Posts

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 13.11.2015

Image
Julius Kambarage Nyerer

MBASHA LIVE NA KIFAA

Image
Richard Bukos CHA KUFIA! Msanii wa muziki wa Injili Bongo, Emmanuel Mbasha, Alhamisi iliyopita alinaswa kwenye maongezi yaliyoambatana na pozi lenye maswali kwa kuonekana akichukua namba fastafasta kwa mrembo ‘kifaa’. Wakifurahia jambo. Mbasha alinaswa na kifaa hicho ndani ya Viwanja vya Ikulu jijini Dar ambapo kulikuwa na hafla ya kumpongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo. Katika tukio hilo, wawili hao walikuwa kwenye kona wakitafuna vipapatio vya kuku na kubadilishana mawazo huku kila mmoja akimuonesha mwenzake tabasamu la amani na upendo.‘Wapiga chabo’ waliowaona walifika mbali zaidi kwa kusema eti, Mbasha akiishi na kifaa hicho watapendezana kwani anafanana na mkewe waliyetengana, Flora. Akizungumza na Amani kuhusu mdada huyo, Mbasha alisema ni shabiki wa kazi zake na hana mpango wa kuziba nafasi ya Flora.

SHAMSA: BORA NIFE KULIKO KURUDIANA NA MUME WANGU

Image
Imelda Mtema MAKUBWA!! Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford ameibuka na kukataa katakata kurudiana na aliyekuwa mumewe, Dickson Matoke ‘Dick’ akisema kuwa kama watarudiana basi atakuwa ameshafariki dunia au bora afe kuliko kurudiana naye. Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford. Shamsa aliyasema hayo juzikati baada ya kuulizwa na Amani kama ana mpango wa kurudiana na mumewe huyo ambapo alisema licha ya kuzaa mtoto mmoja (Terry) na mwanaume huyo, lakini katika maisha yake hafikirii kamwe kurudiana naye huku akasisitiza kuwa, kwa sasa ana maisha yake mengine. “Mimi nirudiane na Dick? Labda niwe nimekufa na ni bora nife kuliko kurudiana na Dick. Ujue sasa hivi nina thamani kubwa zaidi na nipo na mtu ambaye ananipenda, nampenda,” alisema Shamsa.Hivi karibuni, Dick aliripotiwa na gazeti moja la Global akisema bado anampenda sana Shamsha na yuko tayari kurudiana naye baada ya kumwagana.

KIMENUKA CHADEMA: MBOWE APEWA SIKU TATU KUTENGUA UTEUZI WA MBUNGE WA VITI MAALUM

Image
BAWACHA Mkoani Ruvuma wampa Mwenyekiti Mbowe siku tatu kutengua uamuzi wa kumteua Zubeda Sakuru Ubunge Viti Maalum, wasikitishwa na uteuzi huo wadai ni wa upendeleo -Aidha wameshangazwa na uongozi wa Chama kutotokea kwenye kikao maalum cha kupinga uamuzi huo.Wamesema wamesikitishwa kwa chama kuonyesha waziwazi kwamba ni mali ya mtu mmoja na familia yake. Iweje leo waletewe Mbunge wa Viti Maalum kutoka Tanga, hali hajui Mkoa wa Ruvuma ukoje na Jiografia yake. Aidha pia wameshangazwa na uongozi wa Chama hiko kutotokea kwenye kikao maalum cha kupinga uamuzi huo BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

UKAWA KIMENUKA:..JAMES MBATIA AKIONA CHA MOTO MWANZA HAPATOSHI

Image
Viongozi wa chama cha NCCR - MAGEUZI Mwanza inasemekana wamejiuzuli uongozi ndani ya chama chao kwa madai ya M/kiti wa chama hicho James Mbatia kukidhohofisha chama kilichokuwa na wabunge wanne na sasa kina mbunge mmoja. Waliojiuzulu inasemekana ni Kamishina wa mkoa Ramadhan Amran, M/kiti wa jimbo la Nyamagana na Ilemela na Kiongozi wa vijana Nicolas Clinton.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISITAREHE 12.11. 2015

Image

UNYAMA Dar! Mke wa Mtu Atembezwa MTUPU, Apigwa Mawe na Kuchomwa Moto!

Image
Kundi la vijana hao wakimtembeza Shakila mitaani huku akiwa mtupu. Na Makongoro Oging’ DUNIA katili! Mrembo mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shakila Kocho (21), mkazi wa Tabata- Kimanga jijini Dar amelazwa Wadi namba 24, Jengo la Mwaisela, Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia majeraha yaliyotokana na kupigwa mawe na kuchomwa moto wa petroli kwa kisa cha tuhuma za kuwa kwenye mtandao wa wizi wa bodaboda. Wakimshambulia kwa mawe. WALIOTEKELEZA UKATILI Msichana huyo alifanyiwa kitendo hicho hivi karibuni maeneo ya Buguruni Sukita, Dar na watu wanaodaiwa kuwa ni madereva wa bodaboda ambao ndiyo waliomtuhumu. Taarifa zilizopatikana kwa mashuhuda zinadai kwamba, Shakila kabla ya kuchomwa moto alitembezwa mtupu mtaani huku watu wakimsonga na baadaye akapigwa mawe na fimbo halafu akamiminiwa petroli na kulipuliwa kwa kiberiti. Shakila akiwa ameanguka. MSOMALI ASAIDIA Kwa mujibu wa mashuhuda hao, wakati Shakila akiwa chini kutetea roho yake huku akiungua moto, mwanaum

SITTA:NINA SIFA ZOTE KUONGOZA BUNGE LIJALO

Image
Dar es Salaam. Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Samuel Sitta amesema kutokana na hali ya joto la kisiasa ilivyo, ambayo ilidhihirika zaidi wakati wa uchaguzi, wabunge walioshinda wengi ni vijana na ni wazi spika anayehitajika ni mwenye uzoefu. Sitta ameyasema hayo leo wakati akihojiwa na Radio Uhuru FM, ambako amethibisisha kwamba naye anakusudia kugombea nafasi hiyo ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa anaamini anazo sifa zote zinazohitajika.

TAARIFA KUTOKA JIMBO LA LUDEWA MAPYA KUHUSU MRIDHI WA DEO FILIKUNJOMBE

Image
Makada 10 wa CCM waliochukua na kurejesha fomu wanatarajiwa kupigiwa kura na wanachama wa CCM ili kumpata mgombea atakayepambana na wagombea wa vyama vya upinzani. By Joyce Joliga, Mwananchi Ludewa. Wanachama wa CCM katika Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, leo wanapiga kura za maoni ili kumpata mgombea ubunge kupitia chama hicho atakayeziba pengo lililoachwa na Deo Filikunjombe aliyefariki dunia Oktoba 15, mwaka huu. Makada 10 wa CCM waliochukua na kurejesha fomu wanatarajiwa kupigiwa kura na wanachama wa CCM ili kumpata mgombea atakayepambana na wagombea wa vyama vya upinzani. Makada hao ni Philip Filikunjombe (mdogo wa Deo Filikunjombe), Edgar Lugome, Johnson Mgimba, Emmanuel Mgaya, James Mgaya, Jackob Mpangala, Simon Ngatunga, Evaristo Mtitu, Deo Ngalawa na Zephania Chaula. Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Ludewa mjini, Tafuteni Mwasonya alisema kuwa tayari Mungu ame

WAZIRI MKUU MPYA WA SERIKALI YA WAMU YA TANO NI HUYU

Image
Fumbo kuhusiana na mtu mwenye sifa za kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli limeanza kufumbuliwa. Hali hiyo inatokana na kile alichokidhihirisha Magufuli siku moja baada ya kuapishwa kwake na pia baada ya hapo wakati alipochukua maamuzi kadhaa ya vitendo, ikiwamo kutoa maelekezo muhimu yaliyodhihirisha aina ya Waziri Mkuu atakayemteua. Kwa mujibu wa muundo wa serikali, Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, ambaye mbali ya kuwa kinara wa mawaziri wengine, ndiye anayetakiwa pia kutoa maamuzi mazito linapojitokeza jambo linalomlazimu kufanya hivyo. Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya siasa na uongozi nchini wamesema hatua alizochukua Magufuli kuanzia siku ya kwanza ya kuapishwa kwake zinatoa picha ya wazi aina ya watu atakaotaka kuwa nao katika serikali yake. Baada ya kuapishwa Novemba 5, 2015, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Dk. Magufuli alianza kazi siku hiyo hiyo kwa kuto

Maagizo 11 ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa Wizara ya Afya, Ikiwemo ya Maduka ya Dawa Binafsi Yaliyoko Maeneo ya Hospitali za Serekali Kuondolewa

Image

MAGAZETI YALEO JUMANNE.

Image

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA ASHIRIKI HAFLA YA DUA YA KUOMBEA TAIFA AMANI, JIJINI DAR

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape Television Network (ATN) Dkt. Anny Fernandes, wakati wa  hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape Television Network (ATN) Dkt. Anny Fernandes, wakati wa  hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR Mkuu wa Mkoa wa Dar

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA ASHIRIKI HAFLA YA DUA YA KUOMBEA TAIFA AMANI, JIJINI DAR

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape Television Network (ATN) Dkt. Anny Fernandes, wakati wa  hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape Television Network (ATN) Dkt. Anny Fernandes, wakati wa  hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR Mkuu wa Mkoa wa Dar