JOKATE AWACHAMBUA MADEMU WENZIE
Jokate Mwegelo aka Kidoti ana mengi ambayo ameyasoma kwa baadhi ya wasichana wa Tanzania na yeye akiwa mmoja wao na hivyo amezikusanya sifa hizo kama sampuli na kueleza kile anachokipenda na asichokipenda.
Kama mrimbwende amewasifia wasichana wa Tanzania kwa jinsi wanavyojua kuweka sawa na kupendeza.
“kitu ambacho nakipenda, napenda kwa sababu wanapendeza, wanapenda like..kupendeza, wanajitunza vizuri.” Jokate amefunguka kupitia The Switch ya 100.5 Times Fm.
Lakini kwa upande wa kile ambacho anaona hakiko sawa, uvivu ndio anaoupigia mstari.
“Kitu ambacho sikipendi, ni kwamba…yaani sijui niseme kwamba hawajitumi sanaa. Yaani bado sijaona njaa ile.” Amesema Jokate.
“Kwa mfano ukiangalia kwa mfano Marekani sasa hivi, all top artists ni wasichana, kwa hiyo females wanahustle. Wasichana wakibongo tumezoea sijui kupewapewa au kutafuta kupitia njia za kimkatomkato. That’s a thing ambacho mimi sikipendi na sitakiappreciate maisha yangu yote.” Amefunguka Kidoti.
Amefunguka kuwa wasichana wana fursa nyingi zaidi ya wanaume na kwa kuwa wamepewa akili pia ni vyema wakazitumia kwa kiwango kinachotosha, “make the most of it.”
Lakini pia amekubali kuwa kuna wasichana wengi pia ambao wanaofanya vizuri , wasomi na wanaoweza kujituma na wanaongoza katika nyanja mbalimbali.
Comments
Post a Comment