Posts

WAHAMIAJI HARAMU RAIA WA ETHIOPIA WANASWA NA POLISI MIKUMI MORO NDANI YA NOAH KUTOKEA CHALINZE KUELEKEA TUNDUMA..

Image
   Gari walilokuwa wakitumia w ahamiaji    haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa likiwa nje ya je ngo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.   Wahamiaji    haramu wa Ethiopia waliokamatwa na Polisi,    jana wakiwemo na watanzania wawili ,eneo la Mikumi, wilayani Kilosa    katika barabara kuu ya Mikumi- Iringa, wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi eneo la viwanja vya    Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.    Wahamiaji    haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa wakiwasili  eneo la viwanja vya    Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.     Wahamiaji    haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa wakiwasili  eneo la viwanja vya    Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro. Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, akielezea jambo kwa waandishi wa habari , mbele ya wahamiaji    haramu wa Ethiopia waliokamatwa usiku wa kuamkia Februari 2, mwaka huu   pamoja    na watanza

Mwakyembe, Mdee watunishiana misuli kuhusu Kashfa ya Mabehewa Mabovu

Image
Add caption Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe na Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee (Chadema), jana waliingia kwenye mvutano mkali huku wakitunishiana misuli ya sheria kuhusu kashfa ya ununuzi wa mabehewa 274 yanayodaiwa kuwa mabovu. Ununuzi uliofanywa wakati Dk. Mwakyembe alipokuwa Waziri wa Uchukuzi. Mdee aliibua tena suala la kashfa ya ununuzi wa mabehewa hayo 274 akisisitiza kuwa ni mabovu, wakati alipopata nafasi ya kuchangia katika Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2011/- 2015/16 ambapo aligusia ahadi ya serikali ya kukarabati reli ya kati  ambayo alidai haijatekelezwa ipasavyo. Dk. Mwakyembe alikanusha taarifa ya kuwepo kwa mabehewa mabovu kati ya mabehewa hayo 274 yaliyonunuliwa wakati akiwa Waziri wa Uchukuzi. “Leo nikimwambia Halima aniletee mabehewa ambayo hayafanyi kazi atashindwa kunionesha,” alisema. Waziri huyo alieleza kuwa mkataba wa ununuzi wa mabehewa hayo ulitoa mwanya wa kufanya ukarabati au marekebisho katika bidhaa husik

‘Birthday’ ya Nicolaus Trac yafunika Maisha Basement

Image
Meneja Masoko wa  Maisha Basement, Gilla, akimkaribisha Mfanyakazi wa Global, Nicolaus Trac (kushoto) akiwa na Video Queen wa Bongo, Kidoa Salum ‘Akadumba’,  katika usiku wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Nicolaus Trac uliofanyika Maisha Basement jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Kidoa akikata keki na Nicolaus. Msanii wa Filamu Bongo, Salima Jabu ‘ Nisha ‘ (katikati) akiongea jambo, akiwa na DJ Choka (kulia) na Kidoa Salum (kushoto). Kidoa akisalimiana na Nisha. Nicolaus Trac akimlisha keki Nisha. Dj Choka akilishwa keki. Meneja wa Burudani wa Maisha Basement, Hemed Kavu ‘HK’ akimulisha keki Birthday Boy, Nicolaus Trac. Nicolaus akimlisha keki Clarence Mulisa. Msanii wa Nyimbo za Asili Bongo, Dat akilishwa keki. Meneja Masoko wa Maisha, Gilla ‘The Boss’ akilishwa keki. Meneja Masoko wa Global Publishers, Innocent Mafuru, akilishwa keki. Kidoa Salum akilishwa keki na shabiki wake. Kidoa (kulia) akimlisha keki shabiki yake. Musa

SUMAYE AIANGUKIA SERIKALI WANANCHI KUVAMIA SHAMBA LAKE LA EKARI 33 MABWEPANDE

Image
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye  Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kuwasili eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kuangalia eneo la ekari 33 la Sumaye lililovamiwa na wananchi.   WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (wa pili kulia), na mke wake mama Esther (kushoto), wakimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia) eneo la shamba lake la ekari 33 lililopo Mabwepande Manispaa ya Kinondoni lililovamiwa na wananchi walipotembea eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.   Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo.   DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe.   Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake.   Mhe. Sumaye akielezea uhalali wake wa kumiliki eneo hilo.   Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya,  Justine Chiganga (kulia), akizungumza katika mkutano huo