Posts

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI KATI YA BASI LA MAJINJAH NA TOYOTA HILUX MBEYA

Image
Gari aina ya Toyota Hilux ambayo imegongwa na Basi la Kampuni ya Majinja likiwa linatoka Mbeya kwenda Dar. (Picha na Fahari news)   Mtu mmoja amefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamenusurika kifo katika ajali ya barabarani iliyotokea majira ya saa 12:15 asubuhi njia panda ya Mafiati jijini Mbeya ikihusisha magari mawili yaliyogongana uso kwa USO. Ajali hiyo imehusisha basi la abiria mali ya kampuni ya Majinja lililokuwa likielekea Dar es Salaam kutoka jijini Mbeya na gari dogo ambalo halikufahamika Mara Moja.   kutokana na kuharibika sana ambalo dereva wake amepoteza maisha pale pale na hakufahamika jina lake mara moja. Pamoja na hayo shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mlinzi katika kituo cha Oilcom Mafiati amesema kuwa dereva wa basi la Majinja ambaye hakufahamika kwa jina alikuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi kitu kilicho sababisha gari kumshinda na kuparamia gari do go lililokuwa likitokea Mwanjerwa na kuharibika kabisa.   Taarif

SAKATA LA ESCROW: OFISA WA IKULU AHOJIWA NA TUME YA MAADILI

Image
Ofisa wa Ikulu, Rajab Shaban (katikati) akitoka katika chumba cha mahojiano. Tume ya Maadili, katikati ni Jaji Hamis Msumi. Rajab Shaban akitoa ufafanuzi kuhusu kashfa ya kuingiziwa shilingi milioni 80 na James Rugemalira wa kampuni ya VIP. Waandishi na viongozi mbalimbali wakifuatilia yaliyojiri wakati wa mahojiano. OFISA wa Ikulu, Rajabu Shaaban, leo amehojiwa na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyo chini ya Mwenyekiti Jaji Hamis Msumi kuhusu sh. milioni 80 alizoingiziwa kwenye akaunti yake iliyo Mkombozi Bank kutoka kwa James Rugemalira. Kikao hicho kimeahirishwa hadi tarehe 13 mwaka huu ili mamlaka husika ziweze kutoa maamuzi

KIMINI CHAMUUMBUA DADA HUYU

Image
Hiyo ni Picha ya Msichana ambayo siku ya jana imesambaa sana mitandaoni...  Inasemekana alipita maeneo ya Sinza akiwa amevaa kinguo kifupi ambacho kilivuta hisia za wanaume  wakware na kuanza kumzonga zonga wakitaka kumvua kabisa kimini hicho huku wengine wakimchoma vidole sehemu zake za siri. Kwa bahati nzuri alitokea  jamaa  mmoja  mwenye  gari  ambaye  alimchukua  huyu  dada  na  kumficha  ndani  ya  gari  yake..... Baada  ya  Wananchi  wenye  hasira  kali  kutishia  kupasua  vioo  vya  gari, jamaa  aliamua  kutafuta  boda boda ambaye  alimpakiza  na  kutimuka  nae  kwa  kasi  huku  wananchi  wakifukuzia  kwa  nyuma. Baada  ya  jamaa  kuona  wananchi  wanataka  kupasua  vioo  vya  gari  aliamu  kumtosa  huyu  dada  na  kumtafutia  pikipiki   Mpekuzi blog

FORBES: BILL GATES NI TAJIRI NAMBA MOJA DUNIANI

Image
Mmiliki wa kampuni ya kutengeneza kompyuta ya Microsoft, Bill Gates. Bwanyenye mmiliki wa kampuni ya kutengeneza kompyuta ya Microsoft , Bill Gates, ndiye tajiri nambamoja duniani kwa mwaka wa pili mfululizo. Kwa mujibu wa takwimu za jarida la Forbes ambalo huchapiShwa mara moja kila mwaka, Bill Gates ameorodheshwa kumiliki zaidi ya dola bilioni 79.2. Mfanyibiashara kutoka Mexico, Carlos Slim Helu. Mfanyibiashara kutoka Mexico Carlos Slim Helu ameorodheshwa tajiri nambari mbili duniani akiwa na zaidi ya dola bilioni 77.1. Kulingana na jarida hilo, Gates alipata faida kubwa ya dola bilioni $3bn mwaka uliopita. Warren Buffett. Hadi kufikia sasa kuna matajiri 1,826 wenye utajiri unaozidi dola bilioni moja kote duniani hii ikiwa ni ongezeko la mabilionea 181 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Gates ameorodheshwa nambari moja duniani katika miaka 16 kati ya 21 zilizopita. Bwanyenye mwingine kutoka Marekani, W

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE AWASILI MKOANI DODOMA KUANZA ZIARA YA SIKU TISA.

Image
 Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa uwanja wa ndege mjini Dodoma mapema leo asubuhi na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Mh. Adam Kimbisa,tayari kwa kuanza ziara ya siku tisa, yenye lengo la kukagua, kuhimiza miradi ya maendeleo ya wananchi pamoja na kuangalia uhai wa chama, ambapo mara baada ya ku wasili amefanya mkutano wa ndani na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mpwapwa yenye majimbo mawili ya Uchaguzi.Kinana ametokea Mkoani Ruvuma mara baada ya kushiriki mazishi ya aliekuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi,Marehemu Kapteni John Komba aliyezikwa kijijini kwao Lituhi. Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akilakiwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma,Mh.Chiku Galawa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Dodoma mapema leo asubuhi,kulia kwake ni  Katibu wa CCM Mkoa,Albert Mgumba  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.Chiku Galawa mapema leo asubuhi mara baada ya kuwasili

MAAJABU MAZISHI YA KOMBA-TINGATINGA LATUMIKA KUMZIKA

Image
Ndugu na jamaa wakisaidiwa na kijiko cha tingatinga kushusha mfuniko wa zege kwenye kaburi la Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba aliyezikwa katika Kijiji cha LItuhi, wilayani Nyasa, Ruvuma jana. Picha na Emmanuel Herman  Na Joyce Joliga na Ibrahimu Yamola, Mwananchi Nyasa. Safari ya mwisho ya mbunge wa Mbinga Magharibi jana ilihitimishwa saa 9.25 alasiri wakati mwili wake ulipofunikwa na mfuniko mkubwa wa zege uliobebwa na gari maarufu kwa jina la “kijiko”.Haikuwa kitu cha kawaida wakati gari hilo kubwa likishusha mfuniko huo wa zege kwenye kaburi la mwimbaji huyo maarufu wa nyimbo za uhamasishaji za CCM na kiongozi wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT), lakini majonzi yaliwafanya waombolezaji kulichukulia tukio hilo kuwa la kawaida.Safari ya Komba, iliyoanza miaka 61 iliyopita kwenye kijiji cha Lituhi ambako aliazikwa jana, ilikamilishwa kwa salamu mbalimbali ambazo zilielezea ushupavu wa kapteni huyo mstaafu wa jeshi. Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na

NABII AWAPA MIMBA ZAIDI YA WAUMINI 20KISINGIZIO CHA ROHO MTAKATIFU

Image
Wanawake na mabinti waliopewa mimba na nabii huyo. Huko nchini Nigeria wanawake zaidi ya 20 wakiwemo wake za watu na mabinti wamepachikwa mimba na "nabii" wao ambaye amedai aliambiwa na Roho mtakatifu kufanya nao mapenzi wanawake hao. Nabii huyo alifahamika kwa jina la Timothy Ngwu ambaye ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Vineyard Ministry of the Holy Trinity huko Enugu tayari anashikiliwa na jeshi la polisi la jimbo hilo kwa kosa la kuwalazimisha kufanya nao mapenzi na wanawake hao. Mchungaji huyo amedai anatii wito wake wa kinabii na kiroho alioitiwa na kufanya sawa na mapenzi ya Mungu kwa kuwapa mimba yeyote yule aliyechaguliwa na kuwekwa wazi na Roho mtakatifu bila kujali kama mwanamke huyo ameolewa ama la alisema msemaji wa jeshi la polisi Enegu kamanda Ebere Amaraizu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kudai kwamba mwanamke akijifungua mtoto hubakia kwenye huduma hiyo na mzazi wake Taarifa kutoka kwa familia za mchungaji huyo zinasema mkewe a

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA KAPTENI JOHN KOMBA KIJIJINI KWAKE LITUHI

Image
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania kwenda kumzika marehemu Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi. Mke wa Marehemu Kapteni John Komba ,Salome (kushoto) akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu. Watoto wa marehemu Kapteni John Komba wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba yao. Watoto wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yao . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyezikwa kwenye makaburi ya kijiji cha Lituhi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John

WATU WANNE MBARONI AKIWEMO M/KITI WA KIJIJI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YAKIHUSISHA IMANI ZA KISHIRIKINA MKOANI DODOMA

Image
Watu watatu wameuawa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti yanayohusisha imani za kishirikina. Akizungumzia matukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema tukio la kwanza limetokea tarehe 01/03/2015 majira ya saa 01:00hrs katika kitongoji cha Golani, kijiji cha  Masinyeti, kata ya Iduo, tarafa ya Mlali Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la SAIDIA S/O CHAKUTWANGA mwenye miaka 80, kabila Mkaguru, Mkulima Mganga wa kienyeji aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kutobolewa macho. Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina wakimtuhumu marehemu kuwa anazuia mvua kunyesha katika eneo hilo. Pia Kamanda MISIME amesema katika tukio lingine limetokea tarehe 01/03/2015 majira ya saa 02:00hrs katika kitongoji cha Majengo, kijiji cha Ihanda, Kata

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI MKOANI RUVUMA KUSHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU KAPTENI KOMBA

Image
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na   akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma Helena Shumbusho  mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea mkoani humo tayari kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Kada wa CCM na Mbunge wa jimbo la Mbiga Magharibi Marehemu Kapteni John Damiano Komba aliyefariki hivi karibuni katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam, mwili wa Kapteni John Komba unazikwa leo huko kijijini kwao Lituhi mkoani Ruvuma.     Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na   akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali mkoani Ruvuma wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea.     Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndugu Mwigulu Nchemba  na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakisalimiana na wananchi wa Songea  baada ya kuwasili mkoani humo tayari kwa mazishi ya Marehemu Kapteni Komba.    Msanii wa TOT Khadija Omary Kopa akiwasili uwanjani hapo

MAONYESHO YA SIKU YA WANAWAKE YA MKOA WA MOROGORO YAINGIA DOSARI BAADA YA MVUA KUBWA KUNYESHA

Image
  M kurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Bi. Theresia  Muhongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Haji Sajilo ambaye ni Kiongozi msimamizi wa Mipango wa NGO,s ya MOYODEI wakati alipotembelea kwenye mabanda yaliyoharibwa vibaya na mvua iliyonyesha jana jioni. Haya mabanda yalikuwa ni kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyotakiwa kuanza leo jumanne lakini kutokana na maafa hayo maonyesho hayo yamesogezwa mpaka tarehe 5/03/2014 kwa ajili ya ukarabati wa mabanda hayo.(Picha na Pamoja Blog)  M kurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Bi. Theresia  Muhongo akipata maelezo kutoka kwa mama kuhusu mabanda yaliyoezuliwa na mvua iliyokuwa na upepo mkali     Baadhi ya Mabanda yakiwa yameharibika vibaya