DAVID DE GEA AWEKA REKODI USIKU WA TUZO MAN UNITED
David De
Gea ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji
bora wa Manchester United kwa mara ya tatu mfululizo baada ya Jumatatu
usiku kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo.
De Gea
ametwaa tuzo hiyo maarufu kama Matt Busby player of the year ikiwa ni
baada ya kutoruhusu kufungwa bao lolote katika michezo 14 kati ya 32 ya
Ligi Kuu England aliyoicheza Manchester United msimu huu wa 2015/2016
huku pia akifanya vizuri katika michuano ya kombe la FA.Mbali ya De Gea
nyota mwingine aliyewahi kutwaa tuzo hiyo kubwa zaidi mara tatu lakini
katika vipindi tofauti ni Mreno Cristiano Ronaldo. Ronaldo alitwaa tuzo
hiyo mwaka 2004, 2007 na 2008.
Akiongea
baada ya kutwaa tuzo hiyo De Gea amesema: “Ni ngumu kusema chochote,
kutwaa tuzo hii mara tatu mfululizo ni faraja na heshima kubwa. Napenda
kuwashukuru mashabiki wetu ambao ni bora zaidi duniani”.
Wengine
walioshinda tuzo Jumatatu usiku ni: Chris Smalling aliyetwaa tuzo ya
mchezaji bora wa mwaka chaguo la wachezaji (United’s Players’ Player of
the Year), Cameron Borthwick-Jackson aliyetwaa tuzo ya mchezaji wa mwaka
kwa wachezaji wa U-21(Under-21 Player of the Year) huku Marcus Rashford
akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wa U-18 (Under-18
Player of the Year).
Comments
Post a Comment