Posts

KORTINI KWA TUHUMA NJAMA ZA KUTAKA KUMUUWA MWENYEKITI WA NEC JAJI LUBUVA

Image
WATU wawili wakiwemo Mwanasheria na Mwalimu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama za kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva na familia yake. Washitakiwa hao, Mwalimu Samwel Gikaro (30) na Mwanasheria Angela Mbonde (32) walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba. Wakili wa Serikali, Hellen Moshi alidai kati ya Oktoba 23 na Novemba 16, mwaka huu katika maeneo tofauti Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, washitakiwa na wengine ambao hawajafika mahakamani, walikula njama za kumuua Jaji Lubuva na familia yake. Washitakiwa walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa upande wa utetezi, Moses Kaluwa ambaye alifika mahakamani hapo kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala, aliiomba mahakama itoe dhamana kwa washitakiwa kwa kuwa mashi

BREAKING NEWZZZ!!!! ABOUBAKAR KASONGO MPINDA ‘CLAYTON’ AFARIKI DUNIA

Image
King Kiki (kulia) akiimba sambamba na Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ enzi za uhai wake. Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ akiwa na Issa Nundu (kulia). Na Sifael Paul Habari zilizoufikia mtandao huu jioni hii zinaeleza kuwa mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki wa dansi nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ amefariki dunia nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar. Kwa mujibu wa wanamuziki waliofanya naye kazi kwa muda mrefu, Kasongo ambaye alifanya kazi na bendi nyingi kama Maquis du Ziare akiwika na Nyimbo za Angelo, Mwana Malole, Nasononeka, Baharia, Siri ya Mkoko na zingine kibao amefariki dunia baada ya kuumwa kwa muda mrefu akisumbuliwa na Kisukari hivyo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake. Katika siku za mwishoni, Kasongo aliitumikia Bendi ya Bakulutu kabla ya kujiunga katika Bendi ya Bana Maquis ikiwa chini ya Tshimanga Kalala Asssosa.

BREAKING NEWS : KESI ILIYOKUWA INAMKABILI MWENYEKITI WA CUF IBRAHIM LIPUMBA YAFUTWA RASMI

Image
Professor  Ibrahim Lipumba  alikuwa na kesi pamoja na wafuasi 30 wa CUF katika Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya kufanya mkusanyiko bila ya kuwa na kibali cha Polisi. Picha ya January 2015  Prof. Lipumba  akiwa Mahakamani Kesi hiyo ilianza kusikilizwa toka January 2015, ninayo ripoti kutoka kwenye taarifa ya habari ya ITV kwamba  Prof. Lipumba  na watu wote 30 wamefutiwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili Mahakamani hapo.

WOLPER AKIVISHWA PETE TU KWISHA HABARI YAKE!

Image
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper. KUMBE! Waliosema ujana maji ya moto hawakukosea kwani una changamoto nyingi hasa pale unapofikia wakati wa kumtafuta wa kuwa naye maishani yaani mke au mume. Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anaweza kuthibitisha hilo baada ya uchunguzi kuonesha kuwa ana listi ya wanaume waliomvisha pete za uchumba kisha wakapata walichokitaka, wakaingia mitini. Uchunguzi huo ulibaini kwamba, wanaume wengi wamekuwa wakitumia gia hiyo kumrubuni na kumwachia maumivu makali ya moyo. Katika makala haya tunakuletea listi ya wanaume ambao waliwahi kuwa na Wolper na kumvisha pete za uchumba na wengine kujitambulisha au kumtambulisha kabisa kwa wazazi lakini baada ya kumfaidi wakammwaga na kujikuta akihamia kwa mwingine, jambo ambalo watu wengine ambao ni mashabiki wake wamekuwa wakihoji ana nini mpaka yamkute hayo? ABDALLAH MTORO ‘DALLAS’ Mfanyabiashara huyo aliyekuwa na fedha ‘chafu’ alianzisha uhusiano na Wolper ambapo alimvisha pete ya u

SHAMSA FORD AMFUNGUKIA NAY WA MITEGO NA KUMWAMBIA MANENO HAYA MAZITO

Image
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford. KARIBUNI wasomaji wetu wa kolamu hii ambayo tumekuwa tukiwaletea wasanii mbalimbali na kufunguka mambo ambayo yamekuwa yakikutatiza, kwanza napenda kuomba radhi kwa kutomleta mwanadada, Riyama Ally kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Leo hii tunaye staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford ambaye amefunguka mambo mengi ya kisanaa na kimaisha.   Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Msomaji: Habari dada Shamsa kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri lakini ningependa kujua pale unapokumbwa na skendo huwa unajisikiaje au umeshazoea hayo mambo? Shamsa: Nikiwa kama mzazi huwa najisikia vibaya na bora skendo yenyewe iwe ya kweli ikiwa ya kusingiziwa huwa naumia zaidi. Msomaji: Eti dada nilisikia unatoka na msanii Emmanuel Elibarik ‘Nay wa Mitengo ‘ mliishia vipi au bado mnaendelea kimyakimya? Shamsa: Masuala ya Nay tumeshamalizana, kila mtu yupo bize na maisha yake. Msomaji: Hivi dada maisha yako yapoje baada ya kuachana na baba watoto wako (Dickson) huoni ka

Gari la Wema mikononi mwa Rais Magufuli

Image
Hali ni tete! Chanzo kimoja kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kimenyetisha kwamba, kasi ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ kuhakikisha hakuna Mtanzania anayekwepa kodi imepamba moto na sasa, imetua kwa mastaa wa Bongo ambapo kuna madai lile gari la kifahari la Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu (pichani) aina ya Range Rover Evogue linachunguzuwa na TRA, Amani limenyetishiwa. SI YEYE TU Kwa mujibu wa chanzo hicho, mbali na Wema, mastaa wengine ambao nao magari yao yako kwenye orodha ya kuchunguzwa mwenendo wa kodi ni Jacqueline Wolper Massawe (Toyota Prado), Kajala Masanja (Toyota Hilux) na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ (BMW X6). MAELEZO YAKO HIVI “Unajua serikali imedhamiria kukusanya kodi. Anachotaka Rais Magufuli ni kila mtu mwenye haki ya kulipa kodi ya kitu fulani, afanye hivyo bila kukwepa. Na hakuna kumuonea mtu. “Sasa bwana…bwana! Huko makao makuu (TRA) hakukaliki, huyo Kaimu Kamishna Mkuu, Phillip Mpango ni mkali balaa, anadhani Magufuli atamzukia wakat

CHADEMA NAO WATOA MAONI YAO UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI.

Image
Wakati Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli akionekana kuteka hisia za Watanzania wengi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakishtushwi kwani amekuwa akitumia hoja, mikakati na Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho. Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, alisema kuwa wakati wa kampeni Chadema ilieleza jinsi ya kupambana na ufisadi, kuwa na utaratibu bora wa utendaji kazi, uadilifu na uzembe wa watumishi wa umma, mambo ambayo sasa yanafanywa na Dk Magufuli. Hata hivyo, alisema kwa kuwa anachofanya hakikuwamo katika mipango ya Chama cha Mapinduzi (CCM), anaamini atakumbana na changamoto siku zijazo. “Akiomba ushauri tutatoa kwa maana namna gani atekeleze, lakini ni mapema mno kusema kama ana dhamira ya kuyafanya. Pengine anayafanya kwa ajili ya kujitafutia umaarufu wa harakaharaka,” alisema Mwalimu. Mikakati ya Dk MagufulTangu Novemba 5 mpaka sasa, Dk Magufuli ametangaza mikakati kadhaa ya kubana matumizi ya Serikali, ili

Rais Dkt.Magufuli akutana na viongozi na wawakilishi wa umoja wa sekta Binafsi nchini

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015. PICHA NA IKULU

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AGEUKWA NA WAPAMBE WALIOMSHAWISHI AGOMBEE URAIS

Image
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema baadhi ya wapambe na vigogo waliompigia debe na kumshawishi Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, achukue fomu kuwania urais kwa mara ya kwanza mwaka 2010, hivi sasa wamemgeuka na baadhi yao wanamuona kikwazo kutokana na msimamo wake wa kimapinduzi usioyumba, wala kuogopa vitisho katika kuweka maslahi ya umma mbele. Akizungumza wakati alipokutana na makundi ya vijana wa CCM kutoka majimbo manne visiwani hapa jana ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa marudio Zanzibar, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema watu hao walitarajia Dk. Shein baada ya kuwa Rais angekuwa dhaifu, mwepesi na angekubali kutii na kushiriki usaliti dhidi ya uhuru na mapinduzi kwa manufaa ya wachache, lakini imeshindikana kutokana na Rais huyo kuweka mbele maslahi mapana ya Zanzibar na wananchi wake. "Madalali hao wa kisiasa hawakujua wala kufahamu kama Dk. Shein ni zao la mapinduzi. Laiti kama Dk. Shein asingelelewa, kuandaliwa n

Aunt amfundisha ulevi Moze

Image
Staawa Bongo Movie, Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moses Iyobo ‘Moze’. STAA wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel juzi kati baada ya kujitwika kilaji a.k.a masanga vilivyo, alijikuta akijigamba waziwazi kumfundisha ulevi mzazi mwenzake, Moses Iyobo ‘Moze’. Akichonga na kona ya Bongo Movie kwa sauti ya kilevi, Aunt alikiri kuwa mnywaji mzuri wa pombe hivyo kwenye maisha yake hategemei kukaa na mume zaidi ya miaka miwili halafu ashindwe kumshawishi kunywa naye pombe kwani huo utakuwa ni uzembe wa hali ya juu. “Nimejitahidi sana kumuwezesha Moze wangu kuanza alau kugusa kinywaji kilaini maana zamani kila nikimpatia pombe lazima akasirike. Nafurahi kuona sasa ameanza kuonjaonja hadi inafikia hatua anamaliza hadi chupa tatu,” alisema Aunt. Kwa upande wa Mose Iyobo alisema kwa sasa anakunywa bia tatu tu! 

MHE. BALOZI SEFUE AENDELEA KUWASISITIZA WATUMISHI WA UMMA KUVAA BEJI ZINAZOWATAMBULISHA MAJINA YAO WANAPOKUWA KATIKA MAENEO YA KAZI

Image
Katibu Mkuu Kiongozi  Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) beji yenye jina lake ambayo amewaagiza watumishi wa Umma kuivaa wanapokuwa  katika maeneo  yao ya  kazi. Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank . Na Anna Nkinda – Maelezo Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa  katika maeneo  ya  kazi. Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine. Alisema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza  watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao. “Nimeamua kuonyesha mfano kwa vitendo

Mwanamikakati wa Lowassa Ahusishwa na Wizi Mkubwa Stanbic

Image
 Bw. Bashir Awale Kulia Mwenye Tshirt ya Njano Akisalimiana na Lowassa Siku chache baada ya uchaguzi serikali ya Tanzania ilimfukuza mtu aliyejulikana alikuwa mashauri wa Kimkakati wa Mgombea Urais kupitia Chadema, Bw. Bashir Awale (Mkenya ashikiliwa na Polisi nchini TZee kwa kumpigia debe Lowassa kipindi cha campaigns), kwa kuishi kimakosa nchini. Pia, ilijulikana kuwa kabla ya kuanza kujihusisha na siasa, hasa kuwa mshauri wa Ndugu Lowassa katika kuusaka urais alikuwa mmoja wa Maofisa Wandamizi wa Benki ya Stanbic. Katika sakata linalohushisha benki ya Stanbic kufanya udanganyifu mkubwa wa kujipatia fedha na kushitakiwa na Idara ya Makosa ya Uingeleza huyu jamaa katokea. Na imeonyesha alifukuzwa katika wakati huu baada ya kufanya wizi huu kwa kushirikiana na ndugu wa karibu wa Lowassa na aliyekuwa Miss Tanzania 1996, Shose Sinare. Kwa mjibu wa serikali, tayari uchunguzi umeanza kufanyika ili kubaini aliyefaidika na pesa hizo. Aidha, hukumu iliyofanyika jana imeamuru serikal

BREAKING NEWZZZZZ!!!! DR.SLAAA ATOA KAULI HII NZITO MDA HUU KWA RAIS MAGUFULI

Image
 Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini. Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli. “Nadhani sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za mwanzo inahitaji udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka, nimefurahi sana,” Dk. Slaa ameliabia gazeti la Raia Mwema. Amesema kuwa Bunge linatakiwa kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo ili usivuke mipaka lakini limuunge mkono kwa hatua anazochukua. Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amemshauri Rais Magufuli kuiangalia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuifumua. “Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.

Bi harusi amuua bwana harusi kwa kisu

Image
Marehemu Geofrey enzi za uhai wake. Na Makongoro Oging’ MADAI MAZITO!   Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, Dar limesema linamshikilia mwanadada Rhoda Daudi kwa tuhuma ya kumuua kwa kumchoma kisu, Geofrey Valeli Kapulula (37) aliyetarajia kufunga naye ndoa hivi karibuni, Uwazi lina mkasa wote. Tukio hilo la kutisha na ambalo limeacha maswali, lilijiri maeneo ya Ubungo National Housing (NHC) jijini Dar es Salaam, Novemba 23, mwaka huu. Bi harusi anayetuhumiwa kwa kosa la kumchoma kisu   Geofrey. UWAZI ENEO LA TUKIO Mwandishi wa habari hii, alifika katika eneo la tukio na kuzungumza na majirani ambao walisema kwamba siku ya tukio walisikia sauti ya marehemu akiomba msaada lakini hata hivyo, hawakujali kutokana na kuzoea wawili hao kugombana mara kwa mara na kisha kupatana. Mmoja wa majirani hao ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini, alisema siku ya tukio, wapendana hao walikuwa wakinywa kwenye baa moja na marafiki zao huku wakibadilishana mawazo lakini kukatokea

Basi lagongana na lori na kuua watu Singida

Image
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba watu kadhaa wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyotokea baada ya basi la abiria la Takbir lenye namba za usajili T 230 BRJ lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na lori eneo la Shelui mkoani Singida usiku huu.

MISS TANZANIA USA 2015-2016 AEESHA KAMARA ASHINDA KUWA COVER GIRL KWENYE CALENDA YA MISS AFRICA USA 2015-2016

Image
 Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara (kushoto) akiibuka mshindi na kuwa Cover Girl kwenye Kalenda ya Miss Africa USA 2015-2016 shindano ililofanyika New York siku ya Jumamosi Novemba 28, 2015.  Mamiss wengine walioshiriki shindano hilo wakipita mbele ya majaji.  Wadau wakipata picha na mamiss wakati mratibu wa mashindano ya miss Africa Lady Kate alipokua akitangaza shindi. Ma Winny Casey (gauni jeusi) pamoja na Lady Kate (mwenye miwani) wakiwa na mamiss.

Dereva achinjwa kikatili

Image
Salum Masoud enzi za uhai wake. Na Boniphace Ngumije INASIKITISHA! Salum Masoud (35), mkazi wa Kijichi, Rufiji mkoani Pwani ambaye alikuwa dereva wa magari ya kubeba mizigo mkoani humo ameuawa kikatili kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana na ifuatayo ni simulizi ya kusikitisha kutoka kwa dada wa marehemu aitwaye Hawa Masoud, mkazi wa Mbagala, Dar. Akifuta machozi na kuzungumza kwa kwikwi na gazeti hili hivi karibuni, Hawa alisema mazingira ya tukio la kuchinjwa kwa ndugu yake yamejaa utata. “Taarifa za kuuawa kwa kaka yetu zilitufikia Novemba 10, mwaka huu baada ya watu wasiojulikana kumpigia simu dada wa mke wa marehemu na kumtaarifu. “Binafsi nilishtushwa sana. Ilikuwa vigumu kuamini. Lakini hatukuwa na budi kukubaliana na hali halisi, tukaamua kukusanyana na kwenda eneo la tukio kufahamu nini kilitokea mpaka Salum akauawa kikatili namna hiyo. “Tulipofika tulimkuta bosi wa marehemu aitwaye, Salum Bakari Mnolage akifanya taratibu za mazishi. Tulimkataza lakini akatuiti

MAGAZETI YA LEO JUMATANO ya trh 02/12/2015

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .