Posts

HII SASA NI FUNGA MWAKA AKAA JUU YA MNARA AKIHITAJI KUMUONA RAIS

Image
  Wanausalama wakipanda juu ya mnara kumnusuru jamaa huyo.     Wananchi wakishuhudia tukio hilo la kufunga mwaka 2013.     Jamaa huyo akiwatuhumu polisi kwa kuwabambikiza kesi wananchi wakati akiongea na wanahabari baada ya kushushwa kutoka kwenye mnara.   Mwanaume mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amepanda juu ya mnara wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom uliopo Ubungo katika eneo la ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  jijini Dar es Salaam na kutaka kujirusha. Mwanaume huyo amedai alitaka kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kudai kufungwa miaka sita jela kwa kubambikiziwa kesi na  polisi. Mwanzoni alikataa katakata kushuka kutoka katika mnara huo akidai mpaka Rais Kikwete afike eneo hilo aweze kumweleza kero yake hiyo japo wanausalama walifanikiwa kutumia mbinu zao kumshawishi ashijirushe na kufanikiwa kushuka naye. (PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL)

TMK WANAUME WAKINUKISHA ILE MBAYA DAR LIVE

Image
Kundi la TMK Wanaume Family likiwapagawisha mashabiki wa Dar Live kwa burudani. MwanamuzikwaWA kundi la TMK Wanaume Family, Amani Temba 'Mhe. Temba' akiwaatisha mashabiki. Mwanamuziki YP naye akiwapa burudani mashabiki wa Dar Live Nyomi ikifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na TMK Wanaume Family. (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)

RAIS DKT. KIKWETE AMTEUA ERNEST MANGU KUWA IGP MPYA

Image
 IGP MPYA ERNEST MANGU NAIBU WA IGP ABDULRAHMAN KANIKI

HILI BASI JIPYA LA AZAMU NIKIBOKO...KILA KITI KINA TV,CHOO NDANI,FRIJI, YANI NI SHIDAAAA

Image
Hakuna Afrika nzima; Basi jipya la wachezaji wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, lililowasili nchini juzi likiwa tayari kusafirishwa visiwani Zanzibar ambako timu hiyo imekwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi. Hili ni aina ya mabasi ambayo yanatumiwa na klabu za Ulaya kama Manchester United, Bayen Munich na Barcelona ambalo kwa Afrika Azam inaweza kuwa klabu ya kwanza kulimiliki. Kitu cha maana Kila siti ina TV Kuna friji Kuna choo

meza ya magazeti leo jumanne

Image

ANGALIA NAFASI ZA KAZI LEO

Image
Sales Person Jason & Co Ltd. Date Listed:  Dec 27, 2013 Email Address:   Click to Email Phone:  No Calls Please Area:  Dar Es Salaam Application Deadline:  Jan 20, 2014 Position Description:   Click Here Application Instructions: Please send Applications to the Email Link above Yard Controller Mukuba Depot Date Listed:  Dec 27, 2013 Phone:  No Calls Please Area:  Dar Es Salaam Application Deadline:  Jan 10, 2014 Position Description: From Daily News December 27, 2013 MOFED  Tanzania Limited is a Freight and Forwarding service provider wholly owned by the Government of the Republic of Zambia under the Ministry of Transport, Works, Supply and Communications in lusaka  Zambia. It is based in the  Kurasini  Area next to the Dock Yard in Dar  es  Salaam. MOFED  Tanzania Limited is hereby inviting applications from suitably qualified person to fill the vacant position of Yard Controller. Job Summary: Responsib

MTANZANIA HUYU KATAJWA KUWA NI MOJA YA WANAWAKE WAREMBO ZAIDI BARANI AFRIKA..!!

Image
Jarida la Glitz Africa limetoa orodha ya wasichana 20 warembo zaidi barani Afrika (20 Most Beautiful Women in Africa) ambapo hata hivyo imetawaliwa na wanawake wa Nigeria na Ghana. Ni Happiness Millen Magese pekee amekuwa mwanamke kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kuingia kwenye orodha hiyo. Orodha nzima ni hii: Leila Lopes (Angola), Vimbai Mutinhiri (Zimbabwe), Oluchi Orlandi (Nigeria), Yvonne Nelson (Ghana), Dillish Mathews (Namibia), Agbani Darego (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria), Stephanie Linus (Nigeria), Genevieve Nnaji (Nigeria), Joselyn Dumas (Ghana), Yvonne Okoro (Ghana), Jackie Appiah (Ghana), Millen Magese (Tanzania), Omotola. Jalade-Ekeinde (Nigeria), Zainab Sheriff (Sierra Leone), Naa Okailey Shooter (Ghana), Nadia Buari (Ghana), Lerato “Lira” Molapo (South Africa), Babalwa “Barbz” Mneno (South Africa), Elham Wagdi (Egypt).

RASIMU YA KATIBA INAWASILISHWA RASMI KWA MHE RAISI JAKAYA KIKWETE,SOMA BAADHI YA VITU VILIVYOMO HAPA

Image
Rasimu ya Katiba hii ni ndefu kuliko ya kwanza ina ibara 271 ya kwanza ilikuwa na ibara 240  -wananchi wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala bora -lugha ya kiswahili lugha ya taifa. -Madaraka ya Rais yamepunguzwa. -wabunge wasiwe mawaziri -kuwe na ukomo wa wabunge -wananchi wawajibishe wabunge  -spika/naibu wasiwe wabunge wala viongozi wa juu wa vyama vya siasa. -kuwepo na jeshi moja la Polisi na Usalama wa Taifa. MUUNGANO 39000 walitoa maoni kuhusu muungano Tanzania Bara,na karibu wote wa Zanzibar walitoa maoni kuhusu muungano -Taasisi nyingi zilipendekeza serikali tatu. Malalamiko upande wa zanzibar Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Tanzania -mambo ya muungano yamekuwa yakiongezeka -kumuondoa rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais Malalamiko Tanzania Bara. -Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamuhuri ya Muungano -Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar Mambo mengi ya Muungan

TASWIRA KUTOKA KARIMJEE KATIKA MAKABIDHIANO YA RASIMU YA PILI KATIBA MPYA

Image
PICHA NA JULIUS S. MTATIRO

SNURA: WEMA NDIYO ALIYENITOA KIMUZIKI

Image
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi ‘Mama Majanga’ ametoa ya moyoni na kumshukuru aliyekuwa rafiki yake wa damu, Wema Sepetu kwa kuwa ndiye aliyembunia vazi la muziki na fedha ya kurekodi wimbo wake wa kwanza. Snura Mushi ‘Mama Majanga’. Wema Sepetu. Akistorisha na paparazi wetu, Snura alisema fedha ya Wema ilihusika kumtoa kimuziki kwani wakati akirekodi wimbo wake wa kwanza, sauti yake iliingia kwenye wimbo huo na vazi lake la shoo ya kwanza alilibuni Wema ambapo mpaka sasa analiendeleza, hivyo anamshukuru sana na anamuombea kwa Mungu ambariki zaidi. “Namshukuru Wema, kwani alihusika sana kwenye wimbo wangu wa kwanza wa ‘Shogaake Mama’ kwani fedha yake ndiyo ilitumika kurekodi wimbo huo pia aliingiza sauti yake kwenye wimbo huo, alinibunia vazi la shoo yangu ya kwanza ambalo ninaliendeleza mpaka sasa,” alisema Snura.