Matukio Yanayoendelea Mkutano Mkuu wa CCM, Dodoma
Sehemu ya Meza kuu kama ionekanavyo pichani tayari wamekwisha ingia ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM ambaye leo anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Rais Dkt Shein pamoja na Mwenyekiiti mtarajiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa ratiba na miongozo mbalimbali kwa Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao tayari wako ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM. Mwanana mahiri wa nyimbo za Taarab kutoka kundi la Tot Plus Khadija Kopa akiimba mbele ya Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao tayari w