Posts

Moto Wateketeza Godauni la Matairi Mikocheni Dar

Image
DAR ES SALAAM: Moto mkubwa ambao mpaka sasa bado unawaka umeteketeza godauni la  kuhifadhia matairi la Kampuni ya 7 General linalomilikiwa na Wahindi lililopo karibu na Chuo Kikuu cha Tumaini eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam. Tovuti hii imefanikiwa kufanya mahojiano na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo aitwaye Shaban Salum ambaye ameeleza kuwa chanzo cha moto huo mkubwa na wa aina yake ambao unaonekana ni vigumu kuuzima ni shoti ya umeme. Timu ya Kikosi cha Zimamoto imewahi kufika eneo la tukio ikiwa na magari takribani matano na kufanya juhudi za kuuzima moto huo lakini hawajafanikiwa. Mpaka sasa maji yameisha na magari mengine yamefuata maji mengine kwa ajili ya kuendelea na zoezi la uzimaji. Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda yupo eneo la tukio ili kuona jinsi ya kuongeza nguvu katika zoezi la uokoaji mali pamoja na kuzima moto huo. PICHA ZOTE NA HILALY DAUD / GPL

MTV EMA Wampokonya Tuzo Wizkid na Kumpa Alikiba

Image
IKIWA ni siku chache baada ya waandaaji wa Tuzo za MTV EMA 2016 kutoa tuzo hizo na kumtangaza msanii wa Nigeria Wizkid kuwa ndiye mshindi wa Best African Act na Worldwide Act ambapo katika kipengele hicho alikuwa akichuana na msanii wa Tanzania, Ali Kiba. Waandaaji hao wamempokonya Wizkid tuzo hiyo kwa madai kuwa hakustahili na kumpa Ali Kiba ambaye wamesema alistahili kushinda. Siku chache zilizopita baada ya Wizkid kushinda tuzo hiyo, kulitokea sintofahamu huku mashabiki wa kiba wakiponda mchakato mzima wa utoaji tuzo huo ambapo website ya MTV EMA ilionesha kura zilionesha kuwa ni Alikiba ndiye aliyeshinda. MTV EMA kupitia akaunti yao ya twitter wamethibitisha kumpa ushindi huo Alikiba ambapo yeye ameupokea kwa furaha sambamba na mashabiki wake. Amesema baada ya mashabiki wake kulalamika kuhusiana na mkanganyiko huo, MTV EMA walifuatilia na kukiri kuwa na makosa na kuutumia ujumbe uongozi wake kuwa Alikiba ndiye mshindi halali, na sio Wizkid. “Sasa ndio nim

Rais Obama Amualika Donald Trump Ikulu Leo

Image
  Rais Barack Obama wa Marekani  amempongeza Rais Mteule wa taifa hilo, Donald Trump na kumualika Ikulu kujadiliana juu makabidhiano ya ofisi. Maelfu waandamana kupinga ushindi wa Trump Kumekuwa na maandamano ya kupinga ushindi wa Donald Trump kutoka katika miji mbalimbali nchini Marekani. Maelfu ya raia kwa sasa wamekusanyika nje ya mnara maarufu kama Trump Tower mjini New york wakipaza sauti zao kuhusu sera za uhamiaji,mapenzi ya jinsia moja na haki ya uzazi yanayopingwa na Donald Trump. Wanasema hata dunia ina wasiwasi juu ya ushindi wa urais.

MAJALIWA APOKEA MSAADA WA MAAFA YA TETEMEKO LA KAGERA KUTOKA KWA BALOZI WA KUWAIT NCHINI

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya dola za Marekani 33,000 kutoka kwa balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyka ofisini kwa Waziri Mkuum bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya dola za Marekani 33,000 kutoka kwa balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyka ofisini kwa Waziri Mkuum bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Jaji Mutungi Avifutia Usajili Vyama Vitatu vya Siasa Nchini

Image
DAR ES SALAAM: Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi leo amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kwa makosa mbalimbali.  Vyama hivyo vilivyofutwa ni pamoja na Chama cha Haki na Ustawi wa Jamii (CHAUSTA) kinachoongozwa na  James Mapalala, Chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo)  kinachoongozwa na Peter Kuga Mziray na Chama cha Jahazi Asilia kilichokuwa kinaongozwa na Kassim Bakari Ally. Akiongea na wanahabari leo, Jaji Mutungi amesema amevifuta vyama hivyo kwa kutumia kifungu cha 19 cha sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992.    Jaji Mtungi ameongeza kuwa, mchakato wa kufuta usajili wa vyama hivyo unatokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu lililofanyika kuanzia Juni 26  hadi Julai 2016. Katika zoezi hilo la uhakiki ilibainika kuwa vyama tajwa hapo juu vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kuki

Rais Magufuli, Nkurunzinza Wampongeza Donald Trump kwa Kushinda Urais wa Marekani

Image
  Leo November 9, 2016 Marekani imeweka historia nyingine baada Donald Trump wa Chama cha Republican kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais, na tayari ameanza kupokea pongezi kutoka kwa viongozi wa nchi mbalimbali ikiwemo Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ni miongoni mwa viongozi waliompongeza Donald Trump kupitia Twitter.   Rais Magufuli ametoa pongezi zake kwa Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake Twitter Congratulation President-Elect and people of America for a democratic election,I assure and people of Tanzania for a continued friendship. — Dr John Magufuli (@MagufuliJP) November 9, 2016 Nkurunziza ampongeza Trump Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema ushindi wa Trump ni ushindi wa Wamarekani wote. Mr. @realDonaldTrump , on behalf of the people of Burundi, we warmly congratulate you. Your Victory is the Victory of all Americans. — Pierre Nkurunziza (@pnkurunziza) November 9, 2016 Tupia