Mwanamikakati wa Lowassa Ahusishwa na Wizi Mkubwa Stanbic

 Bw. Bashir Awale Kulia Mwenye Tshirt ya Njano Akisalimiana na Lowassa
Siku chache baada ya uchaguzi serikali ya Tanzania ilimfukuza mtu aliyejulikana alikuwa mashauri wa Kimkakati wa Mgombea Urais kupitia Chadema, Bw. Bashir Awale (Mkenya ashikiliwa na Polisi nchini TZee kwa kumpigia debe Lowassa kipindi cha campaigns), kwa kuishi kimakosa nchini. Pia, ilijulikana kuwa kabla ya kuanza kujihusisha na siasa, hasa kuwa mshauri wa Ndugu Lowassa katika kuusaka urais alikuwa mmoja wa Maofisa Wandamizi wa Benki ya Stanbic.

Katika sakata linalohushisha benki ya Stanbic kufanya udanganyifu mkubwa wa kujipatia fedha na kushitakiwa na Idara ya Makosa ya Uingeleza huyu jamaa katokea. Na imeonyesha alifukuzwa katika wakati huu baada ya kufanya wizi huu kwa kushirikiana na ndugu wa karibu wa Lowassa na aliyekuwa Miss Tanzania 1996, Shose Sinare.

Kwa mjibu wa serikali, tayari uchunguzi umeanza kufanyika ili kubaini aliyefaidika na pesa hizo. Aidha, hukumu iliyofanyika jana imeamuru serikali ya Tanzania kulipya dola 6M na Stanbic kama sehemu ya hela iliyoibwa.

Sasa ni wakati wa kujiuliza:

Lowassa angeweza kusimamia masilahi ya taifa hili wakati katika wakati mwingi ameoneka ni mtu wa dili?

Tutaendelea kumwamini Lowassa na Chama alichonunua kwa mamilioni ya fedha bila kulipia kodi ya serikali?

2020 inakuja, atajitokeza tena kama ameanza kuumbuka mwezi wa kwanza wa JPM?
TUPE MAONI YAKO MDAU WETU

Comments

Popular posts from this blog