Posts

Ikulu: Rais Magufuli Akutana na Maafisa Wakuu wa JWTZ

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo kabla hajaanza kuwatambulisha Maafisa Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (hawaonekani pichani) ambao wanatarajia kustaafu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ambaye aliambatana na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao wanatarajiwa kustaafu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaotarajiwa kustaafu ambao ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibolwa wanne kutoka (kulia), Meja Jenerali Michael

Bunge kuunguruma kesho, wabunge watatu kuapishwa

Image
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza kunguruma kesho (Jumanne) na Mkoani Dodoma kwa kuanza kuapisha Wabunge wapya watatu pamoja na kupitisha miswada miwili ya sheria ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tisa. Hayo yamewekwa wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi za Bunge kupitia Kitengo cha Habari na Mawasiliano na kusema kuwataja wabunge hao ambao watakula kiapo cha uaminifu kuwa ni Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kutokea Songea Mjini, Mhe. Monko Justine Joseph wa Singida Kaskazini na kumaliziwa na Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa wa Longido. Aidha, katika mkutano huo wa 10 kutakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na Wabunge huku wastani wa maswali 16 ya kiwa ya papo kwa hapo kuenda kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo yanatarajiwa kuulizwa siku ya Alhamisi mnamo februari mosi. Kwa upande mwingine, Kamati 16 za Bunge za kudumu

Lita 85 za Gongo zakamatwa Manyara

Image
Jeshi la Polisi mkoani Manyara limesema limekamata mitambo ya kutengenezea pombe haramu ya gongo pamoja na lita 85 za pombe hiyo, ambayo ni kinyume na sheria za nchi. Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga, amesema vifaa hivyo pamoja na pombe imekamatwa kutokana na operesheni maalum inayoendeshwa na jeshi hilo. “Mkoa wetu wa Manyara umeendelea na misako mbali mbali ambapo tumekamata mitambo ya gongo pamoja na gongo huko mbulu, kijiji cha hydom Manyara, walimkata mtu mmoja Moshi Bula mwenye miaka 55, akiwa na mitambo minne ya kutengenezea mitambo ya gongo, hivi sasa yupo mahabusu na taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani,”, amesema Kamanda Senga. Kamanda Senga ameendelea kuelezea kwamba...Sambamba na hilo tumekamata lita 65 za pombe haramu ya moshi pamoja na watu watatu wanaohusika na pombe hiyo, ambao ni Neema Doto Matayo, mwenye miaka 21, Law

Sumaye: wanaojiuzulu nafasi zao hawatambui majukumu yao

Image
picha ya mtandao Waziri Mkuu Mstaafu , Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa kazi ya Mbunge ni kutetea wananchi wa jimbo lake na si kwenda kumsifia Rais na kudai wabunge waliojizulu nafasi zao kwa kigezo cha kumuunga mkono Rais hawakutambua majukumu yao. Sumaye amesema hayo kwenye kampeni za Ubunge wa marudio katika jimbo la Kinondoni zinazoendelea na kusema kuwa kwa Wabunge ambao wamejiuzulu nafasi zao na kwenda chama kingine kugombea tena hawafai kabisa kuwa wabunge kwa kuwa hawatambui maana ya Ubunge. "Kazi ya Mbunge si kwenda kumtetea Rais bali ni kutetea wananchi waliompa kura, kama Mtulia yeye anasema ameondoka na kudharau kura za watu wa Kinondoni kwa sababu amependezeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi akateuliwe na Rais kuwa Mbunge maana kazi yake ndiyo itakuwa kwenda kumtetea na kumsifia Rais. Watu ambao wanahama chama eti kwa sababu Rais ametenda mambo mema pamoja na ukweli kwamba mimi naweza kubishana sana maana hatujaona

Nabii Tito Apandishwa Mahakamani, Anyimwa Dhamana

Image
Onesmo Machibya almaarufu Nabii Tito aliyetengeneza vichwa vya habari kutokana na mahubiri yake ya kuhimiza ulevi na uasherati, amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, na kusomewa mashtaka ya kujaribu kujiua. Nabii Tito alifanya jaribio la kujiua Januari 25, mwaka huu akiwa mahabusu, ambapo inadaiwa kwamba alijikatakata na wembe kwa lengo la kuyakatisha maisha yake. Alipotakiwa kujibu mashtaka yanayomkabili, Nabii Tito awali alisema hakumbuki chochote kwa sababu yeye ni mgonjwa wa akili, lakini alipobanwa kwa mara nyingine, alisema ni kweli alitaka kujiua kwa sababu kuna sauti ndani ya kichwa chake iliyokuwa inamuelekeza kufanya kitendo hicho. Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Nabii Tito amerejeshwa rumande huku akiwekewa mapingamizi saba ya dhamana.

Matukio kwa Picha na Video Utambulisho wa Mbosso WCB

Image
WCB wakiwa katika picha ya pamoja, katikati ni msanii wao mpya, Mbosso. BURUDANI ya aina yake imepigwa na wasanii wa Lebo ya WCB usiku wa kuamikia leo wakati kumtambulisha msanii mpya katika kundi hilo, Mbosso ambaye awali alikuwa Yamoto Band kabla ya kundi hilo kuvunjika. Mbosso, Diamond na Rayvanny wakikamua. WCB ikiongozwa na Lejendari, Diamond Platnumz, wamemtambulisha huyo katika Ukumbi wa Hyatt Legency Hotel jijini dar es Salaam na kuhudhuriwa na mastaa kibao wakiwemo, Wema Sepetu na wengine pamoja na wanahabari. Diamond akimsalimia mama yake, Bi Sanura ukumbini hapo. WCB na mashabiki waki-enyoj event. WCB na mashabiki katika picha ya pamoja.   Diamond akikata mauno.

Dk Slaa, JPM wakutana kwa mara ya kwanza Ikulu

Image
Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi mteule, Dk Willibrod Slaa, Ikulu Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 29, mwaka 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema Dk Slaa amemshukuru Rais kwa kumteua kuwa Balozi na kuahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa. Imeeleza kuwa Dk Slaa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uongozi bora na kutekeleza mambo makubwa ikiwemo miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa daraja la juu katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto rufiji na mapambano dhidi ya rushwa. “Kwa kweli naona faraja, ninafurahi Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza hatua kwa hatua karibu yote tuliyokuwa tunayapigania kwa miaka takribani 20 ya huko nyuma, mimi Dk Slaa nilikuwa napiga kelele kwa sababu nilikuwa naon

Basi lateketea kwa moto Tanga Leo

Image
Basi la kampuni ya Tahmeed ambalo linafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa Nairobi limeteketea moto katika kijiji cha Matumbi mkoani Tanga leo. Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya moto na kusema kuwa hakuna abiria ambaye amepata madhara na moto huo ulioteketeza basi hilo. "Ni kweli basi hilo limewaka moto leo, ila hakuna abiria aliyejeruhiwa wala kupata madhara yoyote kwa kuwa dereva alipoona dalili za moto alipaki gari pembeni na abiri ambao walikuwepo kwenye basi hilo kama 15 hivi wote waliweza kushuka mapema kabla ya moto kushika gari zima" alisema Wakulymba

Mtulia:nimefanya maamuzi ya Kiume

Image
Mgombea wa Jimbo la Kinondoni kupitia CCM, Maulid Said Mtulia amesema amefanya maamuzi ya kiume ya yeye kuhamia chama hicho kwa sasa kwa maana wapo wengi wanataka kufanya hivyo lakini wameshindwa kwa madai wanasubiri kulipwa kiunua mgongo. Mtulia ameeleza hayo wakati alipokuwa anaendelea kujinadi kwa wananchi wa jimbo la Kinondoni ambalo hapo awali alikuwa analishikilia yeye kupitia chama chake cha CUF kabla ya kujivua uanachama wake na kuenda kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kuijenga nchi. "Kujiuzulu Ubunge sio mchezo, nimefanya maamuzi ya kiume maana kuna wenzangu wengine mpaka sasa hawawezi kutoka kwa sababu wanasubiri kiunua mgongo. Sasa kijana kama mimi nikae pale nisubirie kiunua mgongo hivi kweli ntaweza kuishi kwa kusubiri kiunua mgongo", alisema Mtulia. Aidha, Mtulia amesema amejinusuru kwa mengi kukihama chama chake cha awali ili aweze kuwapigania wananchi wa jimbo hilo kwa maana hapo awali alikuwa anashindwa

DIAMOND PLATINUMZ AFUNGUKA KUMWALIKA WEMA SEPETU,AGUSIA PIA HAMISA MOBETTO,TUNDA NAYE AJAACHWA

Image
Majibu ya Diamond Platnumz Kuhusu Ujauzito wa Tunda HATIMAYE msanii kutoka industry ya Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameamua kuanika ukweli kuhusu tetesi za kumpachika ujauzito Video Vixen wa Bongo, Tunda. Akifanya mahojiano maalum ya , Diamond amekanusha kumpachika mimba staa huyo na kudai kuwa hajawahi hata kutembea naye wala kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.    

Man U Waitwanga Yeovil 4-0, Sanchez Aibuka Man Of The Match

Image
KLABU ya Soka ya Manchester United imeenedeleza ushindi kwa michezo mitatu mfurulizo tangu itoke mapumzikoni, Dubai ambpo usiku wa kuamkia leo imeitwanga timu ya Yeovil bao 4-0 katika michuano ya Kombe la Shirikisho (FA Cup). Katika game hiyo mchezaji mpya wa Man U aliyesajiliwa hivi majuzi akitokea Arsenal, Alex Sanchez ikiwa ni mechi yake ya kwanza alionyesha uwezo mkubwa huku akiisaidia timu yake hiyo kuibuka na ushindi mnono katika Mji wa Yeovil. Wenyeji Yeovil walianza vizuri lakini walifanya makosa yaliyopelekea kuadhibiwa na klabu hiyo tajiri zaidi duniani kwa sasa. Wafungaji ni; Rashford 40, Ander Herrera 61, Lingard 90, Lukaku 90+3. Yeovil: Krysiak, James, Sowunmi, Nathan Smith, Dickson, Green, Wing, Bird, Gray, Zoko, Surridge. Subs:  Connor Smith, Browne, Maddison, Gobern, Whelan, Santos, Fisher. Man Utd:  Romero, Darmian, Lindelof, Rojo, Shaw, Ander Herrera, Carrick, McTominay, Mata, Rashford, Sanchez. Subs:  Lukaku, Smalling, Lingard, You

DC aamuru mkandarasi akamatwe

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, John Palingo ameamuru kuwekwa mahabusu mkandarasi wa umeme kutoka Kampuni ya Cyber, Benjamin John baada ya kutuhumiwa kuchukua fedha kwa wananchi kwa madai ya kuwaunganishia umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) katika vijiji ambavyo havipo kwenye mpango huo. Palingo alitoa amri hiyo jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mbozi baada ya baadhi ya madiwani kudai kampuni hiyo imekuwa ikiwatoza baadhi ya wananchi Sh20,000 hadi 140,000 kwa ajili ya fomu na usajili wa mteja kuunganishiwa umeme. Kutokana na malalamiko hayo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Erick Ambakisye alilazimika kuuita uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Songwe na mwakilishi wa Kampuni ya Cyber kutoa ufafanuzi mbele ya baraza hilo. Hata hivyo, Mkandarasi na mwakilishi wa Kampuni ya Cyber, Benjamini John alipotakiwa kutoa ufafanuzi alikanusha madai hayo akieleza kwamba iwapo itathibitika kuwa kampuni yake imehusika, fe

Trump Uso kwa Uso na Rais Kagame, Atuma Salamu Afrika

Image
Rais Trump (kushoto) akisalimiana na Rais Kagame. RAIS wa Marekani, Donald Trump amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na kumuomba afikishe salamu zake za upenzo kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU. Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi baada ya Mkutano wa Viongozi na Watu Mashuhuri Kuhusu Uchumi na Biashara Duniani. Mkutano huo wa Kagame na Trump umekuja wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kutoa kauli iliyotafsiliwa kama ni kuyakashifu mataifa ya Afrika. Kutoka kusoto ni mama Jeannette Nyiramongi Kagame, Rais Kagame, Rais Trump na Melania Trump. Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana ambapo  amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyakashifu mataifa ya Afrika huku aki kiri kutumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia w

RUBY ASALIMU AMRI KWA CLOUDS,HATIMAYE AOMBA RADHI

Image
Msanii wa muziki Bongo, Ruby amemaliza tofauti baina yake na Clouds Media Group. Muimbaji huyo ametumia kipindi cha XXL kuwaomba radhi wale wote aliowakwaza katika chombo hicho cha habari. “Yeyote, awe ni mwanakamati wa Clouds, team Clouds au awe ni shabiki wa nje I like to apologize guy to say sorry to my country, sorry to this management Clouds, I love them so much all I need is support mimi naamini kwamba ukiwa mjinga kwenye kila kitu utapata kujua vitu vingi sana,” amesema Ruby. “Nilikaa nikamuomba Boss wangu Ruge samahani, mimi ni mdogo wewe ni mkubwa, of course kwa chochote kile mimi ndio nakosea,” amesema. Clouds Media Group walikuwa wamesitisha kucheza nyimbo za msanii huyo kutokana na tofauti zao, hivyo sasa nyimbo zake zinachezwa na inaelezwa tangu November mwaka jana ilitolewa ruhusu kwa ngoma zake kuchezwa.

Lowassa, Mbowe Kuzindua Kampeni za Ubunge Jimbo la Kinondoni

Image
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kesho Januari 27, 2018 watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo inasema kuwa viongozi hao watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni kumtambulisha Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Salum Mwalimu. Uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika viwanja vya Mapilau kuanzia saa nane mchana mpaka saaa kumi na mbili jioni ambapo wageni rasmi watakuwepo Lowassa pamoja na Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA. Tarehe 17 Februari mwaka huu unatarajiwa kufanyika uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Siha na Kinondoni kutokana na wabunge wa majimbo hayo kujiuzulu nafasi zao za Ubunge wakiwa katika vyama vya upinzani na kuingia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa wanagombea nafasi hizo wakiwa chini ya CCM.

Lulu Diva Jeuri Hii Kaipata Wapi?…Anaishi Kwenye Mjengo wa Kifahari

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’. WAKATI wasanii wengine wakilia njaa kali sambamba na kuwa na maisha ya kawaida, hali ni tofauti kwa msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ambapo kwa sasa maisha yake yameonekana kumnyookea baada ya kunaswa akiishi kwenye mjengo wa kifahari pande za Mbezi Beach jijini Dar. Akisonga ugali. Gazeti hili kwa mara ya kwanza limefanikiwa kuunasa mjengo huo wa kifahari ndani ukiwa na vivutio mbalimbali. KAUNTA ZA VINYWAJI Ndani ya mjengo huo una kaunta mbili maalum kwa vinywaji laini ambapo ya kwanza ipo sebuleni na ya pili ipo jikoni huku pia kukiwa na friji kubwa la kisasa la milango miwili lenye thamani ya mamilioni. …Akifungua Friji lenye mapochopocho. SEBULE YA KISASA Ukiachana na sofa na fanicha za kisasa, upande wa sebuleni umepambwa kwa ‘wallpaper’ za aina yake sambamba na nakshinakshi kwenye meza maalum iliokaa mfano wa ‘dressing table.’ ENEO KUBWA LA PARKING Upande wa nje kuna eneo kubwa la pa

MOTO WAUA WATU 39 NA KUJERUHI 100 HOSPITALINI

Image
A person injured in a fire is carried from a hospital in Miryang, South Korea, Friday, Jan. 26, 2018. The hospital fire causes scores of casualties and injuries, according to a fire agency official. (Kim Dong-mi/Yonhap via AP) WATU 39 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika ajali ya moto uliyotokea katika Hospitali ya Sejong, Kusini Mashariki mwa Korea Kusini usiku wa kuamkia leo. Firefighters try to put out a fire at a hospital in Miryang, South Korea, Friday, Jan. 26, 2018. (Kim Dong-mi/Yonhap via AP) Taarifa za awali zimeeleza kuwa moto huo ulianzia kwenye chumba cha dharura cha hospitali hiyo ambapo maofisa wa usalama wameeleza kwamba huenda idadi ya waliokufa ikaongezeka kutokana na hali mbaya za baadhi ya majeruhi hao. Firefighters try to put out a fire at a hospital in Miryang, South Korea, Friday, Jan. 26, 2018. (National Fire Agency/Yonhap via AP) Zaidi ya majeruhi 100 wanasemakana wamo katika jengo la hospitali hiyo. Picha za mitandao

BREAKING : NABII TITO AJIJERUHI KWA KUJIKATA NA WEMBE TUMBONI

Image
Nabii Tito ameibua mengine baada ya kujijeruhi kwa kujikata na wembe tumboni ambapo kumepelekea ashonwe nyuzi 25 katika zahanati ya polisi Dodoma. Daktari wa hospitali hiyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameeleza kuwa Tito alifikishwa hospitali saa 9 mchana akiwa anavuja damu eneo la tumbo. Ni kweli Tito alifikishwa hapa majira ya saa 9 mchana, tulimfanyia matibabu kwa kumshona nyuzi 25 kutokana na ukubwa wa majeraha hayo” amesema Daktari. Hata hivyo kamanda wa polisi Dodoma, Gilles Muroto hana taarifa kutokea kwa tukio hilo. Nabii Tito sasa anashikiliwa na polisi kutokana na kauli zake zinazopingana na dini, amekuwa akihamasisha watu kunywa pombe, na wanaume kulala na wadada wa kazi akidai kuwa kufanya hivyo sio dhambi. Hivyo baada ya matibabu hayo nabii Tito alirudishwa polisi kwa mahojianao zaidi.

Penny: Sijaolewa, Nafasi Ipo Wazi!

Image
MTANGAZAJI wa kipindi cha Harusini kinachorushwa kupitia Magic Swahili, Pennieli Mungwila ‘Penny’ amefungukia vazi la harusi alilovaa na kuwaacha watu kwenye sintofahamu kuwa hajaolewa na kwamba nafasi bado iko wazi. Akizungumza na Star Mix, Penny alisema kuwa, gauni alilovaa ni kwa ajili tu ya kurekodi kipindi chake na sio kwamba ilikuwa ni harusi yake ya ukweli kama watu wengi walivyodhani. “Jamani nisije kukosa mume bure, gauni lile nilivaa kwa ajili ya kazi tu na si kwamba nilikuwa naolewa kweli kama watu walivyodhani,” alisema Penny.