Mkenya afunga ndoa na mwanamme mwenzake Mmarekani
Bw. Ben Gitau na Bw. Steve Damelin
KATIKA matukio ambayo wanaume wa
Kenya wanaoana na wanaume wenzao katika nchi zinazoruhusu jambo hilo,
mwanamme mmoja wa Nakuru, Kenya, amefunga ndoa na profesa wa hisabati wa
Marekani.
Bw. Ben Gitau (33) na Bw. Steve Damelin
walioana wiki iliyopita huko Ann Arbor, Michigan, Marekani, Jumamosi
alasiri ambapo baada ya tukio hilo wawili hao walionekana wakibusiana na
kukumbatiana ambapo marafiki na wanafamilia walipiga vigelegele na
kushangilia.
Hata hivyo, mshauri mmoja wa masuala ya
kifamilia , Mchungaji Philip Kitoto wa International Christian Centre,
Nairobi,alilaani ndoa hiyo akisema: “Kiutamaduni na kwa mujibu wa
Bibilia, ndoa na kujamiiana kati ya watu wa jinsia moja ni dhambi.”
“Biblia iko wazi kwamba Mungu alituumba
kwa taswira yake; mme na mke. Katika kitabu cha Mambo ya Walawi 18:22
Mungu anamwonya mwanaume kutofanya ngono na mwanaume mwenzake kama
anavyofanya na mwanamke.”
Bw. Kararu Ririe, rafiki wa karibu wa
wanandoa huyo ambaye ni Mkenya aliyewahi kukiri kwamba ni shoga
anayeishi California, Marekani, alitume ujumbe kwenye mtandao wa twitter
baada ya ndoa hiyo akiandika kwamba: “Jioni hii nilimpongeza rafiki
yangu, Ben na mumewe Steve, kwa ndoa yao. Ni jambo adimu kwa Mkenya
kuwa jasiri kiasi hicho. Hongera.”
Gitau alikuwa anaishi Atlanta, Georgia, kabla ya kuhamia California.
Kwa mujibu wa mwanafamilia mmoja aliyezungumza na gazeti la Daily
Nation, Gitau alikutana na mchumba wake huko Atlanta ambako Damelin
alikuwa mwanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD) katika Chuo cha
Teknolojia cha Georgia.
Katika kulaani tukio hilo, Mchungaji
Kitoto alisisitiza kwamba tendo la ndoa kati ya mwanamme na mwanamke
liliwekwa kwa ajili ya uzazi.
Ndoa za jinsia moja zilihalalishwa
katika Jimbo la Michigan mwaka jana mwezi Julai na Mahakama Kuu ya
Marekani iliyoondoa sheria zinazopinga ndoa za watu wa jinsia moja mradi
tu wawe wanapendana.
Source: Daily Nation
Comments
Post a Comment