Posts

BREAKING NEWS: PROF. KITILO AKATAA KUGOMBEA URAISI ACT, BARUA YAKE HII HAPA

Image
Ndugu Wazalendo, Naomba niwashukuru nyote kwa imani kubwa mliyo nayo juu yangu katika kukiwakilisha chama katika nafasi ya Rais. Naishukuru pia Kamati Kuu kwa imani yake kwangu hata kufikia hatua ya kupitisha azimio la kuniomba nigombee urais kwa chama chetu. Jana Kamati Kuu ilituma ujumbe maalumu nyumbani kwangu kwa ajili ya kuzungumza na familia na jamaa zangu juu ya ombi hili. Aidha, Nimekuwa nikilitafakari jambo hili tangu Alhamisi nilipoombwa rasmi kutafakari uwezekano wa mimi kugombea baada ya juhudi zetu za kutafuta mgombea kushindikana. Nimefanya mawasiliano mapana katika familia, ndani ya chama, chuoni ninapofanyia kazi, Kanisani kwangu,na kwa watu na taasisi mbalimbali ninazohusiana nazo. Baada ya tafakari na mawasiliano  CONSULTATIONS  mapana nasikitika kusema kwamba sina utayari na maandalizi ya maana ya kisaikolojia, kifamilia, na kisiasa kuniwezesha kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi huu. Najua nimewaangusha sana katika uamuzi ...

HIVI NDIVYO MABASI YA MWENDO KASI YALIVYO ZINDULIWA JIJINI DAR

Image
Moja ya mabasi yaendayo mwendo wa haraka yakiwa barabarani katikati ya jijini Dar es Salaam leo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki akizungumza katika uzinduzi wa semina ya mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini Dar es salaam, juu ya kuanza kwa kipindi cha mpito cha mradi huo Oktoba mwaka huu, Semina itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi Hawa Ghasia akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) waliokaa mbele, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki na kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi. Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi Hawa Ghasia aliyeshika mkasi akikata utepe kuzindua mafunzo madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mafunzo yayo ya madereva. Baadhi ya viongozi wa jesh...

RAIS KIKWETE AMPA MAKAVU LOWASSA

Image
  Wakati wa sherehe ya kumuaga Rais Kikwete iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi, Rais kikwete alimpa somo Lowasa kwa kueleza kuwa mtu akiwa Waziri hapaswi kujisifia kuwa amelifanya jambo Fulani yeye binafsi katika nchi wakati Waziri hufanya kazi kwa niaba ya Rais. Alitolea mfano huo alipokuwa anamsifia Waziri Pombe Magufuli ambaye pamoja na kazi nzuri ya ujenzi wa Barabara lakini wakati wote amekuwa hajisifii kuwa anafanya yeye binafsi. Uchunguzi unaonesha kuwa Rais alikuwa anampa somo hilo Lowasa ambaye anajitapa kuwa alijenga UDOM wakati wazo hilo ni la JK mwenyewe binafsi wala halikuwa ktk ILANI YA CCM

NAPE ATAKA GARI LA WAGONJWA LIPELEKWE KWA LOWASSA MAPEMA

Image
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza kuwa kitashinda Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwa sababu kina mtandao mkubwa wa wanachama kuanzia ngazi ya chini na kwamba kufurika kwa wananchi katika mikutano ya Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa sio ushindi, kikisema kura ni mahesabu. Aidha, kimesema kuwa mgombea huyo wa Chadema na umoja wa vyama vinne vya upinzani (Ukawa), amedanganywa na wapambe wake kuihama CCM na kumkejeli ikisema gari la wagonjwa linapaswa kuwekwa nyumbani kwake siku ya uchaguzi kwani CCM itapata ushindi wa uhakika asubuhi. Akitoa taarifa kuhusu kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisisitiza kuwa ushindi wa chama hicho tawala na kikongwe hauna shaka kutokana na mtandao wake kuanzia ngazi ya chini. Akijibu swali kuhusu kufurika kwa wananchi katika mikutano ya mgombea huyo wa Chadema, Nape alisema:  “Kwa walioanz...

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 18.08.2015

Image

IRENE UWOYA HATARINI KUPOTEZA UBUNGE VITI MAALUM

Image
Muigizaji wa bongo movies Irene Uwoya aliyejiunga na ccm na kuchaguliwa kuwa mbunge wa viti maalum tabora yupo hatarini kupoteza cheo chake cha ubunge wa viti maalum na huenda wabunge viti maalum wengi sana wa ccm nao wataachia ngazi. Mbunge viti maalum aliechaguliwa kwa sasa ataingia mjengoni mpaka ifikapo oktoba baad ya kampeni na uchaguzi ambapo kila jimbo litapata mbunge(sio wa viti maalum) wake ambapo hawa wabunge wa viti maalum waliochaguliwa saizi italazimu idadi yao ilingane sawa na idadi ya wabunge wawakilishi wa majimbo wa vyama vyao, mfano kwa ccm mwaka 2010 kabla ya kampeni walikuwa na wabunge viti maalum 92 ila baada ya kampeni na uchaguzi ilipata wabunge 60, kutokana na kupoteza majimbo mengi hivyo ikabidi idadi ya wabunge wa ccm wa viti maalum ipungue toka 92 hadi 60, na wakati wao ccm waliandaa wabunge 92 wa viti maalum wakijua watapata majimbo mengi , matokeo yake ikabidi chama kiwapunguze hadi 60 na baada ya hapo nafas zilizobsaki 22 za wabunge viti...

PICHA ZA SIMBA WAKIIDUNDA 2-0 URA

Image
Mshambuliaji Kelvin Ndayisenga akishangilia baada ya kuifungia Simba goli la kwanza Timu ya Simba SC jana ilishinda 2-0 katika mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya URA FC ya Uganda,  mechi ikipigwa uwanja wa Taifa, Dar e salaam Hapa nimekuwekea picha zikionesha matukio mbalimbali wakati mcheo huo ulivyokuwa ukiendelea. Kelvin Ndayisenga (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia timu yake goli la kwanza Watoto wazuri nao walikuwepo wakishuhudia mtanange kati ya Simba na URA FC Juuko Murshid (kulia) akishangilia pamoja na Ibrahim Ajibu baada ya kuifungia timu yake goli la pili Kikosi cha URA kilichoanza dhid ya Simba SC Kikosi cha timu ya Simba SC kilichoanza kwenye mchezo dhidi ya URA Wachezaji wa Simba kabla ya kushuka kwenye gari Basi la Simba likiwasili uwanja wa Taifa

EXCLUSIVEEEE FLAVIAN MATATA WEDDING PHOTOS

Image

KAULI YA LOWASSA BAADA YA MSAFARA WAKE KUPIGWA MABOMU NA POLISI, SOMA HAPA ALICHOSEMA

Image
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa jana kwa mara ya kwanza alikumbana na joto la upinzani baada ya msafara wake kushambuliwa na mabomu ya polisi. Tukio hilo, ambalo lilifanyika mbele ya msafara wa Lowassa, lilitokea jana eneo la Daraja la Nduruma katika Jiji la Arusha na kusababisha umati wa watu kutawanyika na wengine kutelekeza magari yao.Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimkaribisha kwenye chama hicho wakati wa mkutano mkuu alimwambia; “Mzee huku inabidi uwe unafanya mazoezi kidogo, kuna mabomu huku.”Lowassa alikumbwa na kadhia hiyo, akiwa njiani na mgombea mwenza, Juma Duni Haji na viongozi wengine wa Ukawa, wakitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), huku wakiwa wamesindikizwa na umati wa watu na magari. Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema kuwa polisi walilazimika kupiga mabomu ya machozi ili kutawanya watu waliokuwa wakiwarushia mawe polisi na wengine kufunga barabara. “Kwa hali ile...

MGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA NA UKAWA EDWARD LOWASA ALIPOWASILI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA KILIMANJARO KIA

Image
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Philemoni Ndesamburo akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi ,Godluck Ole Medeye walipokutana uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)kwa ajili ya mapokezi ya mgombea urais wa UKAWA na Chadema,Edward Ngoyai ,Lowasa. Mwenyekii wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro akisalimiana na James Lembeli walipokutana uwanja wa Ndege wa KIA. Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasni akizungumza jambo na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Godluk Ole Medeye. Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi,Godluck Ole Medeye akiteta jambo na Henry Kilewo mtia nia waubunge jimbo la Mwanga. Aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Laurance Masha akisalimiana na Katibu wa Chadema kanda ya Kasakazini,Aman Golugwa. Masha akisalimana na Mbunge wa jimbo la Arusha mjini ,Godbless Lema, Mzee Ndesamburo akiwaongoza makada wengine wa chama hicho kwa ajili ya mapokezi ya mgombea ...