Posts

AJALI YAUA MTU MMOJA MKOANI IRINGA

Image
baada ya ajali hiyo,  Inavyoonekana kwa nyuma hii ni sehemu ya mbele ya gari hilo Scania lililogongwa kwa nyuma Sehemu ambayo gari hilo dogo liliingia AJALI mbaya iliyohusisha gari dogo aina ya Land Rover Freelander lenye namba T368 CVK na roli la mizigo aina ya Scania lenye namba T346 BRF imetokea usiku wa juzi katika eneo la Lugemba, kilomita kadhaa kabla ya kufika mji wa Mafinga. Taarifa za awali zinaonesha kwamba dereva wa gari hilo jina lake bado halijapatikana alifariki papohapo baada ya gari yake kuingia nyuma ya roli hilo lililokuwa limepaki kandakando ya barabara ya Mafinga Dar es Salaam, akiwa katika mwendo mkali. Mwanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Tumaini aliyekuwemo katika gari hilo amenusurika kufa; binti huyo ambaye pia jina lake halikupatikana amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na kukatika mkono. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo ilitokea majira...

WACHEZAJI 11 WA YANGA KUTOITUMIKIA TIMU HIYO MSIMU UJAO

Image
Kutokana na ripoti ya Benchi la Ufundi iliyowasilishwa mara baada ya kumalizika kwa Msimu wa Ligi Kuu 2013/2014 baadhi ya wachezaji hawataitumikia tena Yanga SC kwenye msimu ujao, wachezaji 11 wamemaliza muda wao na kumalizana na uongozi hivyo wapo huru kujiunga vilabu mbalimbali: Wachezaji hao ni: 1. David Luhende 2. Athuman Idd "Chuji" 3. Geroge Banda -U20 4. Yusuph Abdul -U20 5. Rehani Kibingu -U20 6. Hamisi Thabiti 7. Reliants Lusajo 8. Bakari Masoud - U20 9. Shaban Kondo 10. Abdalllah Mguhi "Messi" U-20 11. Ibrahim Job Hii ni orodha ya awali ya wachezaji ambao hawataitumikia Yanga SC msimu ujao, huku zoezi la usajili likiendelea kujaza baadhi ya nafasi zilizopo kulingana na maelekezo ya Benchi la Ufundi. CHANZO: TOVUTI YA YANGA SC

MISIMAMO YA TIMU ZINAZOENDELEA NA MASHINDANO KWENYE KOMBE LA DUNIA NCHINI BRAZIL

Image

DIAMOND PLATINUMZ ANAVYOLITENDEA HAKI JINA LA SUKARI YA WAREMBO..!

Image
WALIOSEMA ujana ni maji ya moto hawakukosea. Mkali wao kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni msanii ambaye ana idadi kubwa ya msururu wa wanawake ambao ametoka nao kimapenzi ambapo, wapo wanaojulikana na wengine hawajulikani. Nasibu Abdul ‘Diamond’. Leo katika makala haya tunakuletea wanawake ambao kwa nyakati tofauti walibanjuka kimapenzi na Diamond ambao kimsingi kutokana na idadi yake, anadhihirisha jina lake la Sukari ya Warembo. Takwimu zinaonesha kuwa karibu kila mwaka jamaa anabadilisha wapenzi ambapo wanawake wamekuwa wakipokezana vijiti. UPENDO MUSHI ‘PENDO’ Huyu ni msanii wa filamu ambaye alitokea katika Shindano la Maisha Plus. Aliwahi kukiri kwamba alishatoka kimapenzi na Diamond kabla hajawa maarufu kama alivyo sasa, hawakudumu muda mrefu. WEMA SEPETU Ni mlimbwende wa Tanzania na msanii wa filamu kwa sasa. Diamond baada ya kupata umaarufu kidogo, alikutana na Wema na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi jambo lililofanya umaarufu wake kuz...

AMINI WA THT HATIMAYE AFUNGA NDOA NA BONGO MUVI STAR FARIDA

Image
Muimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka THT, Amini Mwinyimkuu jana June 22 ameukacha ukapela kwa kufunga ndoa na msanii Farida Bashir maarufu kama Namcy Vana aliyeimba ‘Kantangaze’. Tazama picha hapa... Amini akiwa na mkewe Ndoa hiyo imefanyika nyumbani kwa Namcy, Magomeni Dar es Salaam. Pongezi nyingi kwa Amin na mkewe

BREAKING NEWS: MWENDO KASI WASABABISHA GARI KUGONGA NA KUBOMOA NYUMBA MIDA HII MKOA WA MANYARA.

Image
 Picha zote na Manyara yetu Blog

BREAKING NEWS: KICHANGA KILICHO FARIKI CHAKUTWA KIMETUPWA KATIKA JALALA LA POSTA ENEO LA MAKAMA YA WILAYA IRINGA.

Image
   Kichanga kikiwa kimetupwa Jalalani na kuonekana asubuhi hii  Humo ndio Kichanga kilipo tupiwa  Eneo ambalo Kichanga kimetupiwa  Askari wakiwa wamefika eneo la tukio  Mashuhuda wakiwa wanashuhudia tukio hilo. Picha zote na Iringa yetu Blog

ANGALIA PICHA SISTA ALIYEUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI

Image
Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi. Kidole cha dereva kilichokatwa kwa risasi. Ganda la risasi likiwa eneo hilo la tukio. Dereva akiwasiliana na jamaa zake baada ya kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa. Wananchi wakiwa eneo la tukio. SISTA wa Parokia ya Makoka iliyopo Kibangu, Dar ameuawa na majambazi yaliyokuwa kwenye bodoboda wakati akiingia kwenye gari akitokea dukani eneo la River Side, Ubungo jijini Dar es Salaam hivi punde. Kabla ya kuuawa sista huyo, dereva wake alipigwa risasi mkononi na majambazi hayo.Chanzo GPL

Waziri Membe azindua Filamu mpya ya 'I Love Mwanza' jijini Mwanza

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akisadiwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, kukata utepe kuzindua filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’ iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo.  PICHA ZOTE/ JOHN BADI WA Daily Mitikasi Blog Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akionyesha CD ya filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa ...