi, kuna ubuyu kuwa

Rais Magufuli ashiriki Misa ya majivu

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki na wakristo wengine katika ibada ya Jumatano ya majivu inaoashiria kuanza kwa mfungo mtukufu wa kwaresma. Magufuli akiwa na mkewe, Mama Janeth Magufuli wameungana na waumini hao katika ibada iliyoongozwa na Muadhama Askofu Mkuu, Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar, leo Februari 14, 2018.

Rais Magufuli Ateua Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Mpya

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Februari, 2018 amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Pamoja na uteuzi huo, Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali. Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.

LULU AKIWA GEREZANI MIEZI 3 SASA,MAPYA TENA YAANIKWA,MAMA YAKE ANENA

Image
Ikiwa takribani miezi 3 sasa, tunaambiwa Lulu amenenepa huko gerezani kwa kukubaliana na hali halisi na hajawahi kuumwa. Afisa mmoja wa magereza akichonga na globalpublishers amesema Lulu ndie amegeuka kuwafariji wanaoenda kumtembelea hasa ndugu zake badala ya wao kumfariji. Lulu amekuwa akiwaambia wasijisikie vibaya hakuna aijuaye Kesho yake na yeye wachukulie Kama yupo shule Ya Boarding kuna siku atakuwa Huru . Munalove aliyeanzia kuigiza Kaole ambaye amekuwa na Lulu kwa mvua na jua kwa Miaka mingi sasa ambapo hakosi kwenda gerezani kumuona lulu Kila wiki, alipoulizwa na GPL alisema . . “anatushangaza hata sisi, kwanza kanenepa na anaonekana mwenye furaha maana wakati mwingine tukienda kumuona tunakuwa na simanzi lakini yeye anakuwa mfariji wetu akisema kwamba ipo siku atatoka na kuwa huru tena,” . . Mama Lulu yeye alipopigiwa simu na GPL aliwaka kwa kuja juu akisema hataki kabisa kusikia magazeti wala waandishi wa habari kwakuwa yeye sio superstar, ameomba Lulu

Kiongozi CHADEMA Auawa, Mbowe Asimulia Alivyotekwa, Mwili Wake Waokotwa Ufukweni

Image
  MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kiongozi wa chama hicho katika Kata ya Hananasif, Daniel John amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha. Akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 13, 2018, Mbowe alisema John alitoweka siku moja iliyopita. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hana taarifa hizo lakini anawasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni.   Amesema baada ya mawasiliano atatoa ufafanuzi leo  Februari 14,2018. Mbowe alisema John ambaye ni katibu kata alitoweka akiwa na Reginald Mallya ambaye alijikuta yupo ufukweni mwa bahari. Mbowe alisema walitoa taarifa polisi kuhusu kutoweka kwa John na kwamba, walipokwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walielezwa kuna mwili ulipelekwa na polisi. Alisema mwili huo ulitambuliwa na mkewe John na una michubuko inayoashiria alikabwa, una jeraha la panga kichwani na upande mmoja wa kichwa umebonyea kuashiria alipigwa na kitu kizito. Kuhu

Chama cha Wafanyakazi chapingana na Makonda

Image
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu) kimelaani kitendo kikichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kuwavua madaraka hadharani watumishi wa umma wakisema ni kitendo cha kinyama. Akizungumza leo Februari 13, 2018 wakati akitoa tamko la chama hicho, Katibu Mkuu, Rashid Mtima amesema chama hicho hakitetei watumishi waovu, bali taratibu zinatakiwa kufuatwa katika kuwawajibisha Februari 10, 2018  watumishi wa idara za ardhi wa manipaa za Ubungo na Ilala walivuliwa madaraka hadharani hali iliyosababisha mmoja wao, Paul Mbembela (Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Ilala) kuzimia kwa muda. "Tunalaani, tunalaani, tunalaani sana kitendo kilichofanywa na Makonda. Sheria zinataka mtumishi anayekiuka kanuni na sheria za utumishi kushughulikiwa kwa siri hadi uamuzi wa mwisho utakapotolewa,” amesema. " Jambo baya zaidi tunalolaani hata mtumishi huyo alipozimia Makonda aliendelea kusema Dar es Salaam oyee, huu ni unyama.” Amesema kibin

Diwani Mwingine Chadema Atimkia CCM

Image
DIWANI wa Kata ya Hayderer (Chadema) wilayani Mbulu mkoani Manyara, Justin Masuja amejiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Februari 12,2018 katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti. Katika mkutano wa hadhara, Mnyeti aliwaomba madiwani wa upinzani kuhamia chama tawala ili watekeleze Ilani ya CCM ambayo ndiyo ipo madarakani. Masuja alieleza kwamba amejiunga na CCM ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

Mwanamke abambwa na cocaine kwenye makalio

Image
Polisi nchini Ureno wamemkamata mwanamume mmoja kwenye uwanja wa ndege huko Lisbon, ambaye alikuwa amebeba kilo moja ya cocaine kwenye makalio bandia. Vyombo vya habari nchini humo vilisema kuwa raia huyo wa Brazil aliwasili kwa ndege kutoka mji wa Belém do Pará, kaskazini mwa Brazil. Haijulikani ni vipi polisi walifanikiwa kugundia hilo. Mwanamume mwingine ambaye anashukiwa kuwa angepokea dawa hizo alikamatwa kwenye kituo cha treni cha mji huo. Wanaume hao watakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya. Mwezi uliopita polisi nchini Ureno na Uhispania walikamata cocaine ndani ya mananasi yaliyokuwa yamessfirishwa kutoka Amerika ya Kusini.

KAULI YA KWANZA DIAMOND PLATINUMZ NA HAMISA BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI

Image
February 13, 2018 stori inayoshika headlines ni ya Kimahakama ambapo Nyota wa muziki wa Bongo fleva na President wa WCB, Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wamerudi tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuweka rekodi baada ya usuluhishi wao kuhusu matunzo ya mtoto wao. “Hivyo tutaangalia jinsi ya kumtunza mtoto wetu ikiwezekana tunategemea baadaye anaweza kuwa kiongozi fulani . Nawashauri wababa kwamba wazazi wakike na kiume wajitahidi kuweka majivuno pembeni bila kumuathiri mtoto. Hivyo lazima kuweka majivuno pembeni kwani mwisho wa siku anayeathirika ni mtoto.” Diamond Platnumz <span data-mce-type="bookmark" style="display: inline-block; width: 0px; overflow: hidden; line-height: 0;" class="mce_SELRES_start"></span>

RAMAPHOSA AONGOZA JAHAZI KUMUNG’OA ZUMA MADARAKANI, AMPA SAA 48

Image
Rais Jacob Zuma. RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu, wadhfa wake huo huku Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa akiongoza shinikizo hilo la kumng’oa kiongozi huyo mkongwe barani Afrika.Kwa mujibu shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, hatua hii inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala cha nchini humo ANC. Taarifa zinaeleza kuwa, ANC kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani japo mpaka sasa haijulikani kwamba Rais Zuma alipokeaje ujumbe huo. Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama hicho kumng’oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuchukua muda mrefu na wenye madhara zaidi kwa Chama cha ANC. Rais Zuma ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa, alishindwa