KATIBU TFF AKATAA FEDHA ZA MATAJIRI WA SIMBA, YANGA
KATIBU Mkuu mpya wa TFF, Selestine Mwesigwa ameingia ofisini na mkakati ambao hakuna tajiri yeyote wa Simba wala Yanga atataka kuusikia. Kama mkakati huo utafanya kazi hakuna fedha zozote za mashabiki au wanachama matajiri zitatumika kufanya vurugu za usajili, jambo ambalo huenda likashitua wengi. Yanga na Simba zimekuwa zikifanyiana vurugu kwa kupokonyana wachezaji wakati wa usajili huku wanachama matajiri ambao wengine si viongozi wakitaka kutunishiana ubabe na kuonyeshana nani mwenye fungu. Lakini Mwesigwa ameingia TFF na mfumo ambao utazizuia klabu kutumia fedha yoyote ambayo haitokani na soka kama zilivyozowea kufanya Simba na Yanga ambazo hazina vyanzo maalum vya mapato. Kwa mujibu wa Mwesigwa klabu zote za Ligi Kuu Bara zitatakiwa kujihadhari na matumizi ya fedha ambazo hazitokani na soka katika matumizi yake mbalimbali ikiwemo usajili. Mwesigwa aliliambia Mwanaspoti kwamba, moja ya mambo ambayo atayasimamia ni utekelezaji wa azimio la