Watuhumiwa wa ujambazi, wala kichapo hevi Kariakoo
WATU wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wamenaswa leo Kariakoo jijini Dar es Salaam na kupewa kichapo ‘hevi’ kutoka kwa wananchi wenye hasira kali waliokuwa eneo la tukio. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, majambazi hao wawili akiwemo mmoja ambaye ni raia wa Kihindi wamekamatwa Mtaa wa Swahili na Mchikichi, Kariakoo na wanadai raia huyo wa Kihindi anajulikana kwa jina la Samir.