Posts

China Yaipatia Tanzania Msaada Wa Sh. Bilioni 29.4

Image
Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi 29.4bilioni kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu, utalii wa kijiolojia na kuukarabati Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong. Katibu huyo amesema 22.4bilioni  zitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera. “Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” amesema   James Ameeleza kwamba  kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho. “Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu

Serikali Yalifungia Gazeti la Raia Mwema kwa Kuandika Taarifa za Uongo Kuhusu JPM

Image

Aliyeandika Uongo WhatsApp Kuhusu Polisi Kuonekana Hospitali ya Nairobi

Image
MKAZI mmoja wa Kigamboni, Mbutusyo Mwakihaba (40), amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusambaza ujumbe katika mtandao kwamba kachero wa Usalama wa Taifa ameonekana jijini Nairobi karibu na hospitali aliyolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Mbutusyo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa. Wakili wa Serikali Janeth Magoho alidai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kusambaza taarifa za uongo chini ya kifungu namba 16 cha Sheria ya mtandao namba 4 ya mwaka 2015. Janeth amedai Septemba 11, mwaka huu kupitia mtandao wa ‘WhatsApp’ mshtakiwa aliandika “Huyu ni Kachero wa Usalama wa Taifa anatambulika kwa jina la Jose anaonekana Nairobi karibu na hospitali alikolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu…Mwaxcheni mwenzenu” . Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo, upelelezi wa kesi haujakamilika ambapo Hakimu Nongwa alikubali kumpa dhamana kwa masharti ya kuwa n

Magazeti Ya Tanzania Leo Jumamosi, Septemba 30, 2017

Image

Mke wa Lissu aamua kufunguka

Image
Nairobi. Kwa mara ya kwanza, Alicia Magabe ambaye ni mke wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia tukio la mumewe kushambuliwa kwa risasi na kudokeza kwamba haliwezi kuwa limetokana na sababu nyingine isipokuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya. Pia amezungumzia kuhusu afya yake na kueleza kuwa bado siyo nzuri na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombea. Mbali ya Alicia ambaye pia ni mwanasheria, dereva wa Lissu naye amezungumza akisema ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo huku akiahidi kuripoti polisi mara baada ya kurejea nchini. Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu alipopelekwa huko baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari nje ya nyumba yake mjini Dodoma mchana wa Septemba 7 akitokea bungeni. “Watanzania wote wanajua Lissu maisha yake yote amekuwa ni mtetezi wa wanyonge na tukio hili amelipata kutokana na kazi zake hizo hivyo nawaomba tumuombee tu,” alise

NACTE: MAOMBI MAPYA AWAMU YA PILI KWA DIPLOMA NA CHETI YAMESHAANZA KUPOKELEWA

Image
ATTENTION Please read carefully the information in this page before attempting to do anything. WELCOME TO STUDENT’S ADMISSION VERIFICATION SYSTEM Welcome to Student’s Admission Verification System for Certificate and Diploma Applicants. The System allows you to apply for Admission for Further Education in Certificate and Diploma programmes for  academic year 2017/2018 . Currently Available Application Categories:- – Admission Verification for Certificate/DiplomaHealth and Allied Sciences (Including Community Health, Health Records etc) :-  Deadline 01/10/2017 Mafunzo ya Ualimu :-  Deadline 01/10/2017   IMPORTANT NOTES: You are advised to select your most preferred category according to prior qualifications that you hold, because your selection depends on your choices and qualifications. To proceed with the this application you must have the following 1. Valid and Working Email Address2. Valid Phone Number3. Payment Mpesa Confirmation Code   Read Guide

CHUO CHA TUMAINI JIPYA MAFINGA KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO

Image
 MKUU WA CHUO CHA AFYA CHA  TUMAINI JIPYA MAFINGA ANA FURAHA KUWATANGAZIA KUWA CHUO KIMEANZA KUPOKEA MAOMBI YA MASOMO KWA MWAKA WA MASOMO 2017/18 KATIKA KOZI ZIFUATAZO.                                                      1. CERTIFICATE IN CLINICAL MEDICINE YAANI TABIBU MSAIDIZI KWA MIAKA MIWILI Sifa za mwombaji: Awe na ufaulu wa kidato cha nne kwa angalau alama D nne yakiwemo masomo ya sayansi yaani Fizikia (Physics), Kemia (Chemistry) na Baolojia (Biology) 2. CERTIFICATE IN COMMUNITY HEALTH (Uhudumu wa afya ngazi ya jamii) MWAKA MMOJA Sifa za mwombaji: Awe na ufaulu wa kidato cha nne kwa angalau D nne likiwemo somo la Baolojia (Biology) MUHULA MPYA UTAANZA MWEZI SEPTEMBA, 2017. YOTE HAYO YANAZINGATIA MWONGOZO WA WIZARA YA AFYA NA NACTE. CHUO KIMESAJILIWA KWA USAJILI WA KUDUMU KWA NAMBA 144. ADA ZETU NI NAFUU NA ZINALIPWA KWA AWAMU. FOMU ZINAPATIKANA CHUONI TUMAINI JIPYA MAFINGA – IRINGA AU KWENYE WEBSITE YA CHUO. www.tumainijipya.ac.tz Kwa maulizo tafadhali wasiliana na

Mzee Akilimali aliamsha dude Yanga

Image
Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali amemtaka Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Clement Sanga kujiuzulu kwa madai kuwa yeye ndiye chanzo cha matatizo yote yanayotokea ndani ya Klabu hiyo. Mzee Akilimali amesema wamegundua mgomo uliotokea hapo jana kwa wachezaji kutohudhuria mazoezi ni njama iliyopangwa na Sanga wakidai kuwa wachezaji hawajalipwa mishahara yao suala ambalo sio sawa. "Mimi naona tu kwamba Sanga sasa imefikia hapa, ili tufanye vizuri nawasihi Watanzania wote hususani wana Yanga na wapenzi wa Yanga bwana Sanga sasa hivi atamke kujiuzulu, chonde chonde Bwana Sanga iache Yanga watu tuketi pamoja na wewe mwenyewe tuchague viongozi Yanga tusonge mbele" amesema Mzee Akilimali Mzee Akilimali amesema siku moja kabla ya mazoezi alionekana Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sanga akiwa na Nahodha wa Timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' pamoja na Mshambuliaji wa Kimataifa Thaban Kamusoko ambapo baada ya kutoka hap

Irene Uwoya: Napenda mwanaume mwenye sura ya kiume

Image
MWIGIZAJI maarufu wa kike wa filamu za Bongo anayeitingisha Bongo Movie ambae pia aliwahi kuolewa na mcheza soka kutoka Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’, mlimbwende Irene Uwoya, amesema kuwa mpenzi wake wa sasa ana ngeu nyingi mwilini mwake kutokana na kuchanwa visu. Uwoya amesema watu kama hao ndiyo anaowataka yeye, kwa sababu inaonyesha uanaume halisi, na si wanaume kuwa laini kama mtoto wa kike. Alipoulizwa juu ya hilo alifunguka: “Sijasema napenda wanaume wenye sura mbaya. Nimesema napenda mwanaume mwenye sura ya kiume, mwanaume uwe na ngeu. Mimi bwana’angu ana ngeu za kuchanwa visu, viwembe na nahisi hata bunduki zimemkosakosa,” alisema Irene Uwoya Mwigizaji huyo kwa sasa hajaweka wazi mahusiano yake tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake, msanii wa Bongo Fleva, Msami Baby, na amesema hataweka tena mahusiano yake wazi. NA : SAMSON JEREMIAH/GPL

Rais Magufuli Azindua Barabara Mererani Mkoa Wa Manyara Leo

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera alipowasili kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia maelfu ya wananchi alipowasili Mererani kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa Mererani wakati wa kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe M

Miili ya Ndugu 13 Waliofariki kwa Ajali Uganda Ilivyoagwa Dar (Pichaz)

Image
Wanajeshi wa JWTZ wakibeba miili ya marehemu hao kupeleka eneo maalum kwa ajili ya kuaga. SIMANZI, vivlio na majozni imetawala wakati wa kuaga miili ya Watanzania 13 ambao ni ndugu wa familia moja waliofariki kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea nchini Uganda hivi karibuni. Waziri Angella Kairuki akiteta jambo na Betty Kamya ambaye ni mwakilishi wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. Miili ya wanafamilia hao imeagwa leo Septemba 20, 2017 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kuelekea Arusha, Kilimanjaro na Mpwapwa kwa ajili ya mazishi. Waombolezaji wakati wa shughuli ya kuaga marehemu. Katika ibada hiyo ya kuwaaga marehemu, viongozi mbalimbali wa serikali walikuwepo wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala), Angela Kairuki, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijage, Waziri Maalum wa Kusimamia Jiji la Kampala, Betty Kamya kutoka Uganda aliyemwakilisha Rais wa nch