Posts

AUNTY EZEKIEL AFUNGUKA JUU YA BABA MTOTO WAKE.....

Image
Aunty Ezekiel aamua kumchana aliemtundika na mimba yake na baba wa mtoto wake…. Hivi aunty anatukanwa sababu ya kuzaa na dancer wa Diamond au sababu ya kuzaa huku ana mume? I think kosa la aunty hapa ni kutokuweka wazi status ya ndoa yake. Im sure keshaachana na mumewe kitambo mpaka akabeba mimba. Kwa kuwa yeye ni star angetoa tamko tu kwamba aliachana na mumewe kipindi cha nyuma ndo kaamua kuzaa na mtu mwingine. Hilo la kuzaa na dancer si mnajitiaga kusema kuwa mapenzi hayachagua kipato sasa mbona huyu mnamsakama kazaa na dancer….lol…. Mwisho wa siku mie naona bora Aunty hata mtoto wake ana baba na mimba yake ina mleaji angalau hata yuko proud na mimba yake… Jamani raha ya mimba iwe na mleaji hata kama hana kipato kikubwa. Raha ya mimba ni mwanamke kushika kiuno na kupeleka tumbo watu walione vizuri. Raha ya mimba kuwa proud na tumbo lako. Maana kuna wengine mimba zao kama za watoto wa sekondari inabidi ajifiche mienzi 9 mtu asiione. hahahhaha… Si mnajua ...

SAMATTA AREJEA LUBUMBASHI, ATETA NA BOSI WA AZAM FC,HIKI NDICHO WALICHOSEMA CSKA MOSCOW

Image
Mbwana Samatta kulia akiwa na Jamal Bakhresa na Thomas Ulimwengu kushoto jana mjini Lubumbashi MSHAMBULIAJI Mbwana Ally Samatta amerejea jana mjini Lubumbashi kuendelea na maisha chini ya utawala wa Moise Katumbi Chapwe, rais wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Samatta akiwa na Mtanzania mwenzake anayecheza naye Mazembe, Thomas Ulimwengu wamepiga picha na mmoja wa Wakurugenzi wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam iliyo ziarani Lubumbashi, Jamal Bakhresa. Na jamal Bakhresa ameituma picha hiyo BIN ZUBEIRY jana akisema amefurahi kukutana na vijana na kuzungumza nao mawili matatu.  Habari zaidi kutoka Lubumbashi zinasema kwamba, klabu ya CSKA Moscow ya Urusi iliamua kuachana na Samatta kwa sasa baada ya kuumia enka akiwa katika wiki ya kwanza ya majaribio. Kiongozi mmoja wa Mazembe ambaye hakupenda kutajwa jina, ameiambia phars blogspot  jana usiku kwamba timu hiyo ya Ulaya ilivutiwa na uwezo wa mshambuliaji huyo wa Tanzania, ...

Sister wa Kanisa Katoliki Ajifungua Mtoto wa Kiume

Image
Utata umeibuka  baada ya sister wa Kanisa Katoliki huko Italy aliyekuwa akilalamikia maumivu ya tumbo na kukimbizwa Hospitali na kujifungua mtoto wa kiume licha ya kuishi katika Jumuiya hiyo ya wanawake watupu.    Sister huyo  mwenye umri wa miaka 31 yupo kwenye kikundi cha masista cha  Santa Chiara  Italy, asili yake ni Amerika ya Kusini, alilalamikia maumivu makali  ya tumbo baadaye alianguka, madaktari walifika katika eneo hilo na baada ya kumfikisha Labour alijifungua.   Watu wengi wameshindwa kuelewa kwa jinsi gani ameweza kupata ujauzito licha ya kula kiapo cha usafi wa moyo na utii.   Tukio linalofanana na hili lilitokea mwaka jana baada ya sister mmoja wa Salvador ambaye umri wake ni miaka 33 ambaye alijifungua mtoto wa kiume na kumpa jina la Papa Francis.

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MAJENGO YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA JIJINI PARIS

Image
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Sallma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wafanyakazi wa ubalozi baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Sallma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na balozi wa New Zealand nchimni Uraransa baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Janua...

HOJA YA DHARURA: WABUNGE WATAKA WAZIRI MKUU NA CHIKAWE WAWAJIBISHWE

Image
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. BAADHI ya wabunge waliochangia hoja ya dharura bungeni leo wamewataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, wawajibishwe. Hayo yametolewa wakati wa kujadili Hoja ya Dharura kuhusu kupigwa kwa baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) akiwemo mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba na baadhi ya wanachama wake juzi huko Mtoni-Mtongani jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mizengo Pinda. SPIKA MAKINDA: Spika wa Bunge, Anne Makinda, alianza kwa kusema kuwa wabunge wachangie hoja hiyo kwa dakika tatu.WAZIRI CHIKAWE: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alianza kwa kusoma ripoti ya serikali kuhusu kilichotokea wakati wa mkusanyiko wa wanachama wa CUF. Alisema jeshi la polisi lilipokea taarifa kuhusu nia ya chama hicho kufanya maandamano na mkutano wa kuwakumbuka wanachama wa CUF waliouawa Januari 27, 2001 huko Zanzibar.  Aliongeza kwamba kutokana na masu...

ANGALIA PICHA- BIBI ANAYEDHANIWA KUWA MCHAWI AKUTWA AKIWA UCHI HUKO MAGEUZI MJINI SHINYANGA

Image
Hapa ni katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembezi mjini Shinyanga pichani ni wakazi wa Ndembezi wakishuhudia tukio hilo la aina yake limevuta hisia za wakazi wa kata ya Ndembezi huku wengine wakidai kuwa bibi huyo ni mchawi kutokana na kiburi alichokuwa nacho huku akidiriki kupiga watu na kwamba mikono yake inaonekana imekatwa panga na imekomaa sana ambapo wataalamu wa mambo walisema huenda bibi huyo huwa anajigeuza Fisi na kutembelea mikono-picha na Kadama Malunde-Shinyanga Bibi(aliyeko pichani) ambaye hajulikani jina wala anakotoka na ndiyo huyo amezua kizaa zaa baada ya kukutwa nje ya nyumba ya mkazi wa mtaa huo aitwaye Suzana Mwandu akiwa uchi wa mnyama hajitambui huku akitembea kwa kutumia makalio yake.Baada ya kukutwa akiwa uchi wasamaria wema waliamua kumvalisha nguo kusitiri mwili ingawa bibi huyo alijaribu kuzivua lakini baadaye kutulia na kuanza kuzungumza maneno yasiyoeleweka -picha na Kadama Malunde-Shinyanga Mwonekano wa mikono ya bibi huyo i...

PICHA KALI NA MITEGO ZA MREMBO HAMISA MOBETO ZINAZOWATESA WANAUME NA MATAJIRI WENYE PESA CHAFU

Image

WEMA SEPETU AKAMATWA NA POLISI, SOMA KISA KIZIMA HAPA

Image
Waandishi Wetu/Amani KATIKA hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata shughuli pevu kumkamata staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye alidaiwa kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali, Amani linakupa mchapo. Timu iliyofika nyumbani kwa Wema Sepetu kumkamta kwa usumbufu aliosababisha kwa majirani. Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo, Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake aliyejulikana kwa jina moja la Neema. Awali, mapaparazi wetu walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema ambaye alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake na kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero. Spika na vifaa vingine vya muziki vilivyotumika katika sherehe hiyo vikiwekwa kizuizini. “Kwa kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga muziki mkubwa katika sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana (usiku wa Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzi...

UKWELI KUHUSU TEVEZ MUME WA AISHA MASHAUZI ALIYEFANYIWA UNYAMA WA KUTISHA MAJUZI SOUTH AFRICA BAADA YA KUJILIPUA NA SEMBE

Image
Mshikaji wa karibu sana wa Tevez ambaye ni mume wa Aisha Mashauzi, amepiga simu sasa hivi kuirekebisha kidogo hii habari anasema ni kwamba Tevez alijilipua na pipi mbili ambazo alikuwa amejipunda nazo na mpunga katia ndani tayari lakini alipofika tu huko chini kwa Mzee Madiba kuna wazee wa kazi waliokuwa na info kwamba kuwachomoka Wazee pale uwanja wa ndege anazo pipi hizo mbili. Wale wazee wakampiga kabali wanamchomoa zile pipi, so alipofika kwa Wazee wa waliompunda lile sembe akawaambia yaliyomsibu, wazee wakam chenjia gear na kumpa kipigo pamoja na kumchomoa uume wake halafu masaa kama 4 baadaye wakagundua kwamba ni kweli aliporwa zile pipi mbili na wazee wa kazi mtaani, imebidi wamrudie wamuombe msamaha na sasa wao ndio wanaomgharamia kumtibu. Mshikaji anasema habari za kusambaa kwa hizi habari zimemkuta Mshikaji Tevez Hospitalini na anataka kujiua so sasa hivi washikaji kibao wapo naye kwa karibu sana kumbembeleza atulize boli U know this is life na kwenye ...

WAZIRI MPYA WA UCHUKUZI SAMUEL SITTA ALIKUTANA ANA KWA ANA NA WADADA WALIOKAMATWA BAADA YA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

Image
Akiwa kwenye ziara ya kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri mpya wa uchukuzi Samuel Sitta jana alikutana ana kwa ana na wadada waliokamatwa baada ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin waliyomeza tayari kuyasafirisha kwenda HongKong kwa ndege ya Emirates. Wadada hao wawili Rehema Ndunguru (32) mkazi wa Sinza mpaka wakati huo alikwishatoa pipi 78 wakati mtuhumiwa mwenzake Moyo Ramadhanialikwishatoa pipi 86 ambapo kazi ya kuwachunguza ilikuwa ikiendelea. Wanawake hao walidai kuwa kama wangefikisha mzigo huo sehemu husika, kila mmoja angelipwa dola 6.500 (sawa na Sh 11,700,000), ambapo wangepokelewa na tajiri wao ambaye hawajui jina lake, ila angewapigia simu.

Mwanafunzi Ajifungua Ndani ya Daladala

Image
Mwanafunzi mmoja wa Shule ya Sekondari ya Keko amejifungua mtoto akiwa ndani ya daladala maeneo ya Mtoni Kwa Azizi Ally, jijini Dar es Salaam juzi  tarehe 23.   Mwanafunzi huyo ambaye hakuweza kupatikana jina lake mara moja, anasemekana alijifungua mtoto huyo bila ridhaa yake wakati akiwa katika harakati za kuitoa mimba hiyo.   Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, msichana huyo anasemekana alikuwa amekunywa madawa makali kwa lengo la kuitoa mimba hiyo ambayo anadaiwa kuificha  hadi pale alipoumbuka mchana wa siku hiyo.   Haikuweza kufahamika mara moja alikopelekwa mtoto huyo baada ya tukio hilo wala hatua alizochukuliwa binti huyo.

HUYU NDIO MTU ASIYE NA USO, ANAHOFU MTOTO WAKE MTARAJIWA ATAFANANA NA YEYE

Image
Baba mtarajiwa amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya kuishi bila kuwa na uso na kwa namna gani anahofia juu ya hali atakayozaliwa mtoto wake mtarajiwa.Anaitwa Mohammad Latif Khatana, 32, kutoka Kashmir, India, hawezi kuona wala kufanya kazi kutokana na ngozi zilizofunika uso wake. Watu humkimbia barabarani kutokana na hali yake huku wakionekana kuogopeshwa nayo.    Kwa sasa ni mwenye faraja kutokana na ukweli kwamba mke wake ni mjamzito wa miezi saba, ila ana hofu labda huenda mtoto wake anaweza kuzailiwa akiwa anfanana naye. Alisema: “Naingoja kwa hamu hii hali ya kuwa baba na kupata furaha ya maisha. Ila nahofu kila siku na kusali ili mwanangu asije kuzaliwa kama mimi.”   Latif, ambaye anaishi milimani na mke wake mwenye miaka 25 aitwaye Salima, eneo la Tuli Bana, ndani ya Jammu and Kashmir, huwa anatembea mpaka Srinagar mara nne kwa mwaka kwa ajili ya kuomba misaada na ili kupata hela.   Alizaliwa na kinundu kidogo kwenye uso ...

DIAMOND THE PLATNUMZ AWARUSHIA BURUNGUTU LA MAMILION MASHABIKI WAKE KWENYE TAMASHA LA TIGO KIBOKO YAO LEADERSCLUB

Image
  Kwa roho nzuri alokuwa nayo Diamond na kwa kutambua mchango wa mashabiki wake aliamua kurudisha fadhila japo kidogo kwa kuwarushia maburungutu ya pesa wakati akiimba kama ahsante kwa mashabiki .. pengine kuna walokuwa hawana nauli za kuwarejesha makwao..wamepata pesa..kuna walokuwa hawajui.maskin ya Mungu kesho wataamkaje..but wamepata kianzio kuna walopata pesa ya kula bata ..etc... side B sasa . kwanza badala ya kupitia mlango husika karuka ukuta(cjaelewa bdo alikua na maana gani)..mashabiki wenu mloweka kuzomea/kurusha chupa baada ya kuona pesa wakasariti badala ya kuzomea wakaishia kuokota na kudaka pesa na mwisho kupiga shangwe tuu.