MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MAPINDUZI YALIVYOFANYIKA LEO ZANZIBAR
Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha uwezo wao wa kupigana bila silaha katika Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye wawnja wa Aman Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha jinsi matofari yanavyoweza kuvunjwa juu ya kichwa katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwa amelala juu ya misumari huku wenzake wakipita juu yake ikiwa ni moja ya maonyesho ya ukakamavu yaliyoonyeshwa na Makomandoo hao katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 12. 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).