Posts

Ummy Mwalimu: Marufuku Kuozesha Waliomaliza La 7

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. SERIKALI imewaonya wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutowaozesha watoto wote wa kike waliohitimu darasa la saba mwaka huu wakati wa kipindi hiki cha kusubiri matokeo yao, iwe ni kwa sababu yoyote ile au kwa lengo la kujipatia mali kwa njia ya mahari. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mkono wa serikali kisheria ni mrefu, hivyo wazazi au walezi watakaokwenda kinyume watahakikisha kuwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani. Ummy ameyasema hayo jana katika tamko maalumu alilolitoa kwa wanafunzi hao waliohitimu elimu ya msingi nchini kote. Alisema wazazi na walezi wanapaswa kutambua umuhimu wa mtoto wake kuendelea kielimu, na kukua kimwili na kiakili kabla ya kuingia katika ndoa kwani elimu ya watoto wa kike ni moja ya njia bora za kupunguza umaskini katika mataifa yanayostawi. “Natoa rai kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa kw...

PROFESA MARK MWANDOSYA AMTEMBELEA NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI.

Image
 Profesa Mark Mwandosya (kushoto) akielezea uzoefu wake alipokuwa Kamishna wa Kwanza wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1985 mara alipomtembelea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo. Kulia ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Pan African Energy aliyeambatana na Profesa Mark Mwandosya, Jacqueline Kawishe.  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo akielezea maendeleo ya  Idara ya Nishati katika kikao hicho. Kutoka kushoto, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini kutoka  Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo, Profesa Mark Mwandosy...

Rais Magufuli Ateua Makatibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa na Mara

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Septemba, 2016 amemteua Bw. Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara. Bw. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu. Pia, Rais Magufuli amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu. Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye. Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es Salaam 09 Septemba, 2016

GIGY MONEY ACHEZEA KICHAPO,NI BAADA YA KUFUMANIWA NA MCHUMBA WA MTU

Image
Baada ya kurukaruka na wanaume tofauti, hatimaye msanii na Video Queen Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’, amejikuta akichezea kichapobaada ya kufumaniwa akiwa na mchumba wa mtangazaji wa Choice FM aliyetajwa kwa jina moja la Mo, nyumbani kwake Kawe jijini Dar. Video Queen Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money akiwa katika mapozi tofauti. Kwa mujibu wa chanzo makini, Gigy amekuwa hatupii picha za aina yoyote kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa sababu ya majeraha aliyopata baada ya msichana aliyefahamika kwa jina la Shov Mohamed kumfumania nyumbani hapo kwa Gigy. “Mnajua Gigy hivi karibuni alifumaniwa nyumbani kwake na mwanaume wa mtu akapata kipondo hevi mpaka hivi ninavyowaambia majeraha ndiyo kwanza yanaanza kupoa na mara nyingi amekuwa akificha majeraha ya usoni kwa kujipaka make up kwa wingi kama akitaka kutoka. “Shov alimfumania baada ya kwenda kwa Mo anayeishi jirani na Gigy, akagonga mlango bila kuitikiwa ndipo alikuja mtu akamtonya kuwa amemuona Mo anaingia ny...

Tundu Lissu : Prof. Lipumba Hana Hoja, Anawavuruga CUF

Image
MBUNGE wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Tundu Lissu, amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Iblahim Lipumba amekosa hoja ya kuzungumza na badala yake anawavuruga wanachama wa CUF. Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema amesema Lipumba hakuwahi kuwa na idadi kubwa ya wabunge kama walivyo sasa tangu alipoanza kugombea urais zaidi ya kupata viti viwili tu lakini walipoungana mwaka jana katika umoja wao wa Ukawa wakaibuka  na viti 10. Mbunge wa Singida Mashariki ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheia Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari. (hawapo pichani). Kauli hiyo ameisema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo aliongeza kuwa Lipumba aache kukiandama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai ya kuwa kinaivuruga CUF. Aliongeza kuwa Lipumba kuendelea kutoa matamshi hayo kwa w...

PICHA TANO ZA MUONEKANO WA NDANI WA JENGO JIPYA LA J.K. NYERERE AIRPORT TERMINAL 3 JIJINI DAR

Image
Muonekano wa ndani wa jengo jipya la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam ambalo bado linaendelea na Ujenzi. Mafundi wakiendelea na kazi ndani ya jengo (terminal 3).

Viongozi wa EAC Wagoma Kusaini Mkataba wa Ulaya eac

Image
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC), imeiomba Jumuiya ya Ulaya (EU), iipe muda wa miezi mitatu kujua hatima ya wao kusaini Mkataba wa Kiuchumi na Jumuia hiyo (EPA). Uamuzi huo ulifikiwa jana Ikulu Dar es Salaam na viongozi wa Jumuiya hiyo baada ya kikao cha 17 kilichodumu kwa takribani saa sita. Akizungumza baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa EAC, Rais John Magufuli alisema kikao hicho kilikuwa na ajenda nne, ila ya EPA ilikuwa ngumu kulingana na uzito wake. Alitaja ajenda hizo kuwa ni ripoti ya mgogoro wa Burundi, kuingizwa rasmi kwa Sudan Kusini kwene Jumuiya, kupitishwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa EAC na EPA. Rais Magufuli alisema viongozi wote kwa pamoja walikubaliana kupewa muda wa miezi mitatu ili Sekretarieti ya EAC iangalie na kupitia masharti ya EPA kabla ya kusaini ili kila mmoja afaidike. Hata hivyo nchi ambazo zilishasaini makubaliano hayo kutoka Jumuiya hiyo ni Kenya. Alisema katika kikao hicho, walibaini mambo 10 ambayo yanapaswa kuangaliwa kabla ya ...

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 10.09.2016

Image

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image

Hatimaye Mtatiro ‘Amchana’ Prof. Lipumba, Amuita ni Jemedari Aliyekimbia Vita

Image
Dar es Salaam: Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amesema aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba amekiacha chama kwenye wakati mgumu baada ya kujiuzulu wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015. Agosti, mwaka jana, Profesa Lipumba alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kukabidhi barua kwa uongozi baada ya kushauriana kwa kipindi kirefu na viongozi na wazee wa chama hicho, akisema nafsi yake inamsuta kwa kuwa walikiuka malengo ya Ukawa. Hata hivyo, hivi karibuni Profesa Lipumba aliandika barua ya kutengua uamuzi wa kujiuzulu na uchaguzi ulipoitishwa ili kujaza nafasi hiyo hakuchukua fomu ya kugombea. Akizungumza katika mahojiano maalumu, Mtatiro amesema Profesa Lipumba amekitelekeza chama kikiwa katikati ya uwanja wa mapambano. Mtatiro aliyeteuliwa hivi karibuni na Baraza Kuu la CUF kuongoza kamati ya uongozi wa chama hicho baada ya kuvunjika kwa mkutano mkuu ulioitishwa kuziba nafasi ya mwenyekiti, amesema walijaribu kila mbin...

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 08.09.2016

Image
Posted by  PHARS MSIRIKALE at Thursday, September 08, 2016