Posts

LEICESTER CITY YAKABIDHIWA KOMBE LAO LA LIGI KUU ENGLAND

Image
 Leicester City wamesherekea ubingwa wao wa Premier League ambao ni wa kwanza katika historia ya klabu hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 132 iliyopita. Furaha hiyo imechagizwa na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa King Power. Leicester wamekabidhiwa rasmi ubingwa wao baada ya kujihakikishia kutwaa taji hilo tangu siku ya Jumatatu wakati Tottenham iliposhindwa kuifunga Chelsea. Klabu hiyo imeandika historia ambayo imeuteka ulimwengu ambapo nahodha Wes Morgan pamoja na kocha Claudia Ranieri kwa pamoja walinyanyua taji la Premier League baada ya kumaliza safari ya kupambana kutoshuka daraja hadi kutwaa ubingwa katika kipindi cha miezi 12. Ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton ulikuwa unaendelea kudhihirisha uwezo, kujitoa na ubora uliowapa ubingwa, lakini siku ya Jumamosi ya May 7 ni zaidi ya mchezo wa soka kutokana na kufunikwa na hisia za kila aina.

DUNIA INA MAMBO MAZITO BI HARUSI AMPA SUMU MUMEWE

Image
Msichana mdogo alieolewaBi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake. Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu. Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa. Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho. Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi zimekithiri. Msichana huyo wa miaka 7...

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA BI LUCY KIBAKI

Image
 Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.  Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.  Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.

RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA 586 KATIKA CHUO CHA MAAFISA WA JESHI MONDULI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Afisa Mpya wa cheo cha Luteni Usu, Nasra Rashid ambaye alifanya vizuri zaidi kuliko Maafisa Wanafunzi wanawake katika chuo c...

Diamond na Kampuni yake ya Music WCB Yamzawadia Gari Jipya Harmonize

Image
WCB imemzawadia gari jipya msanii wake, Harmonize. Bosi wake, Diamond, ameandika kwenye Instagram: Kama nikusiivyo siku zote ni juhudi na nidhamu yako ndio itayokufanya upate matunda ya kazi yako….. Usiache unyenyekevu, kuheshimu mkubwa na mdogo, kumuomba na kumshukuru Mwenyez Mungu kwa kila hatua ndogo Uipigayo…. Congrats kwa your New Ride.” Naye Harmonize hakuacha kuonesha furaha yake. “Nichukue fursa fupi kuushukuru uongozi wangu mzima wa @wcb_wasafi @mkubwafella @babutale @sallam_sk @ricardomomo @diamondplatnumz kwa kunijali na kunithamini kijana wao wakanizawadia gari daaaaah furaha niliyo nayo haielezeki,” ameandika msanii huyo. “Kwakweli nina furaha na ninashukuru sanaa nina mengi ya kuongea lakini sizani kama nikianza kuandika nitamaliza kubwa ni kwamba namshukuru m/mungu nashukuru kwa kurudia tena uongozi wangu @wcb_wasafi kwa zawadi lakini nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipo washukuru wazazi wangu walio nizaa na kunilea hadi nikafikia hapa na shukrani za ...

HUYU NDO TRAFIKI ANAYE ONGOZA KWA VITUKO KWA STYLE YAKE YA KUONGOZA MAGARI

Image
HUYU ASKARI ANAITWA CONSTABLE ASHRAF …AMEKUWA KIVUTIO KIKUBWA KWA JINSI ANAVYO KUWA ANAONGOZA MAGARI KWA KUTUKIA INSHARA MBALIMBALI AMBAZO NDO HUWAVUTIA WATU WENGI WANAO PITA NJIA HIYO…YEYE HUPATIKANA BARABARA YA HASSAN MWINYI MAENEO YA KIJITONYAMA SAYANSI.

List ya Wanawake Wanaomiliki ndege zao yani....Private Jet zao Binafsi Hawa Hapa

Image
Kwa takwimu zilizofanyiwa uchunguzi zinasema kuwa Nigeria ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na wamiliki wa ndege binafsi almaarufu kama private jet ambazo ziko zaidi ya ndege 177 ambazo zinamilikiwa na matajiri kama Aliko Dangote pamoja na David Oyedepo ambao ni kawaida kwa matajiri kumiliki vitu vya thamani kama hivi sasa nimekuletea list ya wanawake kutoka barani Africa wakiwa wanamiliki ndege zao binafsi hawa hapa 1.Anajulikana kwa jina la  Folorunsho Alakija ameolewa pia ni mfanyabiahara na mjasiriamali kutoka Nigeria  2. Diezani Alison-Madueke akiwa ni Waziri wa petrol kutoka Nigeria mafanya biashara wa mafuta kutoka Nigeria 3. Bola Shagaya huyu ni mwasiasa lakin pia anajishughulisha na biashara za mafuta kutoka Nigeria amenunua ndege yake siku za karibuni kabisa  4. Daisy Danjuma huyu ni mke wa Billionea Theophilus Danjuma ambapo amepewa ndege binafsi na mumewe kama zawadi katika siku yake ya kuzaliwa kutoka kwa mumewe

HII NDO SHERIA MPYA YA GUEST HOUSE DAR…Kabla ya kupewa chumba mnapigwa picha?

Image
Ijumaa ya May 6 2016 kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hususani Whatsapp najua utakuwa ulipokea ujumbe ambao ulikuwa unaripotiwa kuwa umetoka kwa meya  wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, ujumbe uliokuwa umeenea ulikuwa unahusisha kuwa meya wa Dar es Salaam Isaya Mwita ametangaza sheria mpya. Meya Isaya Mwita ameeleza kuwa ujumbe unaoenea kuwa ametangaza sheria mpya Dar es Salaam sio wa kweli na umetungwa na watu ambao wanapanga kumchafulia jina lake. Ujumbe wa uongo ambao ulisambazwa leo May 6 2016 na kudaiwa umetoka kwa meya wa Dar es Salaam “Sio kweli kuwa kuna sehemu nimetoa statement ya namna hiyo ila huyo atakayekuwa ameandika atakuwa na lengo tofauti, kwa hiyo naomba wananchi wapuuze hiyo statement ambayo imekuwa ikisambaa, bahati mbaya sikuwahi kupata mtu akiuliza maoni yoyote kuhusiana na tukio hilo la Kimara ila kwa upande wangu sijatoa tamko lolote”

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 07.05.2016

Image