Posts

RAIS MAGUFULI ATEUA NAIBU AG NA MSHAURI WAKE WA UCHUMI

Image
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akisoma taarifa ya Uteuzi wa viongozi mbalimbali uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23 Mei, 2016 imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mar

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

Image
Mbunge wa CCM, Mhe. Mary Mwanjelwa akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge Mhe Najma Murtaza Giga akiwasili Bungeni kuongoza vikao vya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Mhe. Ally Keissy akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ameongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Jumanne Maghembe wakielekea Bungeni kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano, Mhe. Eng. Edwin Ngonyani akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Naibu Waziri, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Hamis Kingwangalla akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dod

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU NA JAJI MKUU IKULU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.PICHA NA IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman mara baada ya kumaliza mazungumzo yao  Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman Ikulu jijini Dar es Salaam.

www.phars.blogspot.com: Mkenya afunga ndoa na mwanamme mwenzake Mmarekani

www.phars.blogspot.com: Mkenya afunga ndoa na mwanamme mwenzake Mmarekani :   Bw.  Ben Gitau na Bw. Steve Damelin KATIKA matukio ambayo wanaume wa Kenya wanaoana na wanaume wenzao katika nchi zinazoruh...

Mkenya afunga ndoa na mwanamme mwenzake Mmarekani

Image
  Bw.  Ben Gitau na Bw. Steve Damelin KATIKA matukio ambayo wanaume wa Kenya wanaoana na wanaume wenzao katika nchi zinazoruhusu jambo hilo, mwanamme mmoja wa Nakuru, Kenya, amefunga ndoa na profesa wa hisabati wa Marekani. Bw.  Ben Gitau (33) na Bw. Steve Damelin walioana wiki iliyopita huko Ann Arbor, Michigan, Marekani, Jumamosi alasiri ambapo baada ya tukio hilo wawili hao walionekana wakibusiana na kukumbatiana ambapo marafiki na wanafamilia walipiga vigelegele na kushangilia. Hata hivyo, mshauri mmoja wa masuala ya kifamilia , Mchungaji Philip Kitoto wa International Christian Centre, Nairobi,alilaani ndoa hiyo akisema: “Kiutamaduni na kwa mujibu wa Bibilia,  ndoa na kujamiiana kati ya watu wa jinsia moja ni dhambi.” “Biblia iko wazi kwamba Mungu alituumba kwa taswira yake; mme na mke.  Katika kitabu cha Mambo ya Walawi 18:22 Mungu anamwonya  mwanaume kutofanya ngono na mwanaume  mwenzake  kama anavyofanya na mwanamke.” Bw.  Kararu Ririe, rafiki

BREAKING NEWS:KOCHA LUIS VAN GAAL ATIMULIWA,MAN UTD WACHUKUA MAAMUZI MAGUMU LEO

Image
Louis van Gaal has been sacked by Manchester United just two days after leading the club to the FA Cup Van Gaal was pictured arriving at United's Aon Training Complex on Monday morning ahead of his sacking Van Gaal's last act at Manchester United was lifting the FA Cup following his side's win over Crystal Palace Goalkeeper coach Frans Hoek (far left) and Albert Stuivenberg (far right) have also left the club along with Van Gaal, while Ryan Giggs (second left) could stay at the club Performance analyst Max Reckers (far left) has also been shown the Old Trafford exit door by United Jose Mourinho (left, pictured with Van Gaal) will take over the reins at Old Trafford following Van Gaal's sacking Mourinho (right) learned his trade under Van Gaal at Barcelona but will now replace his former boss Van Gaal's predecessor David Moyes was also sacked by Manchester United chief Ed Woodward Woodward (centre left) congratulates Van Gaal following United's 2-1 extra

Huu ndiyo ukweli wa Kitwanga Kuhusu Ulabu

Image
Stori:  Mwandishi Wetu, WIKIENDA DAR ES SALAAM: Ajali ya kisiasa! Gumzo kuhusu Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ kumtumbua Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Muhangwa Kitwanga (56) kwa madai ya kuingia bungeni akiwa ‘amechangamka’ bado liko vinywani mwa Wabongo huku sasa, upande wa pili wa hali hiyo ukijulikana, Ijumaa Wikienda limechimba. Ijumaa iliyopita, JPM alitengua uteuzi wake akidaiwa kuingia mjengoni akiwa amelewa hivyo kukosa umakini wakati akijibu maswali ya wizara yake. Habari zilizonaswa na Wikienda zinasema Kitwanga ni mnywaji lakini si kwa kiwango cha kukosa umakini kiasi cha kushindwa kutiririka vyema kwenye kujibu maswali, ila siku hiyo ilisababishwa na msongo. MSIKIE HUYU “Mimi sikatai ndiyo, Kitwanga anapiga ulabu, lakini yule jamaa yuko makini sana. Huenda siku ile alizidisha lakini naijua sababu. “Unajua siku za hivi karibuni, jamaa amekuwa akiandamwa sana na baadhi ya wabunge kuhusu sakata la Kampuni ya Lugumi na ufungwaji wa vifaa vya

SPIKA AWAFICHUA WABUNGE WAVUTAO BANGI NA UNGA,AJA NA MKAKATI MZITO

Image
Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe baada ya kufanya nae mahojiano juu ya hatua ya Rais Magufuli kumtimua Kitwanga katika baraza lake la mawaziri kwa sababu aliingia bungeni na kujibu swali la Wizara yake akiwa amelewa.Kutokana na hali hiyo Spika Ndugai amelieleza gazeti la Nipashe sasa wanafikiria kuweka vifaa maalumu vya kupima ulevi kwa watunga sheria hao na kutafuta wataalamu wa ushauri nasaha watakaowapa msaada wa kisaikolojia.

Madhara Ya Kula Mayai Yasipoiva Vizuri Kwa Afya

Image
Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips. Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri. Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai. Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza. Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaifa nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu. Hata u

Kauli ya Louis van Gaal baada ya Ubingwa wa Kombe la FA kwa Man United

Image
Baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la FA akiwa na Man United, Louis van Gaal amezungumza kauli ya kujivunia, licha ya kuwa kibarua chake kipo mashakani kuchukuliwa na Jose Mourinho kwa siku za usoni, licha ya kuwa mchana wa May 21 2016 ulianza kwa headlines zisizo njema kwake. Van Gaal ameripotiwa na Metro na AS kuwa atafukuzwa na Man United nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho, hiyo ilikuwa ni saa kadhaa kabla ya BBC na Sky Sports kuziongezea nguvu taarifa hizo, kwa kuripoti habari kama hizo katika tovuti zao. Louis van Gaal amekuwa akiandamwa na tetesi zinazohusu hatma ya kibarua chake, aliongea kauli zya kujivunia kama hana hofu na habari zinazoendelea.‘Hii ni furaha kubwa kwa klabu na mashabiki na kwangu pia ambaye nimefanikiwa kushinda taji hili nikiwa katika nchi nne tofauti ni makocha wachache wanaoweza kujivunia hilo, hivyo nina furaha sana na jambo hili”

Kiba, Diamond Kimenuka Hatari!

Image
    Kimenuka! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mafahari wawili wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kutupiana vijembe vya kufa mtu baada ya kuwepo kwa madai ya Kiba kuhujumiwa.       Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Kwa mujibu wa chanzo makini, ili kuweka hujuma ya kibiashara, hivi karibuni, pamoja na kukanusha mara kadhaa kutokuwa na tatizo na Kiba, Diamond alidaiwa ‘kutengeneza’ kwa makusudi penzi la mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe na msanii wa Wasafi Classic Baby (WCB), Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’ kisha kuvujisha video ya uhusiano huo mpya siku ambayo Kiba alikuwa akiuachia wimbo wake mpya wa Aje (Jumamosi iliyopita), lengo likiwa kuhamisha upepo mashabiki kutoka kwenye wimbo mpya na kujali mapenzi ya wawili hao. “Ni hujuma ya kibiashara, Diamond na uongozi wake wameamua kumfanyia Kiba ili wimbo wake ukose kiki kwa watu,” kilidai chanzo chetu. Harmonize VIJEMBE VYATAWALA Hata hivyo, kwa muji

TAARIFA KUTOKA KWA FAMILIA YA MAREHEMU WILSON KABWE KUFUATIA UPOTOSHWAJI WA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI

Image
Familia ya Marehemu Wilson Kabwe  imesikitishwa sana na taarifa zilizosambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu kauli na msimamo wa familia katika shughuli za maazishi ya mpendwa wao Wilson Kabwe. Familia inapenda kuchukua nafasi hii kutamka bayana kwamba, Dk. Zawadi Machuve si msemaji wa familia. Kauli yake iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba:- " Sisi hapa hatukaribishi viongozi, huu ni msimamo wa familia kama wao watafanya utaratibu wao sawa, lakini hatuko kwa ajili ya viongozi" Kauli hiyo ambayo ililenga kutoishirikisha Serikali katika msiba wa mtumishi wake tunaomba ipuuzwe na siyo kauli ya familia. Familia inatambua na inathamini sana mchango mkubwa wa Serikali katika kugharamia matibabu na  huduma  zote za mazishi. Familia inachukua fursa hii kuwakaribisha viongozi wote wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki wanaopenda kushiriki katika shughuli za mazishi ya mpendwa wetu. Imetolewa na: PHILIP MKENGA KABW

JEMBE FESTIVAL YAWAKUNA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA

Image
Msanii kutoka nchini Marekani Neyo akishambulia jukwaa na kuwapagawisha wakazi wa jiji la Mwanza . Neyo akiwa pamoja na Diamond Platnumz jukwaani wakiambulisha wimbo wao mpya mbele ya mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya. Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ruby akiimba kwenye tamasha la Jembe Festival kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Rapa Stamina akiupagawisha umma na mistari iliyo simama kwenye tamasha la Jembe mjini Mwanza. Mr. Blu akirap nyimbo zake zilizompa umaarufu kwenye tamasha la Jembe lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Diamond Platnumz na vijana wake wakishambulia jukwaa kwenye tamasha la Jembe lililofanyika kwenye viwanja vya CCM Kirumba mjini Mwanza. Mgeni rasmi wa tamasha la muziki la Jembe , Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM Dk. Sebastian Ndege kwenye chumba maalum nyuma ya jukwaa ,CCM Kirumba . BOFYA HAPA KWA PI