WEMA SEPETU AKAMATWA NA POLISI, SOMA KISA KIZIMA HAPA
Waandishi Wetu/Amani
KATIKA
hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata shughuli pevu kumkamata
staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye alidaiwa kupiga
muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali, Amani linakupa
mchapo.
Timu iliyofika nyumbani kwa Wema Sepetu kumkamta kwa usumbufu aliosababisha kwa majirani.
Tukio
hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo,
Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake
aliyejulikana kwa jina moja la Neema.
Awali,
mapaparazi wetu walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema ambaye
alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake na
kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero.
Spika na vifaa vingine vya muziki vilivyotumika katika sherehe hiyo vikiwekwa kizuizini.
“Kwa
kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga muziki mkubwa katika
sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana (usiku wa
Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzia saa mbili usiku mpaka asubuhi na
majirani walimfuata Wema mara kadhaa kumtaka apunguze sauti lakini
aliwajibu vibaya.
Polisi akisimamia zoezi hilo kwa kuwawajibisha wahusika (mmiliki wa muziki na mwenye sherehe).
“Njooni mshuhudie wenyewe, tumeita polisi wamkamate,” alisema jirani mmoja.
Mapaparazi
wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi
wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana
kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.
Mwenye sherehe, Neema( rafiki wa Wema Sepetu) akichukuliwa kwenye bajaji.
“Kwa
sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina lake
halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao
katika ofisi za mtendaji, Kijitonyama kwa ajili ya hatua za kisheria,”
alisema.
Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumza
na gazeti hili, mwenyekiti wa mtaa huo, Mzee Haogwa, alithibitisha
kuletewa malalamiko ya Wema na kufika nyumbani hapo ambapo pia alidai
alishangazwa na kitendo cha kuwakuta wanaume tata kwenye sherehe hiyo.
Imeandikwa na Gladness Mallya, Musa Mateja na Hamida Hassan.
Comments
Post a Comment