WAWILI WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI
Watu
wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi wameuawa kisha kuchomwa moto katika
kijiji cha Ifumbo Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya katika jaribio la
kufanya uhalifu eneo la machimbo ya dhahabu ya Kasanga Lupa Market.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ifumbo Emily Rajab
amesema waliouawa wametambuliwa kwa majina ya Paschaly Paul Simchimba
mkazi wa Ileya Lupa Market na Tegemeo Henus mkazi wa Mjele ambapo
waliouawa na wananchi waliamua kujichukulia sheria mkononi walipokuwa
wakichukuliwa maelezo katika ofisi ya mtendaji.
Rajabu
amesema alitoa taarifa kituo cha Polisi Chunya lakini wakati wakimsubiri
kufika wananchi walimtimua Mwenyekiti wa kijiji na yeye kisha kuwafunga
kamba majambazi hayo na kuanza kuwapiga kwa silaha mbalimbali kisha
kuwachoma kwa kutumia magurudumu ya gari. Polisi walifika walikuta miili
imeteketea kabisa.
Uchunguzi
wa awali umeonesha marehemu walikuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka
thelathini jela mwaka 2014 kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha na
kusababisha mauaji eneo la Lupa Market ambapo baadaye walitoka.Kwa
upande wake mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amesikitishwa na
tukio hilo ambalo limetokea Ifumbo na kuwataka wananchi kuacha tabia za
kujichukulia sheria mkononi kwani wangefikishwa Polisi wangesaidia
kubaini mtandao wa ujambazi.
Baadhi ya
ndugu walionekana eneo la tukio wakishuhudia mauaji hayo ambapo Polisi
walipofika walichunguza na kuamuru kuzikwa miili hiyo kutokana na
kuharibika vibaya .Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio
hilo.
MBEYA YETU
Comments
Post a Comment