PANYA ROAD APEWA KIPIGO KIZITO NA WANANCHI, AZINDUKA AKIWA MOCHWARI
Mtoto
Isack Ernest (16) anayetuhumiwa kuwa ni mhalifu, maarufu Panya Road,
amezinduka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) katika Hospitali
ya Temeke, Dar es Salaam.
Isack ni
miongoni mwa vijana watano waliopigwa na wananchi wenye hasira kwa madai
ya kuiba mali zao hali iliyosabisha apoteze fahamu na kudhaniwa
amefariki dunia.Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Gilles Muroto, alisema
baada ya polisi kupigiwa simu na raia wema kuwa kuna vijana watatu
wamefariki dunia, walikwenda eneo la tukio na kuwakuta wakiwa na hali
mbaya.
“Kabla ya
kufariki, Kelvin alifuatana na wenzake kwa lengo la kwenda kuangalia
tamasha la kuibua vipaji vya muziki wa singeli lililoandaliwa na Radio
Clouds Fm lililofanyika Mbagala Zakhem,” alisema Kamishna Muroto.
Alisema
wakati wanarudi nyumbani, kundi la vijana hao wanaojiita Panya Road
waliokuwa na silaha za jadi (mapanga), waliwavamia watembea kwa miguu na
kuwaibia mali zao na ndipo wananchi walipofanikiwa kuwakamata watano.
Alisema
Isack alipigwa hadi akazimia kiasi ambacho walijua amefariki dunia na
ndipo alipopelekwa chumba cha kuhifadhia maiti na kufanyiwa taratibu
zote, ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nguo na kuwekewa namba tayari kwa
kuingizwa kwenye jokofu.
“Wakati
amewekwa chini kwa ajili ya kuingizwa kwenye jokofu, alizinduka kwa
kupumua na kuonekana bado yupo hai, hali iliyosababisha kupelekwa chumba
cha uangalizi maalumu (ICU),” alisema Kamishna Muroto.
Alisema
baada ya kupata fahamu na afya yake kutengemaa, alihojiwa na Jeshi la
Polisi, akawataja wenzake 10 waliokuwa kikundi kimoja. Vijana hao ni
Menso Somba (16), Adam Jumanne (16), Bakari Amir (14), Ally Said (17),
Abdillah Yusuf (16), Brown Mathias (15), Jafari Salum (13), Hamisi
Mwanda (16), Siraji Hamisi (16) na Jeremia Gaudence (13).
Wakati
vijana hao wakipewa mapanga yao mbele ya ofisi ya Kamanda wa Polisi wa
Temeke huku wazazi wao wakishuhudia, walianza kuyagombea wengine wakidai
kuwa yao yamebadilishwa na kupewa wenzao.
Kamishna
Muroto alisema kikundi hicho kina bendera inayoonyesha michoro
mbalimbali ikiwamo askari mwenye silaha anakimbia huku anatiririka damu,
mtu ameanguka chini akiwa amekatwa mkono, nyumba na vijana wawili
wakiwa wameshika panga
Alisema kundi hilo la vijana ambalo linazunguka maeneo mbalimbali, limekuwa likijiita ‘Taifa Jipya’
Kamishna
Muroto alisema kijana mwingine, Faraji Suleiman (19) ambaye pia hali
yake ni mbaya, amelazwa Hopitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu
zaidi.Kamanda
Muroto alisema vijana wawili aliowataja kuwa Hamisi Mponda (18) na
Abdallah Omari (15) walitibiwa hospitali ya Temeke na kuruhusiwa.
Alisema
jeshi hilo kupitia Sheria ya Watoto ya mwaka 2009 kifungu 7-9,
linakusudia kuwafikisha mahakamani wazazi wa watoto 16 ambao walitajwa
na kuthibitisha kufanya uhalifu huo, kwa kushindwa kuwaangalia watoto
wao.
Kamishna
Muroto alisema wazazi wana wajibu wa kuhakikisha mtoto anakuwa chini ya
uangalizi ambao hauwezi kumsababishia madhara ya kimwili na
kisaikolojia.“Hii
ina maana kila mzazi ahakikishe mtoto wake ana ulinzi, yuko salama muda
wote dhidi ya udhalilishaji na hatari zote ili watoto hawa wakue
vizuri,” alisema Kamishna Muroto.Alisema jukumu la mzazi ni kuhakikisha mtoto anakuwa kwenye malezi bora na si kumwacha akilelewa na walimwengu.
“Mzazi
atakayeshindwa kumsimamia vyema mtoto wake na kukiuka sheria ya mtoto ya
mwaka 2009 katika kifungu cha 14, atafikishwa mahakamani na akitiwa
hatiani atafungwa miezi 6 au kulipa faini ya Sh milioni 5,” alisema
Kamanda Muroto.Alisema kutokana na mazingira waliyokutwa watoto hao, wazazi wao wanatuhumiwa kwa kukiuka sheria hiyo ya watoto.
Akisimulia
mkasa huo, Isack Ernest alisema yeye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu
katika Shule ya Sekondari Lumo na hajawahi kufanya vitendo vya kihalifu.
Alisema wakati yupo kwao, wenzake walimfuata na kumwambia waende kwenye tamasha la singeli Mbagala. “Tulienda
na baada ya kumaliza tamasha, wenzangu wakasema twende tukale
(walimaanisha wakapore), mimi nikajibu sina pesa, ndipo waliposema
wakienda kula hawatanigawia kwa kuwa aliyekula kala, ndipo walipokwenda
kuvamia watembea kwa miguu na kuiba.
“Wakati nikiwa ng’ambo ya pili, nikasikia sauti ya watu wanasema mwizi mwizi, mwizi,” alisema Isack.Alisema baada ya kupigiwa kelele za wezi walikimbia na kumfuata alipo ndipo kipigo kilipomwangukia yeye hadi kupoteza fahamu.
“Nilikuja
kushtuka nipo ICU, huku nikiwa sijui niko wapi, nimekoma kujihusisha na
makundi kwa sababu sijawahi kuiba katika maisha yangu,” alisema Isack.
Baba mzazi wa kijana huyo, Ernest Chalo, alisema mtoto wake alimuaga anakwenda kuangalia mpira Mbagala Oktoba 15, mwaka huu.
Alisema
wakati yeye anafuatilia mchezo wa timu ya Simba na Kagera Sugar,
alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akimpa taarifa ya kuwa mtoto wake
amefariki dunia.
“Kiukweli
nilichanganyikiwa kwa sababu nimetoka kumzika mke wangu wiki moja
iliyopita, tena napokea taarifa ya mtoto kufariki, nilitoka mpaka kwa
mwenyekiti wangu wa mtaa na kumpa taarifa, nikachukua usafiri wa
pikipiki kwenda Hospitali ya Temeke,” alisema Chalo.
Alisema
alipofika hospitalini hapo, aliambiwa mtoto wake yupo chumba cha
kuhifadhia maiti, lakini alipoletewa mwili kuutambua haukuwa wa mtoto
wake, ndipo akatokea msamaria mwema akamwambia mtoto wake alizinduka.
“Kutokana
na baridi kali ya chumba cha kuhifadhia maiti, mtoto wangu alipoingizwa
mle ndani alipumua na hivyo kuhamishiwa ICU,” alisema Chalo.
Comments
Post a Comment