HOJA YA DHARURA: WABUNGE WATAKA WAZIRI MKUU NA CHIKAWE WAWAJIBISHWE
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
BAADHI ya
wabunge waliochangia hoja ya dharura bungeni leo wamewataka Waziri Mkuu
Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe,
wawajibishwe.
Hayo
yametolewa wakati wa kujadili Hoja ya Dharura kuhusu kupigwa kwa baadhi
ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) akiwemo mwenyekiti wake, Prof.
Ibrahim Lipumba na baadhi ya wanachama wake juzi huko Mtoni-Mtongani
jijini Dar es Salaam.
SPIKA
MAKINDA: Spika wa Bunge, Anne Makinda, alianza kwa kusema kuwa wabunge
wachangie hoja hiyo kwa dakika tatu.WAZIRI CHIKAWE: Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alianza kwa kusoma ripoti ya serikali
kuhusu kilichotokea wakati wa mkusanyiko wa wanachama wa CUF. Alisema
jeshi la polisi lilipokea taarifa kuhusu nia ya chama hicho kufanya
maandamano na mkutano wa kuwakumbuka wanachama wa CUF waliouawa Januari
27, 2001 huko Zanzibar.
Aliongeza
kwamba kutokana na masuala ya kiusalama jeshi la polisi liliona si
vyema kuruhusu maandamano hayo lakini wafuasi wa chama hicho waliamua
kukiuka amri hiyo na kukusanyika huko Mbagala Januari 27, mwaka huu
ambapo walidhibitiwa na polisi.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
MWANASHERIA
MKUU: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju, aliomba hoja
ya dharura kuhusu polisi kuwapiga viongozi na wanachama wa CUF juzi
isijadiliwe bungeni maana suala lipo mahakamani.
TUNDU
LISSU: Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alianza kwa kukataa
wabunge kuchangia mada kwa dakika tatu, akisema Waziri Chikawe alikuwa
amepewa dakika 30, na Mwanasheria Mkuu akipewa dakika 15.
Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Asema
sheria inamruhusu mbunge kuchangia dakika zisizozidi dakika 15 hivyo
Lissu alisema angetumia dakika 15 ila Spika aliingilia kati na kusema
wangetumia dakika 10 na Lissu akakubali.Lissu alisema mrithi wa Werema
(Mwanasheria Mkuu wa sasa, Mh. Masaju) si mshauri wa bunge akiongeza
kwamba bunge likitaka ushauri litamfuata Katibu wa Bunge.
Aliongeza
kuwa ‘waziri wa mapolisi’ (Chikawe) ameongea uongo na kudhihirisha kuwa
kauli ya 'Wapigwe Tu' (iliyowahi kutolewa na Waziri Mkuu Pinda bungeni)
si ya bahati mbaya.Alisema viongozi wa upinzani wanapigwa kwa kuwa kuna
mafasisti serikalini na katika jeshi la polisi akiongeza kwamba kazi ya
polisi si kukataza maandamano bali ni kuyaratibu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Alilijulisha
bunge kuwa hivi sasa wapinzani wana kesi nyingi walizofunguliwa na
polisi kwa njama wanazozijua na amelitaka bunge kuchukua hatua na
kuwawajibisha Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa tukio
hilo la juzi.
MHE.
HABIB MNYAA: Mbunge wa CUF Mkanyageni, Habib Mnyaa, alisema ombi la
kufanya maandamano lilipelekwa tangu Januari 22 na si 27 kama alivyosema
Mh. Chikawe, mwaka huu na maandalizi yakafanyika ila jambo la
kushangaza ni kwamba taarifa kutoka jeshi la polisi kusitisha maandamano
hayo ilitolewa siku yenyewe ya maandamano asubuhi ya Januari 27, 2015.
Alihoji
kwa nini nguvu zinazotumiwa na jeshi hilo kuwapiga wanachama wa CUF
zisitumike kupambana na majambazi wanaovamia vituo kama kule Ikwiriri na
Tanga?Katika kuhitimisha, alitaka jeshi la polisi livunjwe na Waziri
Mkuu ajiuzulu.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
MBOWE:
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alisema
amesikitishwa na taarifa iliyotolewa na Waziri Chikawe bungeni kwani
alivyoongea na baadhi ya maofisa wa polisi makao makuu walimwambia agizo
la kupigwa wafuasi wa CUF lilitoka ngazi za juu.
Akisisitiza
alisema yeye na wenzake wamewahi kushambuliwa mara nyingi na jeshi hilo
lakini pamoja na kuripoti kwenye vyombo husika mpaka sasa hakuna
ufutialiaji wowote uliofanyika.
Asema baadhi ya wabunge wanacheka bungeni maana hawajawahi kujeruhiwa na polisi na wanaouawa na kupigwa na polisi si ndugu zao.
Mbunge James Mbatia.
MBATIA:
Mbunge James Mbatia alisema uamuzi uliofanywa na serikali kuikimbizia
mahakamani kesi dhidi ya Prof. Lipumba si sahii kwani zilikuwa ni njama
za kutaka suala hilo lisijadiliwe bungeni.Hata hivyo, alimshukuru Spika
wa Bunge kuruhusu mjadala ufanyike bungeni ambapo alisema ukweli
utaliweka taifa letu huru, kwani mtu yeyote anayemwaga damu ya mwenzake
ni gaidi na hawezi kuvumiliwa.
Mbatia
aliongeza kuwa vitendo hivyo vilivyofanywa na polisi vinajenga uhasama
ndani ya taifa letu na akawataka waliohusika katika tukio la juzi
wachukuliwe hatua kali za kisheria na za kijeshi kwa kukiuka maadili ya
polisi
Comments
Post a Comment