Kajala ajiachia na dada’ke diamond!
- Get link
- X
- Other Apps
Mwigizaji Kajala Masanja akiwa na Queen Darleen wakiponda raha.
Na Musa Mateja
HUKU kukiwa na madai kwamba mwigizaji Kajala Masanja ana uhusiano wa ‘kikubwa’ na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwigizaji huyo amezidi kuyachochea moto madai hayo kwa kutokana na kujiachia mara kwa mara na dada wa Diamond, Queen Darleen, Risasi Mchanganyiko linakujuza.
HUKU kukiwa na madai kwamba mwigizaji Kajala Masanja ana uhusiano wa ‘kikubwa’ na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwigizaji huyo amezidi kuyachochea moto madai hayo kwa kutokana na kujiachia mara kwa mara na dada wa Diamond, Queen Darleen, Risasi Mchanganyiko linakujuza.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala na Queen Darleen wamekuwa ‘beneti’ kila kona ambapo pia kuna fununu kuwa hata familia ya Diamond imebariki uhusiano wake na Mbongo Fleva huyo na wanampa ushirikiano wa kutosha Kajala.
“Fuatilieni tu, Kajala ameshakubalika kwa kina Diamond, ndiyo maana leo utaona Kajala na dada yake Diamond, Queen Darleen wanapiga misele pamoja, hata katika viwanja vingi vya starehe wanakwenda wote,” kilisema chanzo hicho.
…..Wakifurahia jambo.
Mwishoni mwa wiki hii, paparazi wetu aliwanasa laivu Kajala na Queen Darleen katika fukwe za White Sands, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam walipokuwa wameenda kupunga upepo na kuwapeleka watoto wao kuogelea.
Kuonekana kwa wawili hao kuliibua gumzo la aina yake ambapo wafuatiliaji wa ‘ubuyu’ walionekana kunong’onezana kuwa yale waliyokuwa wakiyasikia na kuyasoma kwenye mitandao kuwa Kajala ana uhusiano na Diamond, yana ukweli.
Ili kukamilisha ubuyu huo, mwanahabari wetu alimuibukia Kajala aliyekuwa ameambatana na mwanaye Paula pamoja na baunsa wake, ili aweze kuzungumzia ukaribu wake huo na Queen ambao umeleta tafsiri kuwa ni mtu na wifi yake. Kajala akafunguka:
Kwa upande wake, Queen Darleen alisema mwenye macho haambiwi tazama!
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment