WAHAMIAJI HARAMU RAIA WA ETHIOPIA WANASWA NA POLISI MIKUMI MORO NDANI YA NOAH KUTOKEA CHALINZE KUELEKEA TUNDUMA..
Gari walilokuwa wakitumia wahamiaji haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa likiwa nje ya jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
Wahamiaji haramu wa Ethiopia waliokamatwa na Polisi, jana wakiwemo na watanzania wawili ,eneo la Mikumi, wilayani Kilosa katika barabara kuu ya Mikumi- Iringa, wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi eneo la viwanja vya Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
Wahamiaji haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa wakiwasili eneo la viwanja vya Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
Wahamiaji haramu wa Ethiopia ( mbele ) waliokamatwa wakiwasili eneo la viwanja vya Jengo la Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi mjini Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, akielezea jambo kwa waandishi wa habari , mbele ya wahamiaji haramu wa Ethiopia waliokamatwa usiku wa kuamkia Februari 2, mwaka huu pamoja na watanzania wawili eneo la Mikumi, wilayani Kilosa katika
barabara kuu ya Mikumi- Iringa, baada ya kuwapatia mji wa Chalinze na
kwenda nao Tunduma ili wavuke mpaka kuelekea Afrika Kusini. Picha na
John Nditi
Na John Nditi, Morogoro
POLISI
mkoani hapa leo imewatia mbaroni wahamiaji haramu 12 kutoka nchini
Ethiopia pamoja na watanzania wawili katika eneo la Mikumi, barabara kuu
ya Morogoro- Iringa.
Wahamiaji
hao haramu walikamatwa usiku wa kuamkia Februari 2, mwaka huu majira ya
saa nane na nusu usiku wakiwa katika gari lenye namba za usajili T 876
BHZ aina ya Toyota Noah , iliyokuwa ikiwndeshwa na Kimu Mustafa (25)
mkazi wa Segera, mkoani Tanga akiwa na Kondakta wake aitwaye Rashid
Ally (17) pia mkazi wa Segera Tanga.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonaerd Paulo, dereva
wa gari na kondakta wake walieleza kuwa walielekezwa na tajiri wao
kuwapakia wahamiaji haramu hao kutoka Mji wa Chalinze , mkoa wa Pwani.
Kamanda
huyo alisema, kwa mujibu wa dereva huyo , kuwa tajiri wake alimpingia
simu akiwa Segera na kumwelekeza kuwa aende Chalinze kuwachukua watu na
kuwapeleka hadi Tunduma kwa vile walikuwa wakienda nchi ya Afrika
Kusini.
Kamanda
Paulo alisema kuwa uchunguzi wa awali umeonesha kuwa wahamiaji haramu
hao walikuwa wanasafirishwa hadi Tunduma ili baadaye waelekee Afrika
Kusini.
Amesema
watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na kuwatafuta wafadhili wa biashara
hiyo haramu na baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa Mahakamani.
Comments
Post a Comment