Posts

Breaking News….Darassa Apata Ajali Kahama Mkoani Shinyanga

Image
Muonekano wa gari alilopata nalo ajali ainaya Toyota Harrier Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwanamuziki wa Hip Hop Bongo ambaye anasumbua na ngoma yake kali ya Muziki, Sharrif  Thabit ‘Darassa’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya maeneo ya Ntobo barabara ya kuelekea Mgodi wa Bullyanhulu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Habari zimeeleza kuwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Harrier  ambalo dereva hajajulikana, Darassa alikuwa ameambatana na director wake, Hanscana pamoja na producer wake, Abba Process na wote wametoka salama. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa amethibitisha kupata ajali hiyo na alipopigiwa simu na Global Publishers  alisema hawezi kuongea kwa sasa hivyo atafutwe baadaye.

Penzi la Jide, Nusu Bongo, Nusu Nigeria

Image
Mpenzi wa Jide, Spicy naye akifunguka mbele ya kamera za Global TV Online. BAADA ya kukaa muda mrefu bila kumtambulisha mpenzi wake mpya baada ya kumwagana na aliyekuwa mumewe, Mtangazaji Gardner G. Habash, hivi karibuni mwanamuziki nguli wa kike Bongo, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ aliamua kumuanika mchana kweupe mpenzi wake mwingine aitwaye Spicy. Mwanamuziki huyo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, siku hizi za usoni baada ya kumuweka wazi mpenzi wake huyo ambaye ni raia wa Nigeria, ameonekana ni mtu mwenye furaha na asiyeweza kuficha hisia zake za mapenzi ya kweli kwa mwenza wake huyo. Mapema wiki hii, Jide aliibuka ndani ya mjengo wa Global Publishers akiwa ameambatana na Spicy, mambo yakawa hivi mbele ya waandishi wa Global TV. Wapenzi hao wakifurahia jambo wakati wa mahojiano na Global TV Online. Amefika na je hakuna machozi tena? “Unajua hata kama nilikuwa naimba nyimbo nyingi zinahusiana na mambo ya kutendwa kimapenzi lakini ukweli nil...

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA HALMASHAURI YA ARUSHA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimtwisha ndoo ya maji bibi Agness Silima ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Onderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga ngoma ya msanja iliyokuwa ikichezwa na wnanwake wa Arusha baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kwamrombo wilayani Arusha ambao walijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusimama ili kuzungumza nao. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 17, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Maj...