JOYCE KIRIA:- NILIAMUA KUOLEWA BAADA YA KUKOSA KODI YA NYUMBA, SOMA HAPA
Ijumaa: Wewe ni mwanaharakati ambaye muda mwingi unakuwa mbali na familia yako, vipi malezi ya watoto? Joyce: Wanalelewa na dada ambaye huwafanyia kila kitu. Ijumaa: Historia yako inaonesha uliwahi kuwa ‘house girl’, je ulishawahi kukutana na ishu ya kubakwa? Joyce: Namshukuru Mungu nilikutana na mitihani mingi lakini sikuwahi kubakwa, ila katika kazi yangu nimekuwa nikikutana na wadada wengi waliofanyiwa hivyo na kuwasaidia. Ijumaa: Mume wako amepita kwenye kura za maoni na kuelekea kwenye ubunge, unalizungumziaje hilo? Joyce: Nimefurahi sana, namuombea kila la heri avuke katika hatua inayofuata. Ijumaa: Hivi ni kwa nini uliachika kwenye ndoa ya mwanzo? Joyce: Niliachika kwa sababu sikuwa nimempenda mwanaume niliyekuwa naye bali niliingia kwenye ndoa kwa sababu ya kitu na hili ni fundisho kwa wanawake. Ijumaa: Ina maana wewe uliolewa na mwanaume wa kwanza kwa sababu ya pesa zake? Joyce: Kiukweli nisiwe mnafiki nakumbuka mwanaume wangu wa kwanza alinioa