Nora adaiwa kuwa chizi tena!
Mwigizaji wa kitambo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’. Na Brighton Masalu NURU Nassoro ‘Nora’ ambaye ni mwigizaji wa kitambo Bongo,anadaiwa kuugua uchizi kwa mara nyingine tena, jambo ambalo amelipinga vikali na kwamba wabaya wake wameendelea kumtakia mabaya katika maisha yake, lakini yuko safi na anaendelea na maisha yake. Mwanzoni mwa wiki hii, mmoja wa rafiki zake wa karibu aliliambia gazeti hili kuwa, uzushi na uvumi huo ulianza kuenezwa wiki mbili zilizopita, hali iliyosababisha watu wengi, kuanza kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS),wakitaka kuthibitisha uvumi huo, hali iliyomuumiza msanii huyo. Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Nora kupitia simu yake ya mkononi ambapo alikiri kukumbwa kukutana na madai hayo huku akionesha masikitiko makubwa juu ya uvumi huo. “Mwenyewe nilishangaa sana, nilishindwa kujua ni kwa nini watu wanaendelea kunitakia mabaya kiasi hiki, nilianza kupokea simu kutoka kwa watu wangu wa karibu wakiniuliza kulikoni, lakini ...