Posts

Picha tano za dada yetu UFOO SARO baada ya kunusurika kuuawa na Mpenzi wake

Image
Ufoo Saro baada ya kufanyiwa upasuaji huo. Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufo Saro, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake Kibamba jijini Dar es Salaam leo na mchumba wake ambaye pia alimuua mama yake na kisha kujiua. Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji. Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati akipelekwa wodini.

BAADHI YA PICHA ZA DIAMOND ZINAZOMTESA PENNY HIZI HAPA

Image
Baada ya habari kuenea kuwa Diamond PLatnumz amerudiana na Wema walipokuwa Malaysia katika moja ya show zake na Platnumz kukanusha habari hiyo kupitia website yake, hatimaye BK imepata picha nyingi za Diamond na C.E.O wa Endless Fame Wema Sepetu wakiwa kwenye pozi tofauti tofauti za kimahaba nchini humo. Baadhi ya picha hizo, moja inawaonesha Diamond na Wema wakiwa wamevaa Mapajama (nguo za kulalia) sehemu kama hotelini hivi na nyingine ikimuonesha Diamond akim-kiss Wema wakiwa kitaa .   Lakini Diamond ni real boyfriend wa Penny…

GARI YATEKETEA KWA MOTO MBELE YA ASKARI WA USALAMA BARABARANI

Image
Gari aina ya HIACE inayofanya safari zake mkoani kilimanjaro katika root ya Moshi-Marangu kila siku, Juzi asubuhi tarehe 13/10/2013 Majira ya saa mbili asubuhi iliwaka moto maeneo ya YMCA ikiwa inatokea Marangu na abiria wapatao 18, ila hakuna madhara kwa abiria. Ikiwa katikati ya mji kabisa pasipo kuwa na msaada wa haraka kutoka FIRE iliyojirani na eneno la tukio na hata msaada wa  askari wanaosaidia katika maeneo hayo, kwa mujibu wa Mwanahabari wetu FRANK aliyeshuhudia tukio ilo, hapakuwa na msaada wa haraka toka FIRE mpk baada ya dakika kadhaa kuteketea kwa gari hilo ndio walipokuja kusaidia.  Askari wa barabarani wakigeuka kuwa waandishi wa habari na kusahau majukumu yao kama wanavyoonekana  hapa askari wakiwa wanajadili jambo mara baada ya kutokea ajali hiyo katika maeneo wakiwa na mashuhuda mbalimbali hapa ni FIRE mara baada ya kufika na kukuta gari likiteketea walianza kuzima moto katika gari hilo kama wanavyoonekana. NGUDU WANANCHI PANAPOTOKE...

JACKLINE WOLPER YU HOI HOSPITALINI

Image
Msanii wa Filam Tanzania ajulikanae kwa jina la Wolper yuko hoi Hospitalini huku akiomba Dua kwa wapenzi wake wamuombee ili apone haraka. Wolper ameripot taarifa za kuumwa kwake katika akaunti yake ya facebook na kuainisha ugonjwa unaomsumbua ni Maralia na ujumbe huo umesomeka hivi:

MSANII PHARRELL WILLIAMS ALIPOFUNGA NDOA" angalia PICHA

Image
Msanii na Producer Pharrell Williams amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Helen Lasichanh na kufanya sherehe ndogo kwenye boti huko Miami, Florida. Wapenzi hao wamechagua boti lililoitwa "Never Say Never" na Kwenye sherehe yao wasanii wakubwa kama Busta Ryhmes, Justin Timberlake, Usher na Robin Thicke walikuwepo. Fahamu kuwa Pharrell Williams na Helen Lasichanh wamekuwa na mahusiano kwa muda mrefu sana na zao lake ni mtoto wa kiume mwenye miaka 4 ' Rocket'

Rais Kikwete apendekeza NYERERE DAY iwe siku aliyozaliwa na siyo siku aliyofariki dunia...Una Maoni gani juu ya hili

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amependekeza kuwa siku ya ‘Nyerere day’ inayoadhimishwa October 14 kila mwaka, iadhimishwe siku aliyozaliwa mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Rais kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wananchi mjini Iringa katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru, iliyoambatana na kumbukumbu ya baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere. Amesema anapendekeza siku hiyo iwe siku ya kuzaliwa ili watu washerehekee kwa furaha, wakikumbuka hotuba za Mwalimu. Endapo mapendekezo ya rais yataungwa mkono, Nyerere day itakuwa April 13, kwa kuwa mwalimu alizaliwa siku hiyo mwaka 1922. Una mtazamo gani juu ya pendekezo hili? -timesfm

Mtu mmoja akutwa amejinyonga mjini Morogoro....Jaribu kumwangalia vizuri, huenda ni ndugu yako au rafiki yako

Image
Mtu ambaye jina lake halikufahamika mara moja amekutwa amejinyonga usiku wa kuamkia leo mjini Morogoro.Chanzo cha mtu huyu kujinyonga hakijafahamika. Askari aliyekuwepo eneo la tukio alidai kwamba askari wa doria waliokatiza kwenye eneo hilo majira ya saa 10 usiku walishuhudia mwili wa mtu huyo ukining'inia juu ya mtu na kuanza juhudi za kuutoa mwili huo. Askari akipanda juu ya mti kwaajili ya kuushusha mwili wa marehemu.

Taarifa kuhusu afya ya mwandishi aliyepigwa risasi ( Ufoo Saro ), tarehe ya mazishi ya mpenzi wake aliyempiga risasi na siku ya mazishi ya mama yake mzazi

Image
Hali ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro aliyejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi mbili juzi huko Kibamba, Dar es Salaam inazidi kuimarika na jana alizungumza na Mwananchi na kusema; “Sijambo, naendelea vizuri.” Ufoo, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hata hivyo, anazungumza kwa shida kutokana na kukabiliwa na maumivu baada ya kufanyiwa upasuaji juzi. Mwandishi huyo amehamishiwa katika wodi ya upasuaji wa moyo huku kiongozi wa wodi hiyo, ambaye alikataa jina lake kuandikwa, akieleza kuwa walimhamishia huko ili apate muda zaidi wa kupumzika. “Watu wanakuja kwa wingi kumjulia hali, tuliona tumhamishe ili apumzike,” alisema kiongozi huyo. Kabla ya kupelekwa katika wodi hiyo, Ufoo alikuwa katika wodi ya Kibasila na baadaye alihamishiwa katika Chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU). Ufoo alipigwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi ambaye alijiua baaday...

HIKI NDIO CHANZO kuhusu kupigwa risasi kwa mtangazi wa ITV ( Ufoo Saro ) ambaye mama yake naye AMEFARIKI

Image
Alfajiri ya leo, mtangazaji wa ITV anayejulikana kwa jina la Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua. Akizungumza na mpekuzi wetu, kamanda Wambura ambaye ni kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo. Kamanda wambura amedai kuwa mwanaume aliyetenda mauaji hayo ni mchumba wake na alikuwa anafanya kazi katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika kitengo alichokuwa akifanyia kazi. Kwa mujibu wa Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili awasuluhishe Baada ya usuluhishi kuanza na kuonekana kuwa tatizo liko kwa mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanae na ndipo alipotoa bast...

MASANJA MKANDAMIZAJI AKIWA ANAKULA BATA NDANI YA JIJI LA OBAMA

Image

TANZANIA, RWANDA NA BURUNDI NA BENKI YA DUNIA ZASAINI MKATABA WA MRADI WA UMEME RUSUMO

Image
  Waziri wa Fedha, Wizara ya Fedha Tanzania Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa katikati akisaini mkataba wa mradi wa umeme wa Rusumo, kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi Burundi Mhe. Tabu Manirakiza, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Mkakati na Uendeshaji ukanda wa Afrika Bw. Colin Bruce Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi Eva Valerian – Washington DC   Naibu Katibu Mkuu, Umoja wa nchi za Afrika Mashariki Dkt. Enock Bukuku akimfafanulia jambo Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula walioko pembeni ni baadhi ya walihudhuria mkutano  wa kusainiwa kwa mkataba wa Rusumo.   Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mgimwa akikabidhiwa mkataba na Mkurugenzi wa Mkakati na Uendeshaji ukanda wa Afrika Bw. Colin Bruce mara baada ya kusaini.   Mawaziri wa  Fedha wa nchi tatu, kutoka  kushoto Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Burudi Mhe. Tabu Manirakiza, Waziri wa Fedha wa Tanzania Dkt. Wiliam Mgimwa, Mkurugenzi wa Mkak...

Matokeo ya Nani Mtani Jembe kuanza kutangazwa leo

Image
Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Rage akiwakabidhi wafanyakazi wa TBL Mbeya wanaoshabikia Simba baada ya kuwashinda wanaoshabikia Yanga katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager inawashindanisha mashabiki wa Simba na Yanga. Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Mariam Martin zawadi baada ya timu yake kushinda mchezo wa kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya Wafanyakazi akinamama wa TBL Mbeya wakishindana kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Bahati Msokwa zawadi baada ya timu yake kushinda mchezo wa kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nan...

Balozi wa Oman amuaga Rais Kikwete

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Oman nchini anayemaliza muda wake Mhe.Yahya Mousa Al Bakary ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Balozi huyo alikwenda ikulu kumuaga Rais(picha na Freddy Maro)   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Oman nchini anayemaliza muda wake Mhe.Yahya Mousa Al Bakary ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Balozi huyo alikwenda ikulu kumuaga Rais(picha na Freddy Maro)