SUMAYE AIANGUKIA SERIKALI WANANCHI KUVAMIA SHAMBA LAKE LA EKARI 33 MABWEPANDE
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu
mstaafu, Fredrick Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya
kuwasili eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam
kuangalia eneo la ekari 33 la Sumaye lililovamiwa na wananchi.
WAZIRI
Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (wa pili kulia), na mke wake mama Esther
(kushoto), wakimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
(kulia) eneo la shamba lake la ekari 33 lililopo Mabwepande Manispaa ya
Kinondoni lililovamiwa na wananchi walipotembea eneo hilo Dar es Salaam
leo asubuhi.
DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe.
Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake.
Mhe. Sumaye akielezea uhalali wake wa kumiliki eneo hilo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya, Justine Chiganga (kulia), akizungumza katika mkutano huo
Moja ya kibanda kilichojengwa na wananchi waliovamia eneo la Mhe Sumaye.
Baadhi ya vibanda vilivyojengwa na wananchi katika eneo la Sumaye.
Askari Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa mchakato wa kutembelea eneo hilo lililovamiwa.
Wananchi wa eneo la Mabwepande wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkazi wa eneo hilo Athuman Mnubi akielezea jinsi walivyovamia eneo la Sumaye.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabwepande Abdalla Omari Kunja akizungumza katika mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Ardhi Manispaa ya Kinondoni, Matinga Ernest akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Ardhi katika Manispaa hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
WAZIRI
Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, ameiangukia serikali na kuomba msaada
baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la ekari
33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam.
Serikali
imemuahikikishia Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge
wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki
mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo.
Akizungumza
katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji cha Kimondo mtaa
wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi,
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro
huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali
kuingilia kati ni lazima busara kutumika.
Alizitaka
pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia
bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuache kuendelea
na ujenzi na kugawiana maeneo katika shamba hilo.
“Serikali
ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza
Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi ili kutenda haki
tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna
mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema.
Alisema
katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika
kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli
hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili
kutafuta suluhu.
Zipo
njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa
kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi
kama ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali tuchukue,”alisema.
Alisema
pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa
kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi hao ambao hawana makazi au
Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.
Alizitaka
pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo
kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.
Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye.
Awali
katika mkutano huo Sumaye alimueleza Makonda jinsi serikali ilivyo na
kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia busara
zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.
“Mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu
sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli
eneo hili namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka na
nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa
kujenga Chuo Kikuu,”alisema.
Alisema yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.
Diwani
wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo
lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha
uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu
mbalimbali.
Alisema
kutokana na hatua hiyo walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na
ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha
maji alikataa kuwapa wananchi .
Suzan
alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii
kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo
cha polisi waliamua kuvamia na kujigaia maeneo.
Mmoja
wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa
eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo
uliotelekezwa na Sumaye.
Alisema
wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora
maeneo yaliyotelekezwa na wawekezaji watasaidiwa.
WAKATI
huo huo Makonda alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na
mchanga, wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India Sules Waljan
wanaochimba mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande.
Hatua
hiyo imekuja baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na
alipowahoji wafanyakazi na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema
hawana.
Makonda
amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill ili kutoa
maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa
uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo vya maji na
matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni makubwa.
Comments
Post a Comment