Posts

PICHA 5: Tingatinga Lilivyofukua mamilioni yaliyokuwa Yamefichwa ardhini

Image
Kama wewe unadhani huna fedha, basi kuna wengine ambao wamezichimbia ardhini, tena kwa mamilioni. Benki ya chini ya ardhi iliyosheheni mamilioni ya fedha, zilizoswekwa ndani ya mifuko myeusi ya plastiki na kufukiwa mchangani, imechimbuliwa na matrekta ya kutengeneza barabara jijini Arusha huku noti nyekundu zikitawanywa kila kona na kufanyika kuwa 'Sadakalawe - Amina,' kwa kila mpita njia ambaye angeweza kujitwalia fungu. Ilikuwa ni mshikemshike katika eneo la Mianzini mjini Arusha , ambako kuna mradi mkubwa wa upanuzi wa barabara ya kutoka Mianzini Mataa hadi Ilkiding'a unaoendelea. Watu walipigana vikumbo katika harakati za kujineemesha na fedha zilizokuwa zimetapakaa eneo hilo. Ikiwa imesheheni noti tupu, tena nyekundu na mpya, kufumuliwa kwa akaunti hiyo ya benki ya chini ya ardhi pamoja na kuwa neema kwa wapita njia na wakazi wa eneo hilo, kuligeuka pia kuwa kilio kwa mmiliki wa hazina hiyo, Christopher Akoonay

Magufuli Amwandalia Dhifa Ya Taifa Kabila

Image
 Rais John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila Ikulu jijini Dar.  Kabila akimwamkia rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi  Ikulu katika dhifa ya taifa.  …Akimsalimia Mama Sitti Mwinyi, mke wa Ali Hassan Mwinyi.  …Akisalimiana na spika mstaafu  Anne Makinda .     …Akisalimiana na  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuberi Ali Maulid.   Sehemu ya waliohudhuria dhifa ya taifa.  Kuoka kushoto ni rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuberi Ali Maulid na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi.  Sehemu ya wageni waalikwa.  Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman, waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,  Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC, Raymond Tshibanda

RAIS DKT MAGUFULI ASHUHUDIA RAIS KABILA WA DRC AKIWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE JENGO LA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila akihutubia katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange leo tarehe 04 Oktoba, 2016 wamefanya mazungumzo rasmi Ikulu Jijini Dar es Salaam na kisha kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria katika nchi hizi mbili marafiki na