Posts

VIUNGO VYA BINADAMU VYAKAMATWA HUKO SIMIYU

Image
WAKAZI wawili wa Kijiji cha Bukigi kilichopo Kata ya Malampaka mkoani Simiyu, wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kupatikana na viungo vya binadamu. Waliofikishwa juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Maswa mbele wa Hakimu Tumaini Marwa, ni Matheyo Yumbu (50) na Juma Mihangwa (28). Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Nassibu Swedy kuwa Mei 5, mwaka huu, saa 11 alfajiri katika Kijiji cha Bukigi, washitakiwa hao walikutwa wakiwa na viungo hivyo. Alidai viungo walivyokutwa navyo washitakiwa hao ni fuvu la kichwa, mifupa ya miguu na mikono ya binadamu wakiwa wamevihifadhi katika mfuko wa sandarusi katika nyumba waliyoishi. Hata hivyo, washtakiwa hao walikana kosa hilo na kunyimwa dhamana na walipelekwa mahabusu hadi hapo kesi itakapotajwa tena Mei 29, mwaka huu na upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

ASIMAMISHWA KAZI BAADA YA KUMTUMIA MESEJI RAIS JAKAYA KIKWETE

Image
Mhasibu wa Hospitali ya Rufaa KCMC,  Paul Mhumba  amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kutuma ujumbe wa simu ya mkononi (sms) kwa Rais  Jakaya Kikwete. Kuvuja kwa ujumbe huo na nambari ya simu iliyotuma, kumeibua hisia tofauti kuhusu usiri wa ofisi ya Rais katika kushughulikia malalamiko nyeti ya wananchi na kuwaweka njiapanda watoa habari za siri. Mhumba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu  (TUGHE)  Tawi la KCMC anadaiwa  na Menejimenti ya KCMC kuwa ndiye aliyetuma ujumbe huo. Katika barua yake ya Mei 5, ilidai uchunguzi umebaini kuwa Mhumba ndiye mtumaji wa ujumbe huo. “Uongozi umepokea taarifa iliyotumwa mwishoni mwa Aprili na mwanzoni mwa Mei mwaka huu kwa njia ya ujumbe wa simu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete,”  . KCMC imedai katika barua hiyo, taarifa hiyo ya sms ilibeba ujumbe unaohusiana na matumizi mabaya ya fedha za hospitali hiyo unaofanywa na baadhi ya viongozi na Shirika la Msamaria M

JE, WAMJUA DADA YAKE NA DAIMOND?

Image
 

MADENTI MSINGI WAJIUZA SH.2000 HUKO MOROGORO!

Image
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Farao! Kumekuwa na madai ya baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi mjini hapa kujiuza kwa waendesha bodaboda kwa gharama ya shilingi elfu mbili tu. Mwanafunzi anayedaiwa kujiuza kwa waendesha Bodaboda. Kufuatia madai hayo, mwandishi wa kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ mjini hapa alifanyia kazi madai hayo na kufanikiwa kumnasa Ally Shabani (34) ambaye ni dereva wa bodaboda akiwa na mwanafunzi wa darasa la nne, Shule ya Msingi ya Kiwanja cha Ndege mkoani hapa (jina tunalo).Tukio hilo la kushangaza na kusikitisha pia, lilijiri Jumamosi iliyopita saa 7 mchana katikati ya mashamba ya mkonge yaliyopo Kihonda Kwachambo ambayo yanamilikiwa na Jeshi la Magereza jirani kabisa la Gereza la Kihonda MAMA MZAZI AISAKA OFM Awali, mama mzazi wa denti huyo, Mariam Jongo alimtafuta Kamanda wa OFM Mkoa wa Morogoro na kumweleza kuhusu tabia ya bodaboda huyo na mwanaye, alisema: ”Naomba msaada wako baba, kuna dereva wa bodaboda nimempa tenda ya kumpeleka m

MASOGANGE ACHAFUA HALI YA HEWA TENA

Image
   

AUNTY EZEKEI IMENIFANYA NISIENDE LONDON MOSE IYOBO AFUNGUKA!

Image
    Imelda Mtema MPENZI wa staa maarufu wa filamu Bongo Aunt Ezekiel, Moses Iyobo ambaye pia ni dansa mahiri wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa hakwenda kwenye shoo iliyokuwa ikifanyika katika Jiji la London kutokana na hali ya mpenzi wake. Akichezesha taya na Centre Spread, Mose alisema kuwa alishindwa kujumuika na wenzake akihofia hali ya mpenzi wake hivyo alipenda kuwa naye karibu hadi kwenye hitimisho lake la kumpata mtoto wao. “Unajua nashindwa kwenda mbali sana kutokana na hali ya mpenzi wangu kwa kuwa nakuwa na wasiwasi sana hivyo hata London nimeshindwa kwenda kwani natamani kuona hatua kwa hatua ya bebi wangu hadi kumpata mtoto wetu,” alisema Mose.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS TAREHE 21.05.2015

Image
  MAGAZETI YA UDAKU LEO     MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

COUTINHO MCHEZAJI BORA WA MWAKA LIVERPOOL, BALOTELLI AAAH!

Image
Mbrazil Phillipe Coutinho amewapiga bao wenzake na kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Liverpool. Raia huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 22, ametwaa tuzo hiyo ambayo kura zake hupigwa na mashabiki. Pamoja na hivyo, Coutinho amebeba tuzo nyingine tatu zikiwemo za bao bora na aliyeoonyesha kiwango cha juu kwa mwaka mzima. Raheem Sterling ambaye anataka kuondoka Liverpool yeye amekuwa kinda bora wa mwaka. TUZO Player of the Year: Phillipe Coutinho  First Team Players' Player of the Year: Phillipe Coutinho Goal of the Year: Phillipe Coutinho  Performance of the Year: Philippe Coutinho  Young Player of the Year: Raheem Sterling  Ladies Players' Player of the Year: Fara Williams!  Bill Shankley Community Award: Chris Anders Supporters Club of the Year: OLSC London  Academy Players' Player of the Year: Joao Carlos 

TAIFA STARS YATOLEWA COSAFA KWA AIBU, YATWANGWA 2-0 NA MADAGASCAR

Image
Taifa Stars imefungwa mabao 2-0 na Madagascar na kutolewa katika michuano ya Cosafa. Stars imeonyesha kiwango cha chini na kupoteza mchezo huo. Maana yake, kwa kipigo hicho, Stars imecheza mechi mbili bila bao wala pointi baada ya kuwa imepoteza kwa mabao 1-0 dhidi ya Swaziland. Sasa Stars imebakiza mechi moja tu dhidi ya Lesotho ambayo itakuwa ni kama ya kirafiki tu.

WATEJA WA VODACOM KUPERUZI INTANETI BURE

Image
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akisisitiza jambo. Dar es Salaam, May 20, 2015: Zaidi ya watumiaji milioni 13 wa mtandao wa simu za mkononi kuanzia leo wataweza kuperuzi internet inayofikia MB100 kwa masaa mawili bure kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 2 asubuhi kutokana na ofa inayojulikana kama " Good Morning Tanzania" inayotolewa na Vodacom Tanzania. Promosheni hii imeanzishwa kutokana na kuonenakana kuwepo kwa mahitaji makubwa ya matumizi ya data katika kupata  taarifa kupitia mtandao wa intaneti. Vodacom Tanzania siku zote imekuwa mstari wa mbele kubuni huduma zinazoendana na matakwa ya wateja wake na kuwarahisishia maisha katika nyanja ya elimu, afya,… Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akisisitiza jambo. Dar es Salaam, May 20, 2015: Zaidi ya watumiaji milioni 13 wa mtandao wa simu za mkononi kuanzia leo wataweza

ABBAS MTEMVU AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MAENEO YALIYOHARIBIWA NA MVUA

Image
  Diwani wa Soko la Tazara Vetenary Zahoro Maganga akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu alipotembelea maeneo yaliyoharibiwa  na mvua akiongozana na  viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (TANROADS) jinsi maji yanavyotakiwa kufata mfereji huo ambao haupitishi maji kupeleka katika mfereji huo.  Abbas Mtemvu (kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (TANROADS) …   Diwani wa Soko la Tazara Vetenary Zahoro Maganga akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu alipotembelea maeneo yaliyoharibiwa  na mvua akiongozana na  viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (TANROADS) jinsi maji yanavyotakiwa kufata mfereji huo ambao haupitishi maji kupeleka katika mfereji huo.  Abbas Mtemvu (kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (TANROADS)  katika ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam (kushoto) ni Meneja wa Tanro