MABADILIKO YA MUDA WA MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI SIKU YA JUMANNE TAREHE 19 APRILI 2016
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa Daraja la
Kigamboni kesho, Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016.
Kutokana
na ufunguzi huo, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu
watumiaji barabara na Wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma
ya magari kutumia daraja hilo itafungwa kwa muda kuanzia saa 1:00
asubuhi hadi saa 8:00 mchana ili kuwezesha kufanyika kwa sherehe hiyo ya
ufunguzi wa daraja. Aidha, huduma katika Daraja la Kigamboni itarejea
kama kawaida kuanzia saa 8:00.
Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
18 Aprili, 2016
Comments
Post a Comment