CCM YATANGAZA RASMI KIKOSI CHAKE CHA KAMPENI 2015 JIJINI DAR LEO
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kuhusiana na uteuzi wa kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015,ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Wajumbe Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto. Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto). Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi