Nimebakwa na bosi wangu....Naombeni ushauri wenu ili nijue jinsi ya kukabiliana na Aibu hii
Nime vumilia aibu hii lakini nimeshindwa na hivyo nimeamua niwe muwazi ili niweze kusaidiwa.Sihitaji msaada wa kifedha, bali nahitaji ushauri tu.
Ndugu zangu mwenzenu juzi jumamosi nilipatwa na dhahama iliyo pelekea nione aibu kwenda kazini kuendelea na majukumu yangu baada ya kubakwa na mama mke wa mtu.
Ilikua jioni bosi aliponipigia simu nakuhitaji msaada wangu wa kumpeleka katika sehemu moja ya starehe .
Mimi ni dereva ninaye mwendesha. Nimefanya kazi kwa muda wa miezi sita sasa lakini hakuwahi kunionyesha dalili yoyote ya kimapenzi kwa kuwa anafahamu mimi ni mume wa mtu na yeye ni mke wa mtu.
Mume wake siyo mtu wa kushinda sana nyumbani.Ni mfanyabiashara na mara nyingi huwa nje ya nchi kibiashara. Nyumba yao ina geti kubwa na mlinzi mmoja.
Baada ya kumpeleka huko mapumzikoni, saa tano usiku alinipigia simu nikamchukue ili nimrudishe nyumbani. Nilimkuta akiwa amelewa sana, hivyo nikamkokota mpaka ndani ya gari tukaondoka.
Nyumbani tulikuta mwanae mdogo na house girl wamelala hivyo akaniomba nimpeleke chumbani kwake kwa madai kwamba alikuwa hawezi kutembea kwa sababu alizidisha pombe.
Nilimvuta mpaka chumbani kwake maana sikuwa na jinsi ya kukataa.Cha ajabu nilipomfikisha chumbani yule mama alipata nguvu akafunga mlango.
Alisimama pale mlangoni na kuanza kuvua nguo zake.Nilipojaribu kumvuta ili nitoke, yule mama alitishia kupiga kelele.Akanambia nitulie tulale, vinginevyo atapiga kelele kwamba nataka kumbaka.
Nikifikiria getini kuna mlinzi na nipo ndani ya chumba cha bosi wangu kiasi kwamba mlinzi akija ni lazima aamini kwamba nilikuwa nataka kumbaka..
Akili ya haraka haraka ilinituma nimkubalie tu, lakini nikakumbuka pia sina hata kipande cha kondom.
Mpekuzi naomba niishe hapo maana nashindwa kuendelea kuelezea.Kwa kifupi ni kwamba nilifanya mapenzi na yule mama bila kinga yoyote.
Mlinzi alijua kila kitu tulichokifanya maana niliondoka asubuhi.Siwezi kuendelea na kazi tena maana mumewe akirudi ni lazima aambiwe kila kitu..
Kinachoniuma ni kwamba kazi nimeipoteza na huenda afya yangu nayo ikawa imeingia dosari.Tangu juzi sijafanya mapenzi na mke wangu.Nasubiri miezi mitatu ipite ili nikapime.
Lakini namwelezaje mke wangu kwa kipindi chote hicho ili anielewe.Na mimi kama mumewe naanzaje kumweleza kwamba nimebakwa? Ndoa yangu itakuwaje?
Naomba msaada wa ushauri toka kwenu na kwa wasomaji wenu.
Comments
Post a Comment