Posts

MWANAMKE MWENYE SURA MBAYA DUNIANI

Image
Mwanamke anayedaiwa kuwa na sura mbaya duniani na mitandao inayomuonea ametoa filamu kuhusu maisha yake.Maisha ya Lizzie Velasquez mwenye umri wa miaka 26 yalibadilika kabisa baada ya kuona kanda ya video katika mtandao wa tube iliodai kwamba yeye ndiye mwanamke mwenye sura mbaya duniani. Lizzie ambaye alikuwa na miaka 17 wakati huo alikasirishwa kuona kwamba msichana aliyekuwa katika kanda hiyo ya video alikuwa yeye. Kanda hiyo ilioonekana mara millioni 4 mtandaoni huku wengi wakiwacha ujumbe wa kuudhi kama vile ''angeuliwa alipozaliwa'',nilishangaa nilipoona ujumbe huo alisema Lizzie. Ujumbe mwengine ulisoma ''kwa nini wazazi wake walimlea''. Mwanamke huyo alipiga moyo konde na kuanza mtandao wake wa You Tube akiwaelezea watu kuhusu mwanamke huyo anayedaiwa kuwa mwenye sura mbaya zaidi. Lizzie amesema kuwa anawasaidia wengine ambao wamekuwa wakionewa kuweza kupata msaada ama hata kupambana na maonevu hayo. Mwanamke huyo pia an...

DUKA LA KISASA LA GSM MALL LAUNGUA MOTO

Image
Magari ya Zimamoto na Uokoaji yakiwa nje ya Duka kubwa la GSM Mall tayari kuzima moto uliokuwa unaunguza duka hilo katika Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja.   Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.   Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo Moto Umeibuka katika duka kubwa la GSM Mall ililopo Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda duka hilo lilianza kuungua majira ya 8:30. Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza julikana. Magari ya zimamoto na uokoaji yalijazana eneo hilo kunusuru mali na maisha ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo lenye ghorofa nne. Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa duka hilo walionekana walikimbia nje ya duka kuokoa maisha yao. Baadhi yao walitolewa wakiwa mahututi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia magari ya polisi. Duka hilo kubwa la kisasa lenye yenye aina mbalimbali za ...

Rais Magufuli Akizindua Ujenzi wa Maghorofa Magomeni Kota

Image
Rais Magufuli akihutubia Rais wa Jamhuri ya Serikali ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezindua rasmi ujenzi wa majengo matano ya ghorofa 8 kila moja katika maeneo ya  Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. Akizindua ujenzi huo ambao utagharimu takribani TZS bilioni 20, Rais Magufuli amesema kuwa majengo hayo yatakuwa na unafuu mkubwa kwa wakazi wa Dar, lakini pia ndani ya majengo hayo kutakuwa na maduka ambayo wafanyabiashara wataweza kuweka biashara zao hivyo hakuna ulazima wa mtu atakayeishi humo kutoka kwenda kufanya mahemezi nje. Hizi ni baadhi ya kauli alizozizungumza Rais Magufuli wakati wa uzinduzi huo; Wazee wangu wa Magomeni waliteseka sana, lakini naamini sasa mateso yao yanaelekea kuisha.  Nafahamu mikoa mingi ina maeneo yaliyotengwa kwa makazi ya watu, lakini waliondolewa na watu wenye nguvu kwa hila. Baadhi ya wananchi waliohudhuria. Nyumba hizi zitakapokamilika, wakazi 644 waliokuwa hapa awali, nilisema watakaa miaka mitano bur...

MSICHANA WA MIAKA 21 AUAWA NA MPENZI WAKE KISHA KUMFUKIA CHINI YA KITANDA

Image
Tukio moja lilimeibua hisia kubwa kwa wakazi wa kijiji cha Isyongo kaunti ya nyamira nchini Kenya, baada ya Polisi kufukua maiti ya msichana mmoja Feidhi Omega 21, iliyokuwa imezikwa chini ya uvungu wa kitanda.  Taarifa zinasema kuwa binti huyo alimtembelea mpenzi wake wiki mbili zilizopita lakini hakurudi nyumbani kwao ndipo mama yake alipoanza kumtafuta na kuelekezwa kwa mpenzi wake Daniel Nyabuti, huku akiwa na matumaini ya kumkuta mtoto wake akiwa hai,  walipofika nyumbani kwa kijana huyo Polisi walianza kumtafuta na kukuta kaburi chini ya uvungu wa kitanda kwa kijana huyo ambako binti huyo alikuwa amezikwa. “Nikasilia slipaz zimepatikana kwa njia ya huyo kijana baada ya hapo kufika tarehe karibu tano hivi mwezi wa tatu nikachukua wazee wa nyumbani kuja hapa tulikuwa watatu tukakuja mpaka nyumbani kwa kijana kuuliza huyo mtoto”  Moraa mama wa marehemu. Hata hivyo haikuweza kujulikana kilichotokea na kusababisha kifo cha binti h...

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AWAONGOZA WANANCHI KUUWAAGA POLISI 8WALIOUAWA PWANI

Image
Majeneza yenye miili ya marehemu ya polisi nane waliouawa kwa kupigwa risasi na majambazi, Kibiti, Pwani yakiwa katika Uwanja wa Polisi, Barracks barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akiaga miili ya marehemu. Mwigulu Nchemba Akiendelea kuaga. Shehe akifanya maombi. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kushoto) akiwa na Mwigulu (kulia). Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro (wa mbele) akitoa pole kwa wafiwa. RPC wa Pwani, Onesmo Lyanga akiaga miili ya marehemu. Kamanda wa Polisi Temeke Gilles Muroto akiaga. Wakiendelea kuaga