Posts
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay akabidhiwa Barcode yake
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanamuziki Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua Barcode za Tanzania katika sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini. Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Koti la suti) akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka Profesa Jay. Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi yenye Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku wajumbe wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia. Wanamuziki nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa kujitangaza na kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya Barcode....
Nimebakwa na bosi wangu....Naombeni ushauri wenu ili nijue jinsi ya kukabiliana na Aibu hii
- Get link
- X
- Other Apps
Nime vumilia aibu hii lakini nimeshindwa na hivyo nimeamua niwe muwazi ili niweze kusaidiwa.Sihitaji msaada wa kifedha, bali nahitaji ushauri tu. Ndugu zangu mwenzenu juzi jumamosi nilipatwa na dhahama iliyo pelekea nione aibu kwenda kazini kuendelea na majukumu yangu baada ya kubakwa na mama mke wa mtu. Ilikua jioni bosi aliponipigia simu nakuhitaji msaada wangu wa kumpeleka katika sehemu moja ya starehe . Mimi ni dereva ninaye mwendesha. Nimefanya kazi kwa muda wa miezi sita sasa lakini hakuwahi kunionyesha dalili yoyote ya kimapenzi kwa kuwa anafahamu mimi ni mume wa mtu na yeye ni mke wa mtu. Mume wake siyo mtu wa kushinda sana nyumbani.Ni mfanyabiashara na mara nyingi huwa nje ya nchi kibiashara. Nyumba yao ina geti kubwa na mlinzi mmoja. Baada ya kumpeleka huko mapumzikoni, saa tano usiku alinipigia simu nikamchukue ili nimrudishe nyumbani. Nilimkuta akiwa amelewa sana, hivyo nikamkokota mpaka ndani ya ...
DIAMOND PLATINUM AZUSHA BALAA NDANI YA CHINA
- Get link
- X
- Other Apps
Wakati ile movie ya Temptation iliozua Gumzo Jijini iliyowakutanisha tena Msanii wa muziki Diamond na Mcheza Filamu Wa Tanzania Wema Sepetu ambao waliwahi kuwa wapenzi ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Diamond Na Wema Week End Hii diamond Amekua na Show Ya kukata na shoka huko Guangzhou huku baadhi ya washabiki wakijiuliza mbona hawamuoni Maddam Mkumbuke kuwa Maddam Na Diamond walikutana Hongkong na kwamba tayari Maddam amesharejea nchini, Labda show hiyo ni muendelezo wa Temptation ambayo location yake kuwa inaonekana kuwa Nje ya Nchi. Cheki picha za show hiyo:-
Maiti waendelea Kufufuka mkoani Geita....Huyu alijinyonga mwaka jana na sasa amefufuka yupo hai kabisa
- Get link
- X
- Other Apps
HOFU imezidi kutanda kwa wakazi wa Mkoa wa Geita kufuatia matukio ya watu waliofariki dunia na kuzikwa miaka iliyopita kuibuka wakiwa hai. Mgonda Thomas (22), aliyefariki dunia kwa kujinyonga Mei 28, mwaka jana na kuzikwa siku iliyofuata, Ijumaa iliyopita aliibukia karibu na mlango wa nyumbani kwao akiwa hai. Tukio hilo ambalo bado la moto, lilijiri katika Kijiji cha Rumasa, Kata ya Buseresere, wilayani Chato mkoani Geita. Kwa mujibu wa chanzo, majirani ndiyo waliomshuhudia Mgonda akitembea barabarani saa tisa alasiri hatua chache kutoka kwenye mlango wa nyumba hiyo huku nguo zake zikiwa zimechakaa. Baba mzazi wa kijana huyo, mzee Thomas Msalaba (60) akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema majirani hao ndiyo waliomtaarifu kwamba mwanaye Mgonda alikuwa barabarani. “Niliondoka kwenda kumshuhudia kama kweli ni mwanangu. Nilipofika, nilimchunguza kwa umakini sana na kubaini alikuwa yeye. “Alama kubwa iliyokuwa kwenye mwili wa mwanangu ni kovu kwenye mkono wa...
Hivi ni vyuo 10 vya Tanzania vilivyofutwa na Serikali......Angalia usije ukadanganywa
- Get link
- X
- Other Apps
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imevifuta vyuo 10 ambavyo havikusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) . Naibu Waziri wa wizara hiyo, Philip Mulugo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaama mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuongeza kuwa kufutwa kwa vyuo hivyo ni kutokana na kutokufuata utaratibu wa kusajiliwa. Alivitaja vyuo hivyo ni Media and Research Center, Vision Hotel and Tourism College, East Africa College of Hospitality and Tourism, The Africa Institute of Business Management na Aspiration Training Center, vyote vya Dar es Salaam. Vingine ni Dar es Salaam School of Hair Design, Media and Values Training Institute na Information Technology Training Center vya Dar es Salaam. Pia alikitaja Chuo cha Morogoro School of Medical Sciences cha Morogoro. Katika hatua nyingine, Mulugo alikiri kuwa kuna upungufu katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia bodi ya mikopo. Alisema kun...
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal afungua mkutano wa Mabunge ya SADC mjini Arusha
- Get link
- X
- Other Apps
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia vikundi vya sanaa vya ngoma za aina mbalimbali alipowasili katika Jengo la Ukumbi wa mikutano A I C C mjini Arusha kwa ajili ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC leo Octoba 20, 2013. (Picha na OMR) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbles Lema nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C Arusha, Baada ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC katika ukumbi wa A I C C mjini Arusha leo 20 Octoba 2013. Kushoto Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa wawi kisiwani Pemba Mhe Hamad Rashid nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C Arusha, Baada ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanac...
KATI YA HAWA MASTAA WA KIKE WANAOTINGISHA BONGO NI NANI MKALI?
- Get link
- X
- Other Apps
Wema Sepetu...I just love her voice,lips, skin tone and that caring heart Lulu Michael she knows sifa zake zote ambazo nilikuwa nampa kila siku tukiwa wote... her smile huwa linaninyong'onyeza kabisa. Ana heshima, ni mwelewa na ni Jambazi wa hisia za watu.. akiamua kuiteaka tanzania kwa hisia tu anaweza Jackie cliff.... am sure hapa sipo peke yangu bana kwa kutokwa na udenda... look at her sexy body.... kimwili kisichokomaa!! ana akili na ni mtafutaji katika maisha.. in her Young age she is married and managed to kip her life more personal Tune to 88.4Fm utajua nini kimeniteka kwa huyu mtoto....mke wangu akikosa sauti ya Wema apewe Ya Diva Lovess love... anateka vijana wengi muda wa show yake ukifika... mahusiano yamevunjika sababu ya watu kusikiliza show yake badala ya kula chakula cha usiku na wapenzi zao TUPE MAONI YAKO, NA USISAHAU KULIKE KURASA WETU WA FACEBOOK
WASTARA AUUMIZA TENA MGUU WAKE
- Get link
- X
- Other Apps
MWANADADA anayeendesha maisha yake kwa kupitia filamu za Bongo, Wastara Juma ameumia mguu baada ya kuwekewa mwingine mpya wa bandia huko Nairobi nchini Kenya. Akizungumza na paparazi wetu siku chache baada ya kurudi Bongo, Wastara alisema aliumia wakati akifanya mazoezi ya mguu mpya aliowekewa ambapo kwa sasa anaendelea kuuguza jeraha hilo na amerudi mara moja kwa ajili ya Sikukuu ya Idd, ikimalizika atarejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi. “Nimeshindwa kula sikukuu mbali na watoto wangu ndiyo maana nikaja mara moja japokuwa siko vizuri kwa sababu niliumia kwenye mazoezi ya kutumia mguu mpya huko Nairobi na sasa nauguza kidonda lakini baada ya hapo nitarudi tena Nairobi kwa ajili ya matibabu,” alisema Wastara.
MTOTO WA MIAKA 14 AJIFUNGUA MAPACHA HUKO MOSHI
- Get link
- X
- Other Apps
UKISTAAJABU ya musa utayaona ya firauni ndivyo ilivyotokea kwa mtoto wa miaka miwili ambaye amejifungua mtoto. Mtoto huyo aliyefahamika kama Xiao Feng alijifungua kwa njia ya upasuaji katika hospit ali moja mjini Xuaxi nchini China. Kwa mujibu wa taarifa, madaktari waligundua kuwa mtoto Xiao alikuwa na mimba baada ya kupelekwa na mama yake. Binti wa miaka 14 akiwa na mtoto wake katika Manispaa ya Moshi.Picha ya Maktba. Awali mzazi wake huyo aligundua kuwa tumbo la binti yake lilikuwa kubwa isivyo kawaida hivyo alimpekeka hospitali kujua kulikoni. Nao matabibu hao wakafanya kazi yao ya kumpiga picha za mionzi ya jua ‘x-rays’ na kubaini mtoto huyo alikuwa amebeba mwenzake tumboni. Walimfanyia upasuaji ambao ulimalizika kwa mtoto huyo kuzaa watoto pacha
Mama mwenye UKIMWI amchukua mtoto wa jirani na kumnyonyesha maziwa yake....Serikali yamkamata na kumfunga miaka miwili jela
- Get link
- X
- Other Apps
MWANAMKE mmoja raia wa Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto wa jirani bila ruhusa anakabiliwa na kifungo cha karibu miaka miwili kwa kumwambukiza mtu HIV kwa kukusudia kwa kuwa yeye ni mwathirika. Annie Mpariwa, 39, alifikishwa mbele ya mahakama ya Gaborone wiki iliyopita na kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 24 kuruhusu kipimo cha pili cha HIV kufanyiwa mtoto huyo. Matokeo ya kwanza ya mtoto huyo yalionyesha hana virusi ilhali ya mama huyo yalikuwa na virusi. Mpariwa alikamatwa wiki jana kwa mashtaka ya usumbufu na iwapo mtoto huyo atapatikana na virusi, mashtaka hayo yatazidishwa hadi 'kumwambukiza mtu mwingine HIV kimakusudi.’ Mama wa mtoto huyo wa miezi 14, Nyasha Mironga, alisema kumwona mwanawe akinyonyeshwa na jirani wake lilikuwa ni jambo lililomshtua sana. Kisa hicho kimetokea baada ya kupitishwa kwa sheria mpya ya HIV/Aids inayotoa adhabu kali zaidi kwa wale wanaowaambukiza wengine HIV kimakusudi
WABAMBWA WAKIFANYA MAPENZI KWENYE NDEGE
- Get link
- X
- Other Apps
skip to main | skip to sidebar Wapenzi wawili wamekamatwa kutokana na kitendo cha kufanya ngono ndani ya ndege. Kwenye shitaka lao, wawili hao walipatikana na hatia hivyo kila mmoja alitozwa faini ya $250 kutokana na kitendo hicho kilichotokea wakati ndege hiyo ilipokuwa inatoka Medford, Ore., kwenda Las Vegas. Wapenzi hao walitozwa faini hiyo mnamo June 21, huku ikielezwa, abiria walishuhudia mwanaume aitwaye Christopher Martin, akijiachia kwa raha zake kwa kufanya mapenzi na mwenza wake aitwaye Jessica Stroble, licha ya onyo lililotolewa na wafanyakazi wa ndege hiyo wenza hao waliendelea kufanya yao. Baadaye Martin aliomba msamaha kwa wale walioumizwa au kukwazwa kutokana na kitendo hicho.
Julius Nyaisanga (Mtangazaji wa zamani Radio One na Mkurugenzi wa Abood Media) afariki dunia
- Get link
- X
- Other Apps
Aliyekua mkurugenzi wa Abood media bwana Julius nyaisanga,amefariki dunia huko Morogoro katika hospitali ya Mazimbu... Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na katika Kituo cha Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi. Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN! BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
Ndugu wataka mtoto auawe ili kutoa UCHURO katika familia hiyo......Ni mkasa wa kutisha sana....
- Get link
- X
- Other Apps
MTOTO aitwaye Mwajuma Haji (16) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anayesumbuliwa na ugonjwa wa kusinyaa kwa viungo yuko katika hali mbaya baada ya baadhi ya ndugu kudaiwa kutaka auawe ili kutoa uchuro katika familia. Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Tatu Musa baadhi ya ndugu (siyo wote) wamekata tamaa ya kumuuguza mtoto huyo na kupendekeza heri mtoto huyo akatishwe maisha yake. “Mwanangu haumwi wala hajawahi kuumwa ila ghafla alianza kusinyaa na kukosa nguvu, kinachoniuma baadhi ya ndugu zangu wamekata tamaa wanataka wamuue, waniachie mwanangu,” alisema mama huyo huku akilia mfululizo. Mwandishi wetu amemshudia mtoto huyo akiwa amesinyaa viungo kiasi cha kutoweza kufanya kitu chochote zaidi ya kulala. Mama mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa alijifungua mtoto huyo akiwa na afya njema lakini alipofikisha umri wa miaka mitatu hali ikabadilika na viungo vyake kuanza kusinyaa. Mama huyo amedai kwamba kutokana na hali hiyo hakuweza...
TATIZO LA HARUFU MBAYA UKENI LIJUE VYEMA NA NJIA ZA KULIKABILI
- Get link
- X
- Other Apps
Tatizo la uchafu ukeni Leo tutazungumzia tatizo linalowasumbua wanawake wengi, tatizo la kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano, ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis. Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bacteria au fangasi wanaoleta magonjwa. Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi z...
MCHUNGAJI ADAI KUWAUA SHARO, KANUMBA
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘The Great’. Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605 Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. Steven Kanumba. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab w...
LULU AELEZEA MIPANGO YA KUOLEWA KWAKE
- Get link
- X
- Other Apps
STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekataa kabisa suala la kuolewa kwa sasa akidai moyo wake haupo tayari kwa tendo hilo. Lulu alifunguka hayo Jumatatu iliyopita katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa kupitia Runinga ya East Africa ambacho humpa nafasi staa kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake na sanaa kwa jumla. Wakati mahojiano hayo yakiendelea, mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho anayefahamika kwa jina la Muba, alimtupia Lulu swali ambalo lilimtaka aeleze utayari wake endapo mtu akijitokeza na kutaka kumuoa. “Sitaki kuolewa kwa sasa, muda wa kuolewa haujafikia. Ukifika nitafanya hivyo lakini kwa sasa sipo tayari kuolewa,” alisema Lulu. Aidha, Lulu alikiri kuwa licha ya kutokuwa tayari kuolewa lakini amekuwa akipata usumbufu mkubwa wa kutongozwa na wanaume. Aliainisha kuwa alikuwa akitongozwa kabla na baada ya kutoka Segerea alipokuwa akishikiliwa kwa kesi ya kifo cha aliyekuwa mpenzi wake, marehemu Steven Kanumba. “Watu wanan...
Mwanaume akatwa Uume wake na mwanamke aliyemvamia kwa lengo la Kumbaka...Bofya hapa ujionee
- Get link
- X
- Other Apps
Hii ni stori fupi ya mwanaume aliyekatwa uume wake na mwanamke ambaye alimwingilia kwa lengo la kumbaka... Taarifa toka eneo la tukio nchini Kenya zinaarifu kuwa mbakaji huyo alimvamia mwanamke huyu majira ya saa nane usiku kwa kuvunja dirisha na kisha kuingia ndani huku akiwa amejihami kwa kisu kikali... Alipoingia ndani, alimvaa mwanamke huyu ambaye ni mke wa mtu ( mumewe alikuwa safarini ) na kuanza kumkaba kwa lengo la kufanya naye mapenzi huku akimtishia kumchoma kisu endapo atapiga kelele... Mwanamke hakuwa na jinsi, ilibidi akubaliane naye ili kuunusuru uhai wake.Wangali wakiwa katika tendo huku jamaa akiwa amenogewa, yule mwanamke alimgeuza kwa ujasiri na kufanikiwa kuviminya VIAZI MVINGO VYA MWANAUME... Baada ya kuviminya viazi mviringo ( Korodani ), yule kaka hakuwa na jinsi na ndipo mwanamke yule alipoitumia nafasi ile kuikata MAMBO (Mhugo ) ya ...
CHADEMA yamwaga nyaraka za siri kumjibu Zitto Kabwe...Yawataka Msajili wa vyama na CAG wawajibike
- Get link
- X
- Other Apps
Hii ni taarifa ya Chadema: Kutokana na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali kuwa vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku kutoka serikalini havijawasilisha taarifa yake ya mapato na matumizi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kipindi cha miaka minne mfululizo, yaani kuanzia mwaka 2009/2010- 2012/2013. CHADEMA tunapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo juu ya taarifa hizo; i. Kuwa taarifa hizo sio sahihi na hazina ukweli kuhusiana na CHADEMA labda kwa vyama vingine, hii ni kutokana na ukweli kuwa tulishawasilisha taarifa zetu za fedha kwa msajili wa vyama vya siasa na zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011, 2011/2012 na hili linathibitishwa na barua ya msajili wa vyama vya siasa yenye Kumb.Na . CDA.112/123/01a/37 , ya tarehe 04 september 2012. Iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa (nakala imeambatanishwa). Aidha, hesabu za mwaka wa fedha zilizokaguliwa za 2009/20...