Posts

MAJALIWA AWASILI DODOMA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana  (kulia) , Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (Wapili kushoto) na Mbunge wa  Nachingwea, Hassan Masala baada ya kuwasili kwenye uwanja w ndege wa Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiw kuanza Arili 19, 2016.. Watatu kulia  Mbunge wa Bunge  la Afrika ya Mashariki Adam Kimbisa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana  (kulia) , Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (Wapili kushoto) na Mbunge wa  Nachingwea, Hassan Masala baada ya kuwasili kwenye uwanja w ndege wa Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiw kuanza Aprili 19, 2016.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MABADILIKO YA MUDA WA MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI SIKU YA JUMANNE TAREHE 19 APRILI 2016

Image
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa Daraja la Kigamboni kesho, Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016. Kutokana na ufunguzi huo, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu watumiaji barabara na Wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya magari kutumia daraja hilo itafungwa kwa muda kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana ili kuwezesha kufanyika kwa sherehe hiyo ya ufunguzi wa daraja. Aidha, huduma katika Daraja la Kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia saa 8:00. Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi  (approach roads)  upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.  Imetolewa na; Eng. Joseph M. Nyamhanga Katibu Mkuu  (Ujenzi) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano 18 A

KIGOGO WA DAWA ZA KULEVYA HOFU YATANDA SHKUBA KUTOROKA GEREZANI

Image
Ali Khatib Haji ‘Shkuba’. Stori: Hashim Aziz na Makongoro Oging’, UWAZI Kufuatia kuendelea kushikiliwa kwa kigogo anayedaiwa kujishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’, Ali Khatib Haji ‘Shkuba’ (pichani) katika Gereza Kuu la Mkoa wa Lindi, hofu imezidi kutanda kwa madai kwamba, mfanyabiashara huyo yupo kwenye maandalizi ya kutoroka gerezani hapo, Uwazi limechimba kwa kina. BOMBA LA MAJI LATAJWA Habari zilizolifikia gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita na kutiliwa nguvu na hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea gereza hilo, zilieleza kwamba, kuna ‘mchongo’ unaofanywa na vigogo kadhaa wa unga kwa lengo la kumtorosha Shkuba, wakitumia kivuli cha mradi wa kuingiza bomba la maji gerezani hapo ambapo pengine hata wenye mradi huo hawajui lolote. “Kuna bomba linachimbwa kuingia gerezani, wenyewe wanasema ni mradi wa kulipatia gereza hilo maji lakini kuna tetesi kwamba huenda bomba hilo ndiyo njia ya kutaka kumtolea Shkuba gerezani lakini weny

RAIS MAGUFULI ATINGA BENKI YA CRDB NA GARI BINAFSI

Image
Muuza maji (kushoto) akishangaa gari alilopanda Rais Magufuli leo asubuhi wakati akitoka Benki ya CRDB tawi la Holland. Gari alilokuwa amepanda Rais John Magufuli lenye namba za usaji T 182 DGQ likitoka katika benki ya CRDB tawi la Holland lililopo katika makutano ya barabara ya Samora na Ohio jijini Dar es Salaam. Rais John Magufuli akiwa ndani ya gari lenye namba za usajili T182 DFQ huku akiwapungia mkono watu waliokuwa nje ya Benki ya CRDB tawi la Holland jijini Dar es Salaam jana, wakati akitoka katika benki hiyo. (Picha na Francis Dande) RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezua taharuki mjini leo baada ya kufika katika Tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari binafsi lenye namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya adamu na hawa wala bendera. Tukio hilo lililochukuwa takribani dakika 25, limetokea majira ya saa nne asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam katika tawi la benki hiyo ambalo liko katika makutano ya

Kova aibuka sakata la Lugumi

Image
Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Stori: Ojuku Abraham, UWAZI DAR ES SALAAM: Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (pichani) ameibuka kufuatia ‘kubumburuka’ kwa sakata linalomhusu mfanyabiashara Said Lugumi, anayemiliki kampuni ya Lugumi Enterprises inayodaiwa kuingia mkataba tata na Jeshi la Polisi Tanzania. Mkataba kati ya Lugumi Enterprises na jeshi hilo ulisainiwa mwaka 2011, ulihusu kufungwa kwa vifaa vya kuchukulia alama za vidole katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya shilingi bilioni 37. Lakini hadi sasa, vifaa hivyo vimefungwa katika vituo 14, vyote vikidaiwa kuwa ni vya Dar es Salaam lakini bila kujulikana sehemu. Kova, ndiye aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam wakati vifaa hivyo vikifungwa katika vituo 11 vya Polisi huku ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi ikiwa chini ya Said Mwema. Kampuni hiyo inadaiwa kulipwa karibu asilimia 99 ya fedha zote za makubaliano.  

BREAKING NEWS : MSANII TUNDA MAN APATA AJALI MBAYA IRINGA

Image
  Taswira za ajali aliyoipata Tundaman leo. Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakua umekutana na taarifa inayomhusisha Tunda Man kupata ajali  akiwa Mkoani iringa Asubuhi ya April 17   Tunda Man. Maelezo ya mwanzo ya   Tunda Man   amesema ‘ Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki ‘ Tunda Man   anamalizia kwa kusema ‘ Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu

PAPA FRANCIS AWACHUKUA WAKIMBIZI 12 NA KUWAKARIBISHA KUISHI ROMA

Image
Papa Francis leo amewakaribisha wakimbizi 12 wa Syria wakati wakiwasili Jijini Roma baada ya kuwachukua kutoka kwenye kambi ya Lesbos kufuatia ziara yake katika kisiwa hicho cha Ugiriki. Familia tatu za wakimbizi wa Syria walipanda ndege ya Papa Francis punde tu baada ya ziara yake hiyo ya Lesbos kuangazia mgogoro wa kibinadamu unaotokana na wakimbizi.                  Papa Francis akiwakaribisha wakimbizi wa Syria aliowachukua Lesbos Msemaji wa Vatican amesema Papa Francis ameamua kuonyesha ishara ya kuwakaribisha wakimbizi hao kwa kuwachukua kukaa Roma ambao miongoni mwao wamo watoto sita.               Papa Francis akimbusu mtoto mkimbizi wakati wa ziara yake ya Lesbos                          Papa Francis akisalimiana na wakimbizi waliopo Lesbos Ugiriki

WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA TABIA/AINA HII

Image
Habari za wiki hii mpenzi msomaji. Mimi namshukuru Mungu kwa kuweza kunikutanisha na nyinyi kupitia safu hii ambayo pamoja na mambo mengine nazungumzia juu ya mada mbalimbali ambazo zinagusa maisha yetu ya kila siku. Wiki hii nitazungumazia juu ya aina ya wanawake ambao wanaume wengi hupendelea kuoa. Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha. Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri. Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzur