Posts

PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA KUWASILI MFALME MOHAMED VI WA MOROCCO, NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU

Image
Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI (aliyetangulia mbele) akishuka katika Ndege mara alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Mfalme wa Morocco Mohammed VI akipokea shada la maua alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mfalme wa Morocco Mohammed VI wakisimama kwa nyimbo za Taifa na mizinga 21 mara baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara ya siku tatu

PANYA ROAD APEWA KIPIGO KIZITO NA WANANCHI, AZINDUKA AKIWA MOCHWARI

Image
Mtoto Isack Ernest (16) anayetuhumiwa kuwa ni mhalifu, maarufu Panya Road, amezinduka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam. Isack ni miongoni mwa vijana watano waliopigwa na wananchi wenye hasira kwa madai ya kuiba mali zao hali iliyosabisha apoteze fahamu na kudhaniwa amefariki dunia. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Gilles Muroto, alisema baada ya polisi kupigiwa simu na raia wema kuwa kuna vijana watatu wamefariki dunia, walikwenda eneo la tukio na kuwakuta wakiwa na hali mbaya. “Mmoja wao anayeitwa Kelvin Nyambocha (14) alifariki dunia baada ya kupigwa na kuchomwa moto na wananchi.   “Kabla ya kufariki, Kelvin alifuatana na wenzake kwa lengo la kwenda kuangalia tamasha la kuibua vipaji vya muziki wa singeli lililoandaliwa na Radio Clouds Fm lililofanyika Mbagala Zakhem,” alisema Kamishna

Khadija Kopa Kuwasha Moto Krismas Morogoro

Image
Mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  akizungumza jambo na wanahari (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni mkuu wa matukio kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kurugira Maregesi,  Hamis Abdallah na Khadija Kopa. Khadija Kopa akizungumza jambo. Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat, akielezea namna atakavyopagawisha mashabiki wake. MALKIA wa muziki wa taarab ambaye ni Mkurugenzi wa Kundi la Ogopa Kopa, Khadija Kopa,  anatarajiwa kuwasha moto kwa kutoa burudani ya aina yake katika  Tamasha la Muziki wa Taarab  lililoandaliwa na mtandao wa habari wa Vijana, Tegemeo Arts Group ambalo linajulikana kwa jina la ‘Nani Zaidi’. Tamasha hilo litakaofanyika siku ya X-Mass ya Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi usiku. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  amesema tamsha hilo linalenga kuhamasisha jamiii katika uchang

Rais JPM Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Tanga

Image
Rais Dk. John Pombe Magufuli. Rais Dk. John Pombe Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, Emmanuel Mkumbo. Bwana Mkumbo alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kujifanya ofisa wa usalama wa taifa nakumtishia kwa bastola askari wa usalama barabarani wakati wakielekea kituo kidogo cha polisi Kingoluwira, Morogoro alikotaka apelekwe kuzungumza na mkuu wa kituo baada ya kukamatwa akiwa amezidisha Mwendo kasi katika barabara kuu ya Morogoro – Dar es Salaam.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MAELFU KUAGA MWILI WA MEYA WA ZAMANI WA DAR ES SALAAM DKT. DIDAS MASABURI

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea machache kwenye hafla ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016.  Sehemu ya wafiwa kwenye hafla ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masa b uri katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakitoa heshima zao za mwisho na kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakiwapa pole wafiwa baada ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mk

Nauli Za ATCL Zitakazotumika Kuanzia Oktoba 14 Hadi 28

Image
Ndege mbili mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400 zinatarajia kuanza kazi wakazi wa mikoa ya Mwanza, Arusha na Zanzibar watakuwa wa kwanza kupata ofa. Ofisa Habari wa shirika hilo, Lilian Fungamtama amesema safari mpya za ndege hizo ikiwamo ya Dar es Salaam – Mwanza, nauli iliyopangwa ni Sh160,000. Amesema safari za Dar es Salaam – Arusha nauli yake itakuwa Sh180,00 na Zanzibar – Dar es Salaam ni Sh85,000. “Ofa hii imetolewa na ATCL kwa safari mpya za ndege hizo,” alisema Fungamtama. Amesema hakutakuwa na safari ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, lakini itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam -Arusha hadi Zanzibar. “Ndege ya kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha ndiyo itakayokwenda kuchukua abiria Zanzibar haitatokea Dar es Salaam moja kwa moja,” alisema. Akifafanua kuhusu nauli hizo, Fungamtama alisema nauli ya kutoka Dar kwenda Kigoma itakuwa katika madaraja mawili ambayo ilikuwapo tangu awali. Amesema bado ndege hizo hazijaan

Rais Magufuli Akutana Na Mabalozi Ikulu

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2016 9 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe: Philip Marmo alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi jambo baada ya kupokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara a