Waziri Membe azindua Filamu mpya ya 'I Love Mwanza' jijini Mwanza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akisadiwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, kukata utepe kuzindua filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’ iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo. PICHA ZOTE/ JOHN BADI WA Daily Mitikasi Blog
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akionyesha CD ya filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akinunua CD ya filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Waziri Membe aliwezesha filamu hiyo kununuliwa na wadau kwa zaidi ya Milioni 50/- katika hafla hiyo. Kulia ni Msanii wa Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akipokea cheti kutoka kwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT, Saimon Macheyeki (wa pili kulia) na Makamu wake, Merigoreth Gervas baada ya kutambua mchango wake katika kuhamasisha maendeleo na mchango kwa vijana wa taifa la Tanzania hasa vijana wa vyuo vikuu, katika hafla ya uzinduzi wa filamu mpya ya ‘I love Mwanza’ uliofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kushoto).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akilisaka rhumba lililokuwa likiporomoshwa na Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, katika hafla ya uzinduzi wa filamu mpya ya ‘I love Mwanza’, uliofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Anayeghani (kulia) ni Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steven Mengele ‘ Steve Nyerere’ na (kushoto) ni Mdau Richard Kasesela.

Comments

Popular posts from this blog